Woote mnazunguka huku na kule kutafuta majibu ambayo mnayo tayari bila kujijua!
Swali rahisi sana, ni Wangapi kati yetu Majumbani mwetu kuna vyombo (vile vizuri) ambavyo havitumiki mpaka mgeni aje?
au ni wangapi kati yetu ambayo majumbani mwetu huwa tunafurahia siku mgeni akija kwani ndio tutakula Vizuri? Hata vijijini kwetu si ndio jogoo tena yule mnono atachinjwa?
Kama ni watoto siku mgeni akija si ndio wataambiwa wavae zile nguo za kabatini?
Sasa tofauti iko wapi, au kwa sababu Serikali ndio inafanya?
kumbukeni Serikali siyo Mashine bali inaongozwa na Watu na watu wenyewe ndio sisi, hivyo msitegemee vitu tofauti na yale tunayoyafanya majumbani mwetu, ni swala la Mila na Desturi, Jamii nyingine haziko hivyo, kama ni vyombo vizuri, basi vinanunuliwa kwa ajili ya Familia kutumia na sio Wageni, kama ni makochi yapo kwa ajili ya Familia na Sio wageni, hiyo ndio tofauti!