Bavicha Geita: Tunajifunza mambo haya maisha na kifo cha Bw Mengi

Mhere Mwita

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
235
1,275
Kwa niaba ya baraza la vijana chadema (Bavicha) wilaya ya Geita ninapenda kutoa pole kwa wanafamilia, wa IPP media Limited na Familia ya Reginald Abraham Mengi kwa kuondokewa na Mpendwa wao, Baraza kwa ujumla limepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo chake, maana sote tunatambua kwamba Bw Mengi alikuwa ni mdau Muhimu kuwahamasisha vijana kuondokana na umaskini.

Maisha pamoja na Kifo cha Bw Mengi kimepata Mafunzo mawili makuu ambayo sisi kama vijana tunatakiwa tujifunze kutoka kwake, ili tuweze kuziishi na kuzienzi Falsafa zake za kujikwamua kwenye Lindi la umasikini, ili tuweze kufikia matamanio na ndoto zake za mda mrefu za kuwaona vijana wa kitanzania ndio wanashikiria uchumi ya nchi yetu.

*Funzo Katika Maisha yake*
________________________________
Bwana Mengi ni kijana mmoja wapo ambae alikuwa hautukuzi umaskini, ufukara pamoja na unyonge kama watawala walivyokuwa wanataka ndio maana Leo nchi nzima inaskitika, katika kipindi ambacho anaamua kupambana na umasikini, katika kipindi hicho watanzania wengi waliona kwamba umaskini ni sifa, ishara ya uzalendo pamoja utakatifu. Katika kipindi kile cha chama kimoja utajiri ulikuwa ni dhambi moja kubwa sana.

ukiwa tajiri hauwezi ukawa kiongozi maana wewe sio Mzalendo na utaitwa majina Mengi kama vile Mnyonyaji kuwadi wa Mabepari, Fisadi pamoja na Mwizi lakini Bw Mengi aliyakubali majina hayo yote na kupambana ili afikie ndoto zake ndio maana Leo hii sote tunamlilia na tumuombea apumzike kwa amani.

*Funzo katika Kifo chake*
__________________________________
Bw Mengi katika kifo chake ametuachia funzo kubwa sana sisi Bavicha wilaya ya Geita tumeona viongozi waandamizi wa serikali wamesema neno juu yake Mfano Rais wa wanyonge Dk Magufuli amesema "Nimesikitishwa na taarifa za kifo cha Mzee na Rafiki yangu Dkt. Reginald Mengi. Nitamkumbuka kwa mchango wake mkubwa ktk maendeleo ya Taifa letu na maono yake yaliyopo ktk kitabu chake cha I Can, I Will, I Must. Poleni wanafamilia, wafanyakazi wa IPP na Jumuiya ya Wafanyabiashara"

Hapa funzo tunalipata kama vijana Kama Dk Mengi angepweteka na kushangilia kauli za kuutukuza umaskini na Unyonge Mfano "Mimi ndio rais wa Maskini Mimi ndio rais wa wanyonge" Mara nitawafanya Malaika waishi kama mashetani leo hii tusingemfahamu wala kauli hii kutoka kwa Rais tusingeiona.

Niwaase vijana wenzangu tusiutukuze umaskini maana umaskini hauna Rafiki umaskini hauna raisi wala Mbunge umaskini ni ukatili Mfano Dada zetu wanaotupa watoto ni kwa sababu ya umaskini umaskini ni utumwa ndio maana chadema katika Sera yetu mabadala kwenye Misimamo kumi na mbili ya kisera kuna *Uchumi wa soko jamii* serikali kushirikiana na sekta binafsi kuinua uchumi wa nchi hapo ndio tutakuwa tumemuenzi kwa vitendo Dk Mengi.

Baraza la vijana linamshukuru Mwenyezi Mungu kwa Zawadi ya Bw Mengi tunaomba Serikali iruhusu Demokrasia ili kuwepo na Mazingira mazuri ya kufanyia Biashara ili tumuenzi Bw Mengi. apumzike kwa Amani.

Imetolewa na :~
Mhere Sylvester Mwita
M/kiti Bavicha (w) Geita
 
Kumbe "bwana Mengi" alikua kijana? Mwenyekiti sugu umeharibu vijana hakyanani
 
Kumbe "bwana Mengi" alikua kijana? Mwenyekiti sugu umeharibu vijana hakyanani
Kwa akili zako chache unadhani Mengi hajawahi kuwa kijana. Andiko la vijana limejieleza wazi, wakati wa ujana wa Mengi ilikuwa dhambi kuwa tajiri, ukiwa tajiri unaonekana wewe siyo mzalendo. Mpaka hapo hujaelewa nini!?
 
Kumbe "bwana Mengi" alikua kijana? Mwenyekiti sugu umeharibu vijana hakyanani
KUMBE hebu unaposoma jitahidi kutafakari kwanza hivi hizo akili zoko zinauwezo wa kuchuja kumbe ndio maana mnaitwa wanyonge shauri yenu
 
Back
Top Bottom