Idd Ninga
JF-Expert Member
- Nov 18, 2012
- 5,136
- 4,298
Kuna mengi katika historia ya ushairi na maisha ya washairi ndani ya Tanzania ambayo kwa kiasi kikubwa imekuwa haijukani na wengi wala kuhuifadhiwa katika kumbukumbu nzuri za kihistoria kwa sababu ambazo ni ngumu kuziweka wazi hasa katika kutazama tamaduni na mila za lugha ya Kiswahili,labda kwa sababu ya ukisasa ambao unaweza kuwa ni sababu ya kuuficha utamaduni halisi wa mila ya lugha ya Kiswahili.
Audax Khendaguza Vedasto mmoja kati ya wanasheria na wasomi wa fani ya sharia nchini kupitia kitabu chake ama diwani yake ya CHOPIKWA KIKAPIKA ya mwaka 2010 anaelezea ,mkasa mzito a kupoteza tungo zake nyingi ambazo alizitunga akiwa katika umri mdogo na baadae tungo hizo kupotea na mpaka wa leo hakuna matumaini kama atakuja kuzipata au zitakuja kupatikana.
Tarehe 21 Mei 1996 katika katika ya ziwa Victoria ajali mbaya ya meli ya Mv Bukoba ilizima na mamia ya watu kupoteza maisha akiwemo Mwalimu Dominick Alimanya.
Domonick Alimanya alifariki dunia katika jail ya meli ya ya Mv Bukoba akiwa na hazina ya mashairi yaliyoandikwa na Audax Kahendaguza na mashairi hayo kupotelea majini.
Shairi muhimu kabisa ni shairi lake la kwanza kutunga ambalo alikuwa akijibu shairi la SIZITAKI MBICHI HIZI huku yeye akijibu nazitaka mbichi lakini bahati mbaya shairi hilo pamoja mashairi mengine yaliweza kupotelea majini na kushindwa kupatikana kwa sababu hasa katika zama hizo tungo nyingi zilikuwa zikihifadhiwa katika madaftari.
mawasiliano-iddyallyninga@gmail.com