kakuruvi
JF-Expert Member
- Sep 2, 2009
- 770
- 256
Kama umejifunza biblia vizuri sina shaka umewahi kuona maneno haya, ''mene mene tekel peres'' maana yake '' Mungu ameuhesabu ufalme huu, umepimwa katika mizani na kuwa umepungua, watapewa Wamedi na Waajemi" cha ajabu ninachotaka kuzungumza hapa ni kuwa maneno hayo yaliandkwa ukutani na kiganja cha mkono usio na kiwiliwili kwenye sherehe kubwa ya mfalme tajiri (Belteshaza) mwenye kiburi na asiyemtukuza Mungu na mwenye kunyanyasa watu, usiku huo huo mfalme huyo aliuawa na watu wake walitekwa na utawala mwingine wa Wamedi na Waajemi ukasimama.
Kuna masuala magumu yanayokabili taifa letu sasa halafu kuna viongozi wanatumia akili zao zote na nguvu zao zote kutetea waliosababisha maafa yanayotukabili, watu wengi wanaumia kwa ajili yao bila huruma, nakumbusha 'mkono wa Mungu unaandika mioyoni mwao kuwa wanapimwa katika mizani na uongozi wao umefika mwisho' Mungu ibariki Tanzania.