Membe: Sijatofautiana na JK kuhusu Comoro | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Membe: Sijatofautiana na JK kuhusu Comoro

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Apr 14, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Apr 14, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana.

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe, amesema hakutofautiana na msimamo wa Rais Jakaya Kikwete kuhusiana na suala la uchaguzi mkuu wa visiwa vya Comoro unaotarajiwa kufanyika mwakani.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Membe alisema msimamo wa Rais Kikwete ni kwamba uamuzi uliochukuliwa na Bunge la Comoro kuwa uchaguzi mkuu ufanyike Novemba mwakani uheshimiwe.

  “
  Huo ndio msimamo wa Rais Kikwete na ndivyo nilivyosema mimi, inawezekana watu walioandika tumetofautiana na Rais walimsikia vibaya wakati ule alipokwenda Comoro, lakini sisi tunaheshimu chombo cha kidemokrasia ambacho ni Bunge,” alisisitiza Membe.

  Alisema kamwe serikali ya Tanzania haiwezi kupinga maamuzi yaliyofanywa na chombo cha kidemokrasia kama Bunge na kwamba kufanya hivyo ni kuleta chokochoko ndani ya visiwa hivyo.

  Wapinzani wa Comoro wakiongozwa na Ali Houmadi Msaidie, wanapinga uamuzi huo wa Bunge wakisema kufanya hivyo ni sawa na mapinduzi ya Katiba na kwamba yatakayomwezesha Rais wa Visiwa hivyo Abdalah Mohamed Sambi kuendelea kuwa madarakani kwa miezi18 zaidi badala ya Mei mwaka huu.

  Walisema alipotembelea visiwa vya Anjuan, Moheli na Grande miaka miwili iliyopita, Rais Kikwete alisema si vyema kubadili Katiba ili kumwezesha mtu kuendelea kuwa madarakani.

  Wanapinga kauli ya Waziri Membe aliyoitoa juzi alipotembelea visiwa hivyo ya kuunga mkono uamuzi wa Bunge kupanga uchaguzi huo ufanyike Novemba mwakani kwamba inapingana na ile ya Rais Kikwete.

  Alieleza kuwa wapinzani wa visiwa hivyo wamekuwa wakipita katika balozi mbalimbali hapa Tanzania kupinga uamuzi huo wa Bunge kusogeza uchaguzi huo hadi mwezi Novemba mwakani.

  “
  Rais Kikwete alisema Bunge la Comoro lisikilizwe na lipewe heshima yake na mimi nimesema hivyo hivyo, tunaunga mkono uchaguzi wa magavana wote na Rais ufanyike kama Bunge la Comoro lilivyoamua,” alisema Membe.

  Alisema wakati wa kikao hicho cha Bunge lenye wabunge 83, wabunge 21 wa upinzani walitoka nje wakipinga wazo hilo, lakini wengine 63 waliobaki walipiga kura ya kuunga mkono wazo hilo.

  Alisema viongozi hao wa upinzani walikwenda hadi kamisheni ya AU kulalamikia uamuzi huo wa Bunge lao na viongozi wa kamisheni hiyo walimpigia simu (Membe) kumwomba ushauri wa serikali ya Tanzania kuhusu mgogoro huo.

  Alisema kabla ya kutoa ushauri alikwenda Comoro kuangalia hali halisi na alifanya hivyo baada ya kuagizwa na Rais Kikwete.

  Alisema alipokuwa Comoro aliuliza iwapo wapinzani hao wamepinga uamuzi wa Bunge katika mahakama ya Katiba lakini aliambiwa kuwa hawakuwahi kufanya hivyo.

  “
  Nilikwenda Comoro nikaonana na Rais wao na baada ya hapo nikatoa tamko kwa vyombo vya habari kuwa msimamo wa Tanzania tunaheshimu maamuzi ya Bunge la Comoro kwamba uchaguzi ufanyike Novemba mwakani,” alisema.

  Alisema kwa hali tete ilivyo Comoro lazima serikali ya Tanzania iheshimu maamuzi yanayofanywa na Bunge na aliwataka wapinzani waheshimu maamuzi ya vyombo vya kidemokrasia kama Bunge.

  Alisema kama wapinzani wanataka kufanya maamuzi yao wajitahidi wawe wengi ndani ya Bunge ili wafanikishe malengo yao badala ya kupinga wakiwa nje.

  “
  Comoro imepitia mapinduzi 21 hadi sasa na kwa kweli Tanzania imechagia sana kuleta amani ya Comoro hivyo lazima tuheshimu mamlaka zilizopo ili kuepuka choko choko,” alisema.

  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Apr 14, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Si tuamue tu kuungana nao.. ! Let the dream of African Unity continue!!
   
 3. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #3
  Apr 14, 2010
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Ila kama hali ndiyo hiyo,Bunge lao limeridhia basi ni vizuri

  Maamuzi ya bunge ni ya kuzingatia,hiyo ndiyo maana ya demokrasia

  Hata hivyo Jk na Membe,wanongelea na kusizitiza kuhusu kuliheshimu Bunge but hapa kwetu wanatenda tofauti.Huu unafuiki wa viongozi wetu sijui utatufikisha wapi.
   
 4. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #4
  Apr 14, 2010
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Waandishi wetu wengi ni wababaishaji.Yaani Membe ameitisha press conference kukanusha kuwa hatofautiani na JK lakini mwandishi anashindwa japo kutupa dondoo Membe alisema nini,lini,wapi maneno yaliyopelekea tafsiri kuwa anatofautiana na bosi wake!Wanajua kunukuu tu: alisema hili,alisema lile.Hata kama anazuga,yote sawa tu kwao.
   
 5. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #5
  Apr 14, 2010
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  - Hawa ndio waandishi wetu, utakuta hata the original habari ambayo Rais alisema nini hawana, lakini wako very good kukimbilia kuanizsha controversials bila facts, walitakiwa kuweka wazi Rais alisema nini na Wazirii amesema nini ili wasomaji au wananchi tujue tofauti,

  - Halafu umeona wanavyo jaribu kuigonganisha habari ili ionekane ina walakini lakini wana-fall far away, bunge limeamua that is the bottom line either hao wapinzani watumie fillbuster au wakubali yaishe lakini hakuna ishu hapo.

  - Heshima sana kwa waziri hapa maana anaeleweka na inakubalika na ndio Demokraisa hiyo bunge kuamua lini na wapi uchaguzi ufanyike, kwa hili Rais na Waziri wanahitaji heshima sana.

  Respect.


  FMEs!
   
 6. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #6
  Apr 14, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Nawaamini waandishi wachache sana bongo!
   
Loading...