Membe na 'sizitaki mbichi hizi'

mpayukaji

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
940
349
[h=3]Namna hii si atachemsha hata kabla ya kipute chenyewe kuanza?[/h]


Baada ya waziri wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe kuzindua tamasha la Pasaka sasa naona imeanza kulipa. Anapewe coverage kubwa tena ukurasa wa mbele. Je hii kampeni ya 'sizitaki mbichi hizi' kuelekea uchaguzi mkuu wa 2015 itamsaidia au kumzamisha? Kwanini asiseme wazi kama Samuel Sitta kuwa urais anautaka? Kuna haja ya wanasiasa wetu kuwa wawazi badala ya kujirusha rusha kimanga. Hongera Alex Msama kumfagilia comrade wako mpya Ben Membe.
SAM_0698.JPG
 
unajua kuwa vyombo vya habari hasa magazeti yanaweza kutohoa maana halisi kutoa kwenye hoja ya msingi. Anyway sidhani kama yy kusema atagombea au la kama hajaamua pia siyo sahihi. Hya mamo inaidi aongee na familia yake kwanza before kuongea na mtu yyte au hata chama lake. kwahiyo kumshinikiza aseme kwa ghafla.
 
Mkuu mbona unapayuka kama jina lako lisemavyo?
Kuna dhambi gani kwa Membe kufungua tamasha aliloalikwa? kumbuka hajajipeleka pale ila alialikwa tofauti na mwana mmoja ambae yeye kazi yake ni kutafuta matukio aonekane.
Angeenda hata Mzee makamba ungesema nae anautaka urais.
OTIS
 
Wewe mpayukaji kuwa makini na threads zisizo na kichwa wala miguu. Kwanza yaelekea hujui maana ya msemo uliobeba kichwa cha uzi wako maana hauendani na habari husika, si vibaya ukarudi darasani kujifunza upya kiswahili. Ina maana na Nape naye anataka urais? jina lake si lipo hapo? Riginald Mengi anazindua hafla au sherehe ngapi kama mgeni rasmi? naye anataka urais? Acha kutoa mapovu mkuu
 
Nilijua watu wa Membe mtanitukana na kutaka kunifundisha vitu ninavyofundisha. Hata hivyo sikati tamaa zaidi ya kufurahi kuwa kumbe imewagusa.
 
Nilijua watu wa Membe mtanitukana na kutaka kunifundisha vitu ninavyofundisha. Hata hivyo sikati tamaa zaidi ya kufurahi kuwa kumbe imewagusa.
Usijali sana, hiyo ndo ilikuwa interpretation yako! na hao wangeweza kutoa yao katika coverage hiyo hiyo kosa umeanza.
 
Back
Top Bottom