Nyetk
JF-Expert Member
- Feb 28, 2012
- 1,648
- 1,696
Hn. Dr. Harrison Mwakyembe
Wengi wa wanaofuatilia siasa za Bongo walianza kumsikia Dr. Mwakyembe alipokuwa mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki mwaka 2001 – 2005, au sana sana baada ya kuwa mbunge wa Kyela 2005 ktk awamu ya kwanza ya Rais Kikwete. Hata hivyo bwana huyu alianza kujulikana zaidi kisiasa mwaka 2001 alipoanza kuwa mshauri wa kisheria wa CCM, Mjumbe wa Kamisheni ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (2001 – 2005), Kamanda wa vijana CCM wa Mkoa wa Dar (2004 – 2009) na baadaye kuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM (2006 – 2010).
Nyota ya Mwakyembe iling’aa kwa kasi ya ajabu akiwa mbunge wa CCM alipoteuliwa kuwa mwenyekiti wa Tume ya Bunge kuchunguza kashifa ya Richmond ktk awamu ya kwanza ya serikali ya Mzee Kikwete; pale aliposimama kidete yeye na Spika wa Bunge wa wakati huo Mzee Samweli Sita (R.I.P.) kuanika ukweli wenye hatari kubwa na uliowagusa viongozi wa juu wa serikali ya awamu ya nne. Hii ilipelekea waziri mkuu wa wakati huo Bwana Edward Lowasa ambaye alikuwa swahiba mkubwa na wa siku nyingi wa rais Kikwete kuhusishwa moja kwa moja na ufisadi wa Richmond na Kikwete akalazimika kumtosa, na yumkini ukawa ndiyo mwisha wa uswahiba wao.
Ktk awamu ya pili ya Kikwete Dr. Mwakyembe ambaye ktk “ranks” za kitaaluma za Chuo Kikuu cha Dar aliishia kuwa “Senior Lecturer in Law” aliingia kwenye Baraza la Mawaziri kama Naibu Waziri wa Kazi na baadaye akawa Waziri wa uchukuzi…. Watu walijiuliza maswali: “kwa nn Kikwete huyu ampe uwaziri bwana Mwakyembe? Je, ni kwa sababu anataka kumnyamazisha? Au kwa sababu anataka kuvuna nyoyo za watanzania ambao wanamwona Mwakyembe kama shujaa ndani ya CCM? Au, ...? Au,? Au…?
Leo hii ktk awamu hii ya tano ya Mzee Pombe baadhi ya maswali haya ya wakati huo juu ya Mwakyembe yameanza kujibika, na yumkini “graph” yake imegota kilele na imeanza kushuka kwa kasi ya ajabu. Watu husema ‘urua humharibu mtu’. Kwa lugha ya kigeni ‘power corrupts!’
Style ya utawala wa Mzee pombe haina kanuni na ndo maana wote wanaopenda madaraka na wanataka kuwepo kwenye serikali hii wanapata shida sana maana hawajui wafanyeje ili wamfurahishe mkulu. Mh. Juma Nkamia bungeni jana alihoji: “Kwenye press conference ya Roma Mkatoliki Waziri alienda kufanya nini?
Hata sisi tunajiuliza maswali: Mwakyembe anatetea kubaki tu kwenye utawala hata kama sote tunaona JPM ameshaanza kumdanadana anatafuta uelekeo wa kumpigia golini? Au ni ile athari ya sumu aliyotangaza hadharani marehemu Sita kwamba alipewa na mafisadi? Kwa vyo vyote vile sad news ni kwamba Honorable Mwakyembe anaelekea kuegesha.
-----------------
Mchangiaji onyx ameleta sahihisho kwamba Bwana Mwakyembe hajawahi kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM (CC), bali Mjumbe wa Halimashauri Kuu ya CCM (NEC). Naomba radhi kwa mkanganyo wa tafsiri. Nyetk