Mengi awaponda wanaomwandama

Serikali inatakiwa siku zote ijali wazalendo wake. Serikali inatakiwa iwawezeshe wazalendo wake (indeginous empowerment) in all spheres, especilly owenrship of the economy. I doing so, policies and Acts must safe guard the long term and sustainable efforts of the citizens, especially indegionous. Je Tz inafanya hivyo??? Iko tayari kutetea interest za fisadi kwa kuwa anachangia siasa badala ya kutete interest za locals ambao wanachangia na kutetea sustainable and real economy??? Leo hii mifisadi yote na jamaa zao wa karibu wana uraia zaidi ya moja, sasa huyo ni sustainable!!!! ???Nachelea kusema hatuna serikali ya watanzania kwa manufaa ya watazania wazalendo, bali tuna serikali ya mafisadi tu. Samahani sana kwa wale ambao nawaudhii ila msimamo wangu ndiyo huu na si msimamo wa Uongozi wa Jamii Forums, its Founder, and any other member.

Ningekuwa naweza ningebadili uraia, au kuhamia nchi nyingine, ningekubali kuwa uhamishoni kama akina Kambona. Ila tu huko ugenini ningekuwa treated as a fifth class resident wakati Tanzania mgeni is a first class citizen (not resident), kuna tofauti hapo tena kubwa tu. Tunahitaji mapinduzi ya haraka.

Mkuu hasa hilo ndo shida kubwa, yaani watanzania tumejengewa dhana ya kujidharau sisi wenyewe, na hata kudharau vitu tunavyo vifanya wenyewe 'products' na kuamini vya wengine na hao wageni kwamba ni bora kuliko sisi! Nadhani mchawi wetu ni aliye pandikiza hii sumu!

Ndiyo maana RA kijana mdogo anaipeleka puta serikali nzima iliyo sheheni watu wazima na akili zao na umri wa kutosha!

Kwa mfano, hela za EPA alikwapua bilioni 40, akalamba 30 bil, 10 bil tu ndo alizo kigawia chama ambacho sasa amekigeuza kinga yake na kuigeuza dola nzima vibaraka! Pesa yetu, kakwapua, kawagawia kiduchu.. bado anawapelekesha na watu wazima wana haha usiku kucha akiguswa! Haiingii akilini kwakweli!
 
Kazungumza j'pili kanisani mkoani kilimanjaro na kuombewa na askofu wa kanisa la kilutheri jimbo la moshi askofu Shao na kuonyeshwa kwenye taarifa ya iTV saa mbili usiku 1/6/09
 
Hatari iliyopo juu ya ujasri wake in kwamba ataangamia yeye mwenyewe na kuwaangamiza wengine ambao siyo walengwa kama tunavyoona kwa wale wanaojitoa muhanga; ninamfanaisha Mengi na Mrema katika harakati zake za miaka iliee..!!. Unaweza kuwa na nia njema katika kutekeleza jambo fulani lakini ukakosa mipango sahihi katika utekelezaji wake. Nia ya Mrema haikutimia juu ya Taifa hili. Mimi sifurahishwi na taarifa zinazotolewa juu ya watu wachache kutumia raslimali za Taifa letu kwa manufaa yao, lakini wasiwasi wangu ni harakati zilizoanzishwa na Mzee Mengi kutokuzaa matunda. Mimi nafikiri huu sio wakati wa kuendelea kumtafuta mchawi aliyetufikisha hapa tulipo, badala yake Mzee Mengi angeendelea kuwahamasisha vijana katika elimu na uhamasishaji katika uzalishaji mali na kutoa mbinu mbadala zilizomfikisha yeye hapo alipo. Ninaamini kinachotusumbua ni huu ujinga wetu na unyonge uliotawala katikati ya watanzania wengi.

Mkuu,
Ni kweli unayoyaongea, anachokifanya sasa hivi hakina tija yeyote na anashindwa kufanya walau quick evaluation na change course. He has engaged himself in the political wrangles huku akiwa hana platform ya kufanya hivyo zaidi ya kutegemea uwezo wake binafsi wa kipesa.

I guess kwamba sasa hivi anahitaji kutumia pesa na resources nyingine nyingi ambazo mwisho wa siku hazitatatua tatizo lililopo. Mimi binafsi, sina tatizo naye yeye kama yeye, bali the way ambavyo anavyoendesha hili swala ninabaki ninapatwa na mshangao mkubwa sana. Inawezekana kuwa tayari amejenga misimamo fulani, lakini hiyo pekee haitoshi, ni muhimu aweke mazingira ya kupata ushauri na kuukubali hata kama ni tofauti na misimamo ambayo tayari ameijenga.

Leo hii unakwenda mahali ambapo watu wamekualika kwa harambee, unadhani wataweza kukuambia ukweli kama umekosea? Wakuambie umekosea ili iweje, wakose pesa yako? ...atasifiwa sana... kuambiwa kila ambalo angependa kuambiwa.


Pia nina wasiwasi kuwa huenda washauri wake si wa kweli au kama ilivyo kawaida ya matatizo yetu binafsi, hatutaki kumwambia mfalme yuko mtupu. He has business, he is successful, basi kama nia ni kuwasaidia hasa wale wanaohitaji angefanya kama wanavyofanya matajiri wengine wakubwa duniani wanaoheshimika, anzisha foundation weka pesa yako pale angalia jinsi inavyowafaidisha wale wanaohitaji.

Angalizo:Haya ni maoni yangu binafsi

"Discover that the most powerful way to help those
you love is to lead by example - and realize
you're leading by example all of the time."

- Joe Caruso: Authority on human development and transformation thinking
 
Mengi: Nimeanza kuandamwa sasa

• Afanya kufuru kwa kumwaga milioni 400/- Hai

na Mwandishi Wetu

MWENYEKITI Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi, ameeleza kusononeshwa kwake na hatua ya baadhi ya viongozi wa serikali na taasisi zake, kumsakama tangu alipotaja majina ya watu aliodai kuwa ni mafisadi papa.

Akizungumza wakati wa ibada iliyofanyika juzi katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri la Kisereny wilayani Hai, mkoani Kilimanjaro, Mengi alisema baada ya kutaja majina hayo, alianza kuandamwa na baadhi ya mawaziri, vyombo vya dola na taasisi za serikali.

Katika ibada hiyo ya Sikukuu ya Pentekoste, mgeni rasmi alikuwa Mhashamu Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini, Dk. Martin Shayo na iliambatana na hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la Shule ya Msingi Kisereny, uzinduzi wa zahanati ya Ndekyo na Chama cha Akiba na Mikopo (SACCOS) cha Kisereny.Huku akishangiliwa na umati wa waumini wa kanisa hilo lililopo katika eneo la kijiji alichozaliwa, Mengi alimtaja waziri wa kwanza kumwandama kuwa ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Sophia Simba.

Mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Hai, Dk. Norman Sigalla na Mbunge wa Hai, Fuya Kimbita (CCM), Mengi alimtaja waziri mwingine aliyemwandama baada ya kutaja mafisadi papa kuwa ni Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, George Mkuchika, aliyesema alimwita mbaguzi wa rangi.

Mwenyekiti huyo wa IPP, alisema mbali ya mawaziri hao kutoa kauli hizo, pia wahariri wa magazeti yake anayoyamiliki, walihojiwa na Msajili wa Magazeti wa Idara ya Habari.


Huku waumini wa kanisa hilo wakiwa kimya, Mengi alisema yeye mwenyewe pia aliitwa na kuhojiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), ikidai alivunja sheria ya utangazaji kwa kutaja majina ya watu kuwa ni mafisadi papa, na kwamba hatua hiyo iliashiria ubaguzi wa rangi.

Mengi ambaye alikuwa mgeni mwalikwa kwenye hafla hiyo, alivitaja vyombo vingine vya dola vilivyomwandama kuwa ni pamoja na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), ikimtaka apeleke vielelezo.

Kwa mujibu wa Mengi, pia aliitwa na maofisa wa Jeshi la Polisi, linaloongozwa na IGP, Said Mwema, chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani, inayoongozwa na Laurence Masha, wakimtaka apeleke vielelezo vya tuhuma zake.

“Nimeitwa na Kamati Ndogo ya Ulinzi na Usalama wa Taifa ili kuhojiwa juu ya tamko langu kuhusu ufisadi. Yote haya yamefanyika pamoja na kwamba kuna kesi mahakamani juu ya jambo hili.

“Tukumbuke kwamba Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alikwishatoa tamko bungeni kuwa wote waliotajwa, kama wanaona hawakutendewa haki, waende mahakamani. Sasa ni nani ana tamko la mwisho katika hili? Ni mawaziri, taasisi za serikali, vyombo vya dola ama Waziri Mkuu?

“Kama raia wa Tanzania, vyombo vya dola ni moja ya mategemeo yangu ya kunilinda mimi na mali zangu, kama raia wengine, lakini pamoja na kusakamwa na vyombo hivyo, nasema siogopi. Ulinzi wangu unatoka kwa Mwenyezi Mungu, pili utatoka kwa Rais Jakaya Kikwete ambaye naamini hatakubali kuona sitendewi haki, na tatu ulinzi wangu utatoka kwa Watanzania wanaochukia ufisadi, hasa masikini na wanyonge.

“Hawa hawana fedha nyingi, ama madaraka, lakini wana nguvu ya sala na umoja bila kujali dini zao,” alisema Mengi na kushangiliwa na waamini wa kanisa hilo.

Alisisitiza kuwa, hatarudi nyuma katika msimamo wake wa kupiga vita ufisadi, kwani anaamini rushwa ikiachwa bila kukemewa, wananchi watagawanyika katika makundi mawili; la watu wenye kipato na madaraka na la watu masikini.

“Watanzania wenzangu wanaochukia umaskini, wanaochukia ufisadi, ndugu zangu waumini, nawaomba mniombee na tuimbe wimbo namba 59 katika kitabu cha ‘Mwimbieni Bwana’, usemao ‘Kazi ni yako Bwana’,” alisema.

Hatua ya Mengi kutoboa siri ya kusakamwa kwake mara baada ya kutaja majina ya aliowaita mafisadi papa, ilitokana na mahubiri ya Askofu Dk. Shao, aliyeunga mkono harakati zake katika vita dhidi ya ufisadi.

Askofu huyo alimtaka Mengi asikatishwe tamaa na wajanja wachache, ambao wamekusudia kurejesha nyuma juhudi za kujiletea maendeleo.
“Taifa letu limegubikwa na mafisadi wachache, wapo Watanzania wenzetu kama Mengi, wamekuwa mstari wa mbele kupinga vitendo vya kifisadi, lakini wanakwamishwa na baadhi ya viongozi walioko madarakani, tukemee kwa pamoja.

“Mwaka huu na mwaka ujao ni vipindi vya uchaguzi mbalimbali, kuna watu wamejaa choyo, wivu, chuki na ubinafsi miongoni mwetu, hakika watu hao ni wabaya kwa maendeleo ya taifa, msiwachague,” alisema.

Dk. Shao aliomba wananchi kutomchagua kiongozi asiye na ujasiri na uthubutu, na kujitoa kwa ajili ya wengine.

Alisema, Mengi hataki urais wala hana nia ya kuwania kiti hicho, wala uongozi wa aina yoyote, lakini amejitoa kusaidia wanyonge, na rafiki zake ni masikini, walemavu, wajane, wanaoishi na virusi vya VVU pamoja na wenye matatizo mengine ya kijamii.

Mara baada ya kumalizika kwa ibada hiyo iliyodumu kwa zaidi ya saa sita, Mengi alitoa sh milioni 400 kwa ajili ya vikundi na miradi mbalimbali inayosimamiwa na kanisa hilo.

Kwanza alitoa sh milioni 100 kwa ajili ununuzi wa jengo linalotumika kama zahanati ya Ndekyo, pia alitoa sh milioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa shule ya kisasa ya msingi ya Kisereny na sh milioni 100 kwa ajili ya SACCOS ya Kisereny.

Pia alitoa sh milioni 100 kwa ajili ya kwaya ya kanisa hilo, akina mama wanaoishi na VVU, wajane na watoto yatima.

Hii habari nimeiona soon baada ya kuweka post yangu nyingine hapo juu.

Ninachotaka kusema kuwa ni vigumu kwa mtu ambaye unategemea atakusaidia katika shida uliyonayo mkononi ukakupa ushauri ambao unahisi utamkera. Mara nyingi anayekuja kukusaidia utamnyenyekea na kila analosema utaitikia na tena utamsifu bila ya kujali hali yeyote ile.
Hebu angalia Askofu anajisahau hadi kutoa maneneo kama haya

"Alisema, Mengi hataki urais wala hana nia ya kuwania kiti hicho, wala uongozi wa aina yoyote"

Ni nani kamtuma amsemee Mengi maneno hayo? au ni kwa sababu anajua kuwa Mengi amekuja kwa ajili ya tendo hilo hapo chini,

"Mengi alitoa sh milioni 400 kwa ajili ya vikundi na miradi mbalimbali inayosimamiwa na kanisa hilo.

Hapa ndipo ninapoona kuwa washauri wake hawafanyikazi yao sawasawa, Kitu ambacho angeweza kufanya ni kwenda na kutoa misaada yake na kufanya ibada yake tu, au kama alikuwa amepewa ugeni rasmi basi asingeongelea habari za ni nini kilifanywa na nani, Kikwete atamfanyia nini na mengine mengi.

Tumsaidie huyu mzee kwa kumpa ushauri ambapo utakuwa endelevu na si vinginevyo.


Angalizo: Haya ni maoni yangu binafsi
 
Last edited:
Hivi SERA hii mpya ni kwa watu binafsi tu ama? Vipi kuhusu TBC1,TBC TAIFA,TBC FM,HABARI LEO, DAILY NEWS? Imekaaje hiyo?
 
Big up Mengi kwa kupania kuinusuru TZ mikononi mwa manyang'au,tunakuunga mkono,usikatishwe tamaa na mawaka wa mafisadi na mafisadi papa.
 
Mkuu,
Ni kweli unayoyaongea, anachokifanya sasa hivi hakina tija yeyote na anashindwa kufanya walau quick evaluation na change course. He has engaged himself in the political wrangles huku akiwa hana platform ya kufanya hivyo zaidi ya kutegemea uwezo wake binafsi wa kipesa.

I guess kwamba sasa hivi anahitaji kutumia pesa na resources nyingine nyingi ambazo mwisho wa siku hazitatatua tatizo lililopo. Mimi binafsi, sina tatizo naye yeye kama yeye, bali the way ambavyo anavyoendesha hili swala ninabaki ninapatwa na mshangao mkubwa sana. Inawezekana kuwa tayari amejenga misimamo fulani, lakini hiyo pekee haitoshi, ni muhimu aweke mazingira ya kupata ushauri na kuukubali hata kama ni tofauti na misimamo ambayo tayari ameijenga.

Leo hii unakwenda mahali ambapo watu wamekualika kwa harambee, unadhani wataweza kukuambia ukweli kama umekosea? Wakuambie umekosea ili iweje, wakose pesa yako? ...atasifiwa sana... kuambiwa kila ambalo angependa kuambiwa.

Pia nina wasiwasi kuwa huenda washauri wake si wa kweli au kama ilivyo kawaida ya matatizo yetu binafsi, hatutaki kumwambia mfalme yuko mtupu. He has business, he is successful, basi kama nia ni kuwasaidia hasa wale wanaohitaji angefanya kama wanavyofanya matajiri wengine wakubwa duniani wanaoheshimika, anzisha foundation weka pesa yako pale angalia jinsi inavyowafaidisha wale wanaohitaji.

Angalizo:Haya ni maoni yangu binafsi

"Discover that the most powerful way to help those
you love is to lead by example — and realize
you're leading by example all of the time."
— Joe Caruso: Authority on human development and transformation thinking
Hueleweki msimamo wako ni upi,uwe muwazi la utaonekana bandera fuata upepo tu.Sema msimamo wako ni upi katika vita juu ya ufisadi?
 
Namuomba sana Bw. Mengi amwambie rafiki yake JK anashughulikie mafisadi bila kujali chochote_Nchi lazima iendeshwe kwa utawala wa sheria. kama kuna watu wana tuhuma nzito washughulikiwe mara moja kabla waTz hatujakosa imani na serikali yetu.
 
Mkurugenzi mtendaji wa IPP Bw Reginald Mengi amewaponda Jeshi la Polisi, Takukuru, kamati ndogo ya usalama wa taifa kwa kumuhoji na kumwagiza apeleke ushadi juu ya mapapa aliowataja katika kituo chake cha Tv cha ITV, vile vile amewaponda Sophia Simba kwa kumkejeli kuwa amechemka na Bw Mkuchika kwa kumuita kuwa ni racist, amehoji ni nani yuko juu ya sheria baada ya waziri mkuu kutoa tamko la kwamba mahakama iachiwe ifanye kazi yake.
Habari kwa ufupi.
MJ
Mkuu Mengi hakuwaponda Takukuru alichoongea Mengi hiki hapa
[ame=http://www.youtube.com/watch?v=OjuK2pgNmM8]YouTube - Mengi na vita zidi ya ufisadi papa[/ame]
 
Mkuu Mengi hakuwaponda Takukuru alichoongea Mengi hiki hapa
YouTube - Mengi na vita zidi ya ufisadi papa

As a broke Tanzanian young man! I support na ntakuombea Mengi kama uyasemayo yana nia ya kweli na kwa kuwa niliyoshuhudia tangu vita dhidi ya ufisadi uanze kuna dalili nyingi kwamba serikali haipo upande wako! there i said it!!!..Coz i dont understand why a man with your kind of money in a poor country like tanzania would want to fight the government of the day..ungeweza kula maisha tuu kimyakimya...its either arrogance or a calling...for now i will follow the later.
 
mengi yuko straight forward kawataja mawaziri husika na kahitaja serikali mara kwa mara kuwa inahusika na huu ndio ujasiri ambao unatakiwa TZ, watu wangapi wanaweza kusumbuliwa kama mengi anavyosumbuliwa na bado kuendelea mapambano hii ni wazi kuwa jamaa siyo mbinafsi, angeweza kukaa kimya na kuendelea kuiona TZ inaliwa mpaka mwisho, baadhi ya viongozi wangefurahi sana magazeti yake yafungiwe lakini wanajua ni sawasawa na kuzima moto kwa petroli....
wakati umefika wa TZ kumuunga mkono mengi
wakati wa TZ kukataa kununuliwa na kina papa
huu ni upumbavu wa aina gani papa anachukua bil 40 anakupeni nyinyi 10 yeye anabakia na 30
chama kikiwa hakina hela anajidai anatoa hela zake je ni hizo hela ni zake au ni zetu ccm amkeni, hivi watu wa ccm wana akili kweli inakuwaje wananyanyaswa na pesa zao/zetu wenyewe
 
Hueleweki msimamo wako ni upi,uwe muwazi la utaonekana bandera fuata upepo tu.Sema msimamo wako ni upi katika vita juu ya ufisadi?

Msimamo wangu? katika misimamo ipi au mingapi? hebu niorodheshee hiyo misimamo niione?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom