Membe: Nchi hii inahitaji majasiri kama mimi

Membe: Nchi hii inahitaji majasiri kama mimi

Jasiri Yuko mmoja tu.........

MAGUFULI MAGUFULI

MEMBE alitaka awarubuni Hawa wajumbe 1822?!!!

Angeweza WAPIIIIII.......

Popote Ulipo Mfikishieni Habari mbunge wa Nkasi mh.Ally Kessy,mwambieni AYATAFAKARI SANA YALE MANENO ALIYOMALIZIA MH.MZEE ALLY HASSAN MWINYI PALE JUKWAANI LEO TAREHE 11/7/2020.

NI Mimi mnyonge wa uswahilini.
Muuza Al Kasus Tandale,
Jumbe Brown
 
Mkuu kwenye huo mgao wa Membe nishirikishe na mimi niwe kwenye list ya wapanga mapambio. Kuna shughuli zangu zimekwama hata nipate kiasi cha kuzimua.

Hakuna mgao wowote ndugu yangu

Nimefuatilia rekodi ya Membe tangu akiwa serikalini ni mtu msafi hajawahi kuitia nchi hasara kwa mikataba yoyote ya kifisadi tofauti na mzee wa Chato mwenye maskendo kibao tangu akiwa waziri

Pili ni mtu ambaye amepambana na utawala wa Jiwe kwa kuzungumza bila hofu wala unafiki

Tatu nakubaliana naye kwenye msisitizo wake wa kutaka nchi itawaliwe kwa kuheshimu katiba na utawala wa sheria

Pamoja na hayo nakubaliana naye sana kwenye sera yake ya maendeleo kuwa ni lazima kilimo kipewe kipaumbele sana, utawala huu umesahau kilimo kabisa.

Pia ni mtu mwema, siyo katili, siyo muonevu, hawezi kuonea onea watu pindi akiwa rais

Lakini ukiacha hayo anajiamini, anajua kujenga hoja na kuzisimamia na ana uwezo wa kuelezea mawazo yake very clearly

Hakuna cha kununuliwa, Sijanunuliwa na mtu yeyote
 
Julai 2020
Nafasi za ubunge nako moto ni mkali CCM kubanwa na upinzani
Wakati hayo yakiwa kwenye ungwe ya urais, wakati huu pia kunashuhudiwa idadi kubwa ya wanasiasa wanaoendelea kujitokeza wakitangaza nia zao za kutaka kuwania nafasia za ubunge katika maeneo mbalimbali ya nchi.

Tansania Präsident John Magufuli

Rais John Magufuli wa Tanzania anawania muhula wa pili
Chama tawala CCM ndicho kinachoonekana kuongoza kwa kuwa na makada wengi wanaojitokeza hadharani ambao wameyabainisha maeneo wanayokusudia kuongeza ushawishi wao kwa ajili ya kusaka kura.

Majimbo yaliyoko eneo la kaskazini kama vile Kilimanjaro na Arusha maeneo ambayo ni ngome ya chadema yanatarajiwa kuwa na ushindani mkali zaidi hasa kutokana na kuwavutia wanasiasa wengi ambao wameonyesha nia zao.

Hali hiyo inafanya mtihani wa kubashiri kama majimbo hayo yataendelea kubakia mikoni mwa upinzani ama kwenda CCM kuwa ngumu hasa kutokana na mwenendo mpya wa kisiasa unaoendelea kushuhudiwa sasa.

Wakati hayo yakiendelea hivyo, baadhi ya wateule wa rais kama vile wakuu wa mikoa na wilaya waliokuwa na kiu ya kutaka kuwania ubunge sasa wameanza kujiweka kando wakisitisha mipango yao,baada ya onyo la mwenyekiti wa chama hicho, Rais John Magufuli.

Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila ambaye awali alikuwa na mipango ya kuwania ubunge katika Jimbo la Iringa Mjini, ni miongoni mwa wale waliyoyaweka kabatini mawazo yao kwa sasa.

Hata hivyo, duru za habari zinasema kuwa baadhi ya wateule hao bado wanaendelea kupima upepo kuangalia kama wajitose kwenye mbio za ubunge au kusitisha moja kwa moja mipango yao.

Source : Joto la Uchaguzi Mkuu lapanda nchini Tanzania | DW | 08.07.2020
 
Hakuna mgao wowote ndugu yangu

Nimefuatilia rekodi ya Membe tangu akiwa serikalini ni mtu msafi hajawahi kuitia nchi hasara kwa mikataba yoyote ya kifisadi tofauti na mzee wa Chato mwenye maskendo kibao tangu akiwa waziri

Pili ni mtu ambaye amepambana na utawala wa Jiwe kwa kuzungumza bila hofu wala unafiki

Tatu nakubaliana naye kwenye msisitizo wake wa kutaka nchi itawaliwe kwa kuheshimu katiba na utawala wa sheria

Pamoja na hayo nakubaliana naye sana kwenye sera yake ya maendeleo kuwa ni lazima kilimo kipewe kipaumbele sana, utawala huu umesahau kilimo kabisa.

Pia ni mtu mwema, siyo katili, siyo muonevu, hawezi kuonea onea watu pindi akiwa rais

Lakini ukiacha hayo anajiamini, anajua kujenga hoja na kuzisimamia na ana uwezo wa kuelezea mawazo yake very clearly

Hakuna cha kununuliwa, Sijanunuliwa na mtu yeyote

Mkuu hizi ni sifa za marehemu, Membe alikuwa madarakani muda wote wa JK, weka mchango wake kwenye katiba mpya ndani ya rasimu ya Warioba. Ujasiri wa Membe umeanza baada ya kuwa nje ya mlo kipindi hiki cha Magufuli? Oneni aibu ya kutetea wahuni walio nje ya mlo.

Ni kweli Magufuli ni bomu kwenye nafasi ya urais, lakini haimaanishi kuwa Membe ni sahihi. Kama ni mrejesho wa hela yake nitakulewa maana ni mambo ya utafutaji, na sio kinyume chake.
 
Hali ilivyo kisiasa kuna majasiri wananchi wengi sana Tanzania wapo kila kona kuikabili CCM Mpya kupitia sanduku la kura 2020

Julai 2020
Mbozi, Tanzania

Pascal Haonga na CHADEMA waonesha hali ya hewa halisi ya kisiasa kata ya Igamba wilaya ya Mbozi
CCM Mpya ipo katika hali ngumu sana kisiasa nyanda za juu kusini na katika kanda nzima ya CHADEMA Nyasa inayojumuisha mikoa ya Iringa, Njombe, Mbeya , Songwe nchini Tanzania

Source : Vwawa TV onilin
 
Mkuu hizi ni sifa za marehemu, Membe alikuwa madarakani muda wote wa JK, weka mchango wake kwenye katiba mpya ndani ya rasimu ya Warioba. Ujasiri wa Membe umeanza baada ya kuwa nje ya mlo kipindi hiki cha Magufuli? Oneni aibu ya kutetea wahuni walio nje ya mlo.

Ni kweli Magufuli ni bomu kwenye nafasi ya urais, lakini haimaanishi kuwa Membe ni sahihi. Kama ni mrejesho wa hela yake nitakulewa maana ni mambo ya utafutaji, na sio kinyume chake.

Kuhusu katiba mpya, Membe alikuwa anaunga mkono katiba mpya

Kwenye kuhusu aina ya Muungano, yeye anataka kura za maoni wananchi wachague aina ya muungano, yaani wananchi wao wenyewe kwa wingi wa kura zao waamue ni aina gani ya muungano wanautaka!

Cheki Interview hii ya mwaka 2012, unaweza kuona baadhi ya misimamo yake ya kisiasa toka zamani kabisa

Back
Top Bottom