Ushauri nasaha kwa Mzee Mengi Watanzania hatuna haja ya kutaka kujuwa Urafiki wake wa karibu na watokea zamani kwa Rais Kikwete sisi hautusaidiii ni yurafiki wenu na mnajuwana wenyewe au mtajuwana wenyewe kwani Mtaka nyingi nasaba hupata mwingi msiba wahenga walinena. Towa ushahidi Mahakamani wa Mafisadi PAPA nasi tuko Nyuma yako, lakini ikiwa sio kweli umesimama kwa ajili ya Kukashifu wenzako kwa mitizamo ya kiushindani wa Kibiashara basi tarajia kupata laana ya Walalahoi tuliowengi ndani ya Nchi yetu, tumechoka kusikia kila uchao nyimbo hii ya UFISADI Sisi tuliowengi tunasubiri kuona hatuwa dhidi yao zikichukuliwa harakiza kwenda Mahakamani hivi sasa ili haki itendeke na ionekane kuwa inatendeka.
Hivi kweli wewe kutoka ndani ya moyo wako unaona kweli alio wataja Mengi si mafisadi wanao liangamiza taifa letu?
Anza na nafsi yako kuona ukweli ulipo.. hizo siasa na propoganda ndizo zimetufikisha hapa tulipo, haya majamaa ni mafisadi mabaya sana na mabinafsi makubwa ambayo hayafai kabisa katika jamii ya wanyonge watanzania wano taabika kwa kufisadiwa kila kilicho chao!