The Hunter
JF-Expert Member
- Dec 25, 2010
- 1,048
- 307
Nimesoma magazeti ya leo, na kuona bwana mkubwa unavyotishia nyau, kwamba liwalo na liwe utapata ushindi wa kishindo katika nec ijayo
Sikushangaa sana lakini nilishtushwa na tambo zako ambazo kiukweli zinaweza kukutokea puani muda si mrefu na ukawa mpole kama lile Tingatinga la mtera, kumbuka Pedeshee Sumaye na ukwasi wake wote aliishia kulalama kama jibwa koko...mkumbuke Mama makelele na kiherere mwenyeji wa upareni aliishia kufyata kimya na mpaka wa leo haamini kilichotokea
Membe kushinda NEC iliyopita isikufanye uamini wewe ni kidume, kumbuka ccm ina wenyewe ambamo wewe haupo.
Ngoja nikukumbushe kitu bro
. Bunge la 2005-2010 lilipokaribia ukingoni Bw. Sita, alijigamba, alijiaminisha kwamba atachaguliwa tena bunge la 2010-2015, matokeo yake unayakumbuka aliishia kulialia, kupiga magoti na kuomba msamaha, maana hata kadi ya chama ilikuwa ndo inaondoka, mwishowe wenye chama walikutana Msoga wakachinja ngamia na kunywa bia baada ya kumkomesha.
. Bunge hilohilo alitokea Bw. Malecela, akajitapa mbelembele kwamba atahakikisha Sita anapita, matokeo yake hata yeye mwenyewe hakupita tuu kwenye kura za maoni
Nakutakia mafanikio bro, hivyo siamini kama kuwatambia watesi wako ni njia ya kuwashinda, zaidi ni njia ya kuwaamsha na kuwakumbusha kufanya lolote wawezalo ili usipite, kama vijiji vilihongwa mpaka Nagu akapita itakuwa hiyo Nec ambamo wenye njaa ni wengi kupindukia na wote si wasafi.