Mimi siungi mkono uchepukaji katika maisha yangu, na napenda kuwa mfano wa mume mwema kwa mke wangu. Ila nataka nitoe mfano au somo kwa faida ya wote wenye ndoa waume na wake, kuna mdada ana ndoa yake ya miaka zaidi ya 5. katika maisha yake ya ndoa alikuwa anashangazwa na hali anayoikuta chumbani kwao kila arudipo toka kazini, tofauti na alivyoiacha anapokuwa anaenda kazini. Kwa bahati nzuri siku moja alipata dharura ya kurudi nyumbani maana kuna kitu alikuwa amesahau nyumbani, basi alimfumania mume wake na mke wa mtu mubashara kitandani kwao na huku mtoto wa huyo mama akiwa anacheza sebuleni bila wasi. Yule mke wala akufanya ugomvi, bali alitoka chumbani akaenda kukaa sebuleni , yule mgoni wake alivaa haraka haraka na kumchukua mwanae na kuondoka mume akampigia magoti , mkewe akamsamehe maisha yanaendelea mpaka leo mwaka wa tatu na wakaongeza na watoto 2 zaidi.
Sasa kama angechukulia hasira inamaana angemfaidisha yule mchepuko , angevunja ndoa yake siku moja tu katika maisha yake yote, aliyoitunza.
Muda mwingine huitaji kufanya maamuzi ya jazba kwenya jambo kubwa kama ndoa. Ndoa si jambo dogo au rahisi kama watu wachache wanavyolichukulia kwa wepesi.
Hebu jiulize wakati, mnachumbiana , na wakati mnachangisha michango ya arusi yenu, na viapo vyenu pale madhabahuni mbele ya watumishi wa MUNGU na familia na jamii kwa ujumla iliyoudhulia arusi yenu!!!!
Ukisha tafakari hayo , jiulize tatizo lipo wapi mpaka yanatokea hayo, mwisho jiulize kweli nimwachie mchepuko avunje ndoa yangu kirahisi hivyo? Jibu hapana.
Basi , samehe maisha yaendelee ...
Hakuna atakayeuchua uume wa mumeo na kuondoka nao.
Msipende kuwapa watu faida zisizowastaili.