Membe to sue Mwananchi & Tanzania Daima?

Mbona wakitudanganya kwenye kampeni awatuombi msamaha?

Dowans wamechakachua no msamaha.

Wanasheria kama wanajua sheria tuna kesi ya dowans tunaomba taaluma zao na sio kwenye misamaha ya waheshimiwa.
 
Kama kawaida yao "alinukuliwa vibaya na vyombo vya habari" vyote viwili....., imekula kwake!
 
Kumbe mende oho sori membe hajakomaa kisiasa kutoa maneno ya busara aliyokaririwa akiyatoa! Mi nlidhana tunaweza kumpata mwenye hekima kumbe bado,duh! Sasa 2015 magufuli atapambana na nani ndani ya ccm,mana jamaa kasharudi nyuma!
 
hii nchi bana..
 

Attachments

  • kp.jpg
    kp.jpg
    66.1 KB · Views: 46
nina wasiwasi wameanza kubana waandishi bcs on mapinduzi day nothing about mapinduzi on those 2 newspapers. dirty politics and it is going to get ugly.
 
The contents of your publication in their very plain meaning tells the public and international community that our client, both as a person and as a government minister, has no confidence with the Police Force and the entire government machinery entrusted with peace and security of the country and also that as a minister responsible for foreign affairs he failed his duty to address the government position on the Arusha issue to the international community until compelled by the Ambassadors. Due to your publication, our client's good working relations with the Police Force and his reputation in the government and members of diplomatic corps has been seriously injured. As a result of your publication, our client's reputation has been harmed, and lowered, and you have exposed him to hatred, contempt and ridicule in the eyes of the right thinking members of the society.


Please let us go slow on this one. I can fully understand the reaction of the members in relation to the contents of the letter.

But we should narrow down the issue to only three or four issues;

1) Whether Membe said the words that are complained of.

2) Whether the words complained of are defamatory

3) Whether Membe's reputation has been lowered among the right thinking members of the society.

4) Whether the words compalined of were maliciously communicated.


I understand that someone else may formulate the issues either widely or narrowly. But for the purpose of discussion the issues as posed may be of help to guide the contributors.

Now, some people have confirmed that Membe said those words. They heard him on TBC1 uttering those words. He, through his lawyers, says that he didnt say those words. he goes further saying that the words have been maliciously published. For some reasons he believes Mwananchi (and may be Tanzania Daima) are malicious!! And that, his reputation has been dented!!

The question then is, does he believe that the police did act ethically? That the force used was reasonable and necessary? He unfortunately must make his stand known. If he says he had informed the ambassadors that the Prime Minister will give a statement then has the latter given a statement? Who is lying now? Everyone has given a statement, Wassira, Kagonja, Makamba, Chitanda etc. But the PM has not given a formal statement. Not one that I know of.

That is beside the point, getting back to our issues, are those words defamatory? I think the words were making him a hero where he is none. He is such a coward!! He is just like the rest of the pack. And, if at all he did not utter those words Mwananchi MUST apologize to us readers and NOT him!! We readers should be the ones complaining and filing a suit for believing Mwananchi while this guy is just a coward. He can not stand up and say what he believes to be the truth rather he hides behind the Prime Minister. If he believes that the police acted ethically and with mandate he should say it to contradict what Mwananchi reported.

And the lawyer who wrote the letter, has he read what the Tanganyika Law Society said in its statement?? If the TLS said that the force used was excessive and it was wrong for the police to act as they did then why take up such a case? Legal right?

I feel like I am loosing it slowly, labda niandike kiswahili. Hivi Membe ameshushiwa heshima mbele ya nani?? Viongozi wenzake wa CCM na Mabalozi? Heshima ipi anayoilinda kwa nguvu zote hizo? Kwa nini tusiamini kwamba yeye ndie amejivunjia heshima (kama alikuwa nayo) kwa wananchi kwa kushindwa kuweka wazi msimamo wake badala yake kukimbilia kukana kwamba hakusema maneno hayo!! Kama alikuwa anajua suala la Arusha halimuhusu alikuwa na sababu zipi 'out of courtesy' kuwaeleza mabalozi kwamba Waziri Mkuu atatoa tamko wakati mpaka sasa hivi hakuna tamko lililotolewa na Waziri Mkuu?? Alikuwa anawadanganya ili iweje? kwani si Mabalozi hao hao walielezwa na Jakaya Kikwete kwamba kilichotokea Arusha ni bahati mbaya na hakitajirudia?? Hilo tamko la Waziri Mkuu lilikuwa kuhusu nini? Kwamba kilichotokea Arusha si bahati mbaya na kitajirudia hivyo wawe na subira???

Membe anachukiwa na Mwananchi (na Tanzania Daima) kwa sababu zipi? Kwanini wawe malicious?? Anataka aombwe msamaha kwamba amewekewa maneno mdomoni ili kumfurahisha nani?? Nafsi yake au nafsi za wakubwa zake? Mbona Malecela halalamiki kwamba amevunjiwa heshima kwa Mabalozi na Viongozi wa serikali baada ya kusema ukweli? Kumsifia mtu uongo kwamba ni shujaa kwa watanzania ni kumkashifu? Itakuwa kumkashifu tu endapo Mabalozi na Viongozi wenzake wa serikali watatamka hadharani kwamba walichofanya polisi kilikuwa ni sawa na hawajakiuka maadili hivyo Membe kusingiziwa kwamba amesema wamekiuka maadili ni kumuonea.

Ni chombo gani kinaweza kuwasafisha polisi kwamba hawakukiuka maadili?? Tume Huru!! Ili Membe aweze kushinda kesi yake alazimishe kuundwa kwa Tume hiyo na ikishatoa ripoti yake kwamba Polisi hawakukosea basi kweli atakuwa amesingiziwa maneno ambayo yamemvunjia heshima!!


Ndugu, hili ni jambo ambalo mwanafunzi wa chuo cha mahakama Lushoto wa Cheti (certificate) anatakiwa alione!!

Heshima inavunjwaje kwa kuitwa shujaa wakati wewe ni muoga wa kwanza??? Amegombanishwa na watanzania gani kwa yeye kusemekana amesema maneno hayo?? Kuna ushahidi kwamba wapo watu walimtumia salamu za pongezi kwa kusema ukweli. Ninafahamu viongozi wa CHADEMA na Polisi ambao walimsifu kwa kauli yake. namfahamu mtu ambaye alisema Membe anaweza kuwa Raisi!! Sasa nadhani alimaanisha Membe anaweza kuwa Rahisi.


Kama ni shinikizo basi ameingia mtegoni kwa sababu ndoto zake (kama zilikuwepo) za 2015 zimeishia hapa! Watakuwa wamemsukuma asonge mbele na kukana kauli iliyompatia umaarufu asiostahili na yeye hajaliona hilo badala yake amekurupuka ametaka yakanushwe.


My advice, Membe tulia. Kama umesifiwa uongo tunashukuru watanzania tumejua msimamo wako. Tunakushukuru kwa kurudisha sifa zetu na heshima imeanguka baada ya kusoma barua yako na siyo kwa kusoma habari iliyoandikwa na Mwananchi!! Siku ya kesi watakuja mashahidi kusema ni jinsi gani walivyokuona shujaa baada ya kusoma ile habari na wewe utahitajika kuleta mashahidi Viongozi wa Jeshi la Polisi, Serikali na Mabalozi watakaosema walikudharau kwa kusoma ile habari na mahakama itaamua!! Mashahidi wataitwa kutoka kila mkoa ambao gazeti la mwananchi linasambazwa. Kila shahidi atakuja kutoa ushahidi wake na mimi nitakuwa shahidi wa kwanza kwamba habari hiyo haikukuvunjia heshima bali ilikupa sifa za uongo usizostahili.


Nawaomba wanaJF wote watakaokuwa tayari kutoa ushuhuda na ushahidi kwamba Membe amejivunjia heshima yake mwenyewe baada ya kusoma barua yake wajitokeze siku kesi hiyo itakapokuja kusikilizwa. Na kama wanategemea kwamba vyombo vya habari vitanyamazishwa kwa staili hii wameumia. Hawataweza kufunga midomo ya magazeti, hawataweza kuzuia nguvu ya UMMA.


Kwa kweli membe umenitoka kama alivyonitoka Makamba na CCM! Mnakera, mnatukwaza, mnatuudhi, mnatupa hasira. Ni heshima gani uliyonayo kuwa kiongozi kwenye serikali ambayo deni lake la taifa ni mara mbili kwa sasa? ni heshima gani uliyonayo kuwa kiongozi kwenye serikali inayojisifu kuwa na spika wa kwanza mwanamke lakini inapiga wanawake wajawazito? ni heshima gani uliyonayo kuwa kiongzi kwenye serikali ambayo vijana wake hawana ajira na wamechoka wako tayari kufa ili mradi kuleta mabadiliko? ni heshima gani uliyonayo kuwa waziri wa mambo ya nje wakati kuna kampuni hewa kutoka nje ambazo zinatuiibia mchana kweupe kama Dowans na Richmond? ni heshima gani uliyonayo wakati jimboni kwako wananchi wanapigana kugombea maji kwenye bomba la mtu la nyumbani? ni heshima gani uliyonayo kuwa kiongozi wa serikali ambayo wanafunzi wake hawana posho za kujikimu? Ni heshima gani uliyonayo kuwa kingozi wa serikali ambayo imeshindwa kuwalipa wazee stahili yao badala yake inawapiga mabomu? ni heshima gani uliyonay kuwa kiongozi kwenye serikali ambayo imeingia kwenye mkataba na TICTS ikavunja, DAWASA ikavunja, ATC ikavunja, IPTL, TTCL, TRC ikavunja n.k.

Membe, umevunjiwa heshima mbee ya polisi ambao hawana fedha za kuwapeleka watoto wao shule au kuwapatia matibabu? Umevunjiwa heshima mbele ya viongozi wa polisi ambao wanageuka walinzi wa security baada ya kustaafu? Wanakuheshimu sana?? Ni heshima hiyo imevunjwa??? hao right thinking members of the society ni kina nani??? Polisi? Wangekuwa ni right thinking members wangeua raia? na Mbeya pia walikuwa wanateka kituo cha polisi chenye silaha nzito??

Wangekuwa ni right thinking members unafikiri Kagonja angeenda kuonyesha waandishi wa habari DVD ya kutengeneza wenyewe? Kama wananchi walikuwa wanenda kuteka kituo cha polisi cha kati, je saa tano wakati wanawapiga raia na kuwafyatulia risasi walikuwa wanaenda kuteka nini?? maji?? na Freeman Mbowe na wengine walienda kuteka kituo cha polisi ndipo wakapigwa na kuwekwa lock up?

Na kwanini mabomu ya machozi yalipigwa uwanjani? Ukweli wasiousema polisi ni kwamba mabomu ya machozi yaliisha baada ya kupigwa hovyo uwanjani then wakaamua kutumia risasi za moto!! Waliopewa jukumu hilo ni wananfunzi kutoka CCP ambao hawajafuzu!! Hao ndio umevunjiwa heshima mbele yao!! Na wewe hao ndio wanaokupa heshima!!
 
Never heard of a lawsuit this damn stupid.Tena kutoka kwa mtu aliepachikwa uwaziri! Yani anataka kuwashtaki kwa kumpakazia mazuri?Nwyz labda ni haki yake ila statement zake zinapingana unless watasema yale mauaji ni matokeo ya "kiherehere" cha wananchi wenyewe!Maana anapinga kusema polisi walifanya makosa mauaji ya Arusha kwasababu ataonekana anaponda jeshi la polisi alafu anarudi kusema serikali haijafurahishwa na mauaji hayo?Wana mpango wakumtupia nani lawama?Kweli viongozi tumepata mwaka huu!
 
Yaani kwa kifupi ni kwamba viongozi wetu wako radhi at any cost kumfurahisha jk kuliko wananchi waliowachagua!
 
Of course moja ya sababu ni kiherehere cha wananchi na kutumiwa vibaya kama kondom na VIONGOZI WA CHADEMA

Never heard of a lawsuit this damn stupid.Tena kutoka kwa mtu aliepachikwa uwaziri! Yani anataka kuwashtaki kwa kumpakazia mazuri?Nwyz labda ni haki yake ila statement zake zinapingana unless watasema yale mauaji ni matokeo ya "kiherehere" cha wananchi wenyewe!Maana anapinga kusema polisi walifanya makosa mauaji ya Arusha kwasababu ataonekana anaponda jeshi la polisi alafu anarudi kusema serikali haijafurahishwa na mauaji hayo?Wana mpango wakumtupia nani lawama?Kweli viongozi tumepata mwaka huu!
 
Naomba mkae kimya, hapa magazeti yanayoandika habari za weledi na za ukweli na uhakika na hawana majungu wala chuki wala makundi wala mitandao ya kimaslahi, ni magazet haya hapa:
1. Uhuru
2. Daily news
3. Mtanzania
4. Rai
5. Habari leo.

Haya ndio magazeti makini kwa hapa Tanzania, na ushahidi ninao sijawahi kusikia yakishitakiwa mahakamani wala baraza la habari magazeti haya. kwahiyo naomba mkae kimyaa kabisa kama mnanyolewa.

hahahahah,hayo magazet ni maalum kwa ajili ya kufungia maandazi
 
Ingawa Biblia imeandiaka neno USIOGOPE mara 365 (kila siku katika mwaka) lakini inashangaza jinsi waziri anavyoweza kukana kauli yake mwenyewe kutokana na uwoga.
 
Mbona nilimsikia tbc huyu bwana akiongea tena kwa msisitizo??inaelekea jk ameshamshushia rungu, jinga kabisa mi nilifikiri membe una akili kidogo kumbe hamnazo bwana!!!!!!!
 
bado hajapata safari maana safari zake zote ziko booked na Mkwere. He is iddle for the time being, labda badaye kidogo atapata trip.
Hizi nguvu na huu muda angeutumia kushughulikia mambo yenye tija ningemuona wa maana.... au yupo idle na hana shughuli za kufanya?
 
Kabla sijasoma signature yako nilitaka ku-coment..................


Nashukuru kwamba wewe ni great thinker na ni mtu makini, haukurupuki kucomment kabla haujatafakari na kujuwa ni nini unataka kucomment, kuna wavivu wa kufikiri humu, ambao wao hawajui hata kudadisi, kazi yao ni kuongea tu kama bata(Jaji Werema) wamenikejeri bila kujuwa mimi ni mtu wa namna gani, lakini msingi mkubwa wa hoja yangu ni kwamba roho inaniuma sana kuona hayo magazeti ambayo nimeyaorodhesha hapo yakileta uchochezi, kukashifu watu na kila aina ya uovu lakini hayashitakiwi wala hata hayajawahi kukanywa na baraza la habari, ndio maana nikachokoza mjadala kwamba kaeni kimya kama mnanyolewa, na kwa lugha nyingine ipo siku, utasikia redio yeyote makini inapelekwa mahakamani rakini yule mpumbavu pale clouds fm Kibonde anaetukana watu kila siku kwenye kipindi chake cha jahazi, usishangae kusikia kwamba redio yao haijawahi hata kulalamikiwa baraza la habari.
Wito: changes beggins with you. tuanze kuchukua hatua sasa badala ya kuwa watu wa kulalamika.
 
Unatuambia tukae kimya wewe kama nani?


Mimi ni mwana JF mwenzako, nimetumia uhuru wangu wa kutoa maoni kama ulivyofanya wewe, ndio maana sijakuuliza kwamba unaniuliza swali wewe kama nani?
Ombi: tuwe na bidii ya kusoma na kudadisi. some people they don't listen to understand, but they listen to intend to reply. don't be in that category.
 
Back
Top Bottom