Benson Mramba
JF-Expert Member
- Oct 29, 2013
- 766
- 1,884
Habari hizi nilizikia tangu 2016 nikiwa pale Makao Makuu ya CHADEMA. Ilisemekana kuwa Nape, Membe na wengineo wanapanga kuhamia CHADEMA.
Mwaka huo huo nikakutana na ndugu mmoja aliyekuwa makao makuu ya CCM lakini alikosa uteuzi wa wakuu wa wilaya na alikuwa kwenye mtandao wa Membe nikamjulisha habari za Membe kuhamia CHADEMA alishtuka kwa furaha. Akaniambia Membe ana dola nyingi ameficha ambazo alizipata kwa Gadafi.
Mwaka 2017 rafiki yangu mmoja mbunge kijana wa CHADEMA aliniambia kabla ya 2020 kutakuwa na uhamaji wa Wabunge kutoka pande zote. Aliniambia siasa za 2020 zitakuwa kama za Kenya. Siasa za muungano wa watu maarufu sio Umaarufu wa Vyama tena.Mwezi uliopita kuna rafiki yangu mwingine wa CHADEMA aliniambia umehama ila 2020 hamuwezi kushinda maana mtakimbiwa na wana CCM wengi.
Aidha Miaka mitatu sasa baadae nikifuatilia yanayoendelea ndani ya CCM na hatua mbali mbali za serikali kudhibiti fedha haramu kwenye maduka ya kubadilishia fedha na benki zetu naamini pasi na shaka kuwa huenda kweli zipo dola zimefichwa mahali zinataka kuingia kwenye mzunguko.
Taarifa za uhakika kutoka vyanzo vya ndani vya CHADEMA ni kuwa Membe anahamia CHADEMA. UKAWA unakufa kunakuja kitu ambacho Zitto amekuwa akikitangaza kinachoitwa ADF (Alliance for Democratic Front).
Vyovyote itakavyokuwa Magufuli ameshamaliza harakati hizi kwa mambo aliyoyafanya mpaka sasa. Kumshinda ni ndoto za mchana. Atabeba kura **** anakusanya senene au kumbikumbi.