Meneja wa bar mjini ni mtu mkubwa Sana

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
19,579
44,825
Mameneja wengi wa bar kubwakubwa na za Kati hawajitambui potential yao unakuta meneja anakuzingua kisa umevunja glass. Meneja mjanja wa bar hatakiwi kukosa mtu wa kumuazima million 2 kwa sababu bar wanaingia watu wengi wengine Wana pesa nyingi kuliko hata mmiliki wa bar sema tu bar sio biashara zao.

Bar wanakuja watu wenye michongo mpaka ya million 400 ni suala la meneja kuhakikisha anawajua wateja wake wote na deal wanazofanya kwani unaweza ukafaidika na sekta mbalimbali. Mteja unakunywa mpaka laki tano kwa mwezi kwenye bar Ila siku umeishiwa pesa mfukoni muhudumu anakudai huna anamuita meneja Cha kushangaza meneja na mwenyewe badala atumie akili anakuwa upande wa muhudumu wanakuchangia wanakuabisha wengine mpaka simu wanaichukua.

Meneja wa bar ukitumia akili unapata pesa kuliko hata mwenye bar au hata meneja wa vibank kwa mfano case ya umejikuta huna hela mfukoni meneja anatakiwa awe neutral akunyenge Fulani uachie simu Ila baadae anakurudishia kimya kimya wewe kwa akili zako utaona meneja ni mwana hutaacha kuja kunywa pombe kwenye hio bar meneja mwingine hata motisha hatoi kila siku anakuona Ila anakulia buyu hata kukuagizia bia tatu hajawahi.
 
Leo umeamua... Unaporomosha threads kama mvua
Leo ndo sijalewa toka mwaka uanze nimetulia home Kisha Nina safari sitaki hangover..siku zote hizi huwa nakula maisha nawakaanga ndo maana nimegundua ukiwa busy kupata pesa na kula pesa unakuwa mvivu kuandika thread unakuwa msomaji msomaji tu kiaina.
 
Itakua kadi ya ATM imemezwa sasa kakosa hela ya kutoa lock na mameneja wa bar hawasomeki teh teh teh......
Hahaha mkuu me huwa sikopagi pombe ovuo kwa mwaka labda mara mbili tena nishakunywa sana ndo zakuongeza
 
Mameneja wengi wa bar kubwakubwa na za Kati hawajitambui potential yao unakuta meneja anakuzingua kisa umevunja glass.Meneja mjanja wa bar hatakiwi kukosa mtu wa kumuazima million 2 kwa sababu bar wanaingia watu i.

Kipindi 40/40 inaitwa 40/40 kweli kuna meneja pale nilimuelewa na alielewa wateja sana! Ipo siku tumekula kilaji pale na washikaji, bata likakolea tukajikuta mfukoni hatuna kitu na tunataka kuendelea! Nikamwita meneja, alipofika nikamweleza nia!

Kiroho safi akamwita mhudumu na kumpa maelekezo atuhudumie hadi tutakapotosheka bili apewe yeye!
Kesho yake saa nne akanipigia simu niende nikapate supu atalipa!
Nilipofika akanipa ile bill nikaclear....!!

Huu utaratibu uliendelea, asipotuona anatupia simu hata kama hatuna hela tuende... yule jamaa sijui alihamia wapi...na alipoondoka kiwanja kikawa hovyo kweli!!!
 
Back
Top Bottom