Membe: Malawi haiwezi kuishtaki Tanzania ICJ, Tanzania haiitambui ICJ

mwl mwenzangu mie napata hisia kwamba hawa wanachochewa na UK kisa baba yake banda alikuwa daktari wa malkia, sasa ifike mahali na sisi tuonyeshe kwamba we can na hatuombi ni chetu. kamalawi ni kanchi kadogo sana tena hakana hata ardhi na hivi sijui hata kama kapo SADC inamaana kwa kutumia nchi za SADC tu tena kwaajili ya matumizi ya ardhi zao malawi kwishney.

to me wameitwa wamegoma tuendelee na kazi zetu ili waje kivita sasa wakutane na wababe alaah!

Hivi J. Banda ni mtoto wa Kamuzu Banda?
 
Read in between the lines we mzee Tanzania ni mjumbe wa ICJ ila haitambui mamlaka ya hiyo mahakama kwa hivyo ina haki ya kutokubaliana na maamuzi ya hiyo mahakama

Hivi kwa upande wa ICC vipi? Tanzania inatambua mamlaka yake? Ha ha ha ha ha! Wanasiasa wetu sidhani kama wanaweza thubutu kufanya hilo kosa - ni sawa na kujitundika mwenyewe.
 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb) amewambia waandishi wa habari kuwa Malawi haiwezi kuipeleka Tanzania katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) ili iamue mgogoro wa mpaka kwenye Ziwa Nyasa unaozozaniwa baina ya nchi hizi mbili.

Mhe. Membe alibainisha hayo mbele ya Waandishi wa Habari jijini Dar es Slaam siku ya Jumamosi tarehe 06 Oktoba, 2012. “Tanzania ni mjumbe wa ICJ lakini bado haijatambua Mamlaka ya Mahakama hiyo, hivyo Malawi haiwezi kuipeleka Tanzania ICJ isipokuwa Tanzania inaweza kuipeleka Malawi”, alisema Mhe. Membe.

Mhe. Waziri aliitolea wito Malawi irudi katika meza ya majadiliano na kuiomba Serikali ya nchi hiyo kutuma wawakilishi katika kikao walichokubaliana kufanyika Dar es Salaam kuanzia tarehe 07 - 10 Oktoba, 2012.

Kikao hicho kinakusudia kupendekeza msuluhishi ambaye atakubalika na pande zote baada ya kubainika kuwa Tanzania na Malawi zenyewe hazitaweza kusuluhisha mzozo huo.

Mhe. Waziri aliwafahamisha waandishi kuwa alipokea kwa mshtuko taarifa kwamba Malawi haitashiriki katika kikao kilichopangwa kufanyika Dar es Salaam kwa hoja kuwa lazima Serikali ya Tanzania itoe maelezo ya kina kuhusu boti ya kijeshi iliyoonekana kufanya doria kwenye Ziwa Nyasa ambayo inasemekana kuwaletea hofu kubwa wakazi wa maeneo ya Ziwa kwa upande wa Malawi.

Aidha, Malawi inataka kupatiwa maelezo kuhusu toleo jipya la Ramani ya Tanzania lililotolewa na Mamlaka za Tanzania ambayo inaonyesha mpaka baina ya nchi hizo mbili umepita katikati ya Ziwa Nyasa.

Akitolea ufafanuzi masuala hayo, Mhe. Membe alisema kuwa toleo hilo jipya lilikuwa na lengo la kuionyesha Mikoa mipya minne na Wilaya mpya 19 katika ramani ya nchi, na kuonyesha mpaka kupita katikati ya Ziwa, hilo si jambo jipya kwani ndivyo ramani ya nchi yetu ilivyokuwa katika matoleo yote manne yaliyotolewa na Serikali kabla na baada ya uhuru.

Kuhusu boti ya kijeshi kufanya doria kwenye Ziwa Nyasa, Mhe. Waziri alisema taarifa hizo sio sahihi, ila kinachofanyika ni doria ya kawaida ambayo inaendeshwa na Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi kuwasaka wavuvi haramu na wale wanaotumia zana za uvuvi zilizopigwa marufuku.

Mhe. Waziri aliwahakikishia wananchi kuwa Serikali ya Tanzania inapenda kuona mgogoro huo unamalizika katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Nne inayongozwa na Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete na kitendo cha Malawi kutishia kugomea majadiliano hakitarudisha nyuma dhamira ya Serikali.

Alisema Serikali imejipanga vyema kuhakikisha kuwa inakuwa na hoja za kisayansi na kisheria ili ishinde katika mgogoro huo. Moja ya mikakati ya Serikali imeunda Kamati tatu ambazo zimeshaanza kazi na kazi yao inaendelea vizuri. Kamati hizo moja inahusika na utafutaji wa nyaraka kuhusu Ziwa Nyasa, ya pili inahusika na masuala ya kisheria na ya tatu inahusika na masuala ya majadiliano.

Alidokeza kuwa katika kufuatilia kesi zilizohukumiwa na ICJ hakuna nchi iliyodai umiliki wa ziwa lote au mto uliopo mpakani baina ya nchi mbili ilishinda kesi. Hivyo, aliwataka Watanzania wasiwe na wasiwasi kwani Serikali yao itaibuka mshindi katika mgogoro huo.

Alihitimisha mazungumzo yake kwa kuwataka Wananchi wanaoishi kando ya Ziwa Nyasa kufanya shughuli zao kama kawaida pasi na kuhofia chochote kwani hakuna tishio la vita kabisa baina ya Tanzania na Malawi.

It's a good move kwa mtazamo wangu tusikubali kwenda huko ICJ tunaweza shindwa hii kesi
...........BRAVO!!!!!!!!!! Mnaikaribia signature ya marehemu JK (jembe)
 
kuhusu boti ya kijeshi yatz kuonekana mpakan juzikat nilimwona mama banda akilalama tv mozambique alisema watz wameshajipanga kwa vita wameweka boti za kijeshi mpakani then wanapretend kutaka diplomatic solution so wao wanakwenda ICJ wapate haki yao

kumbe wanatuogopa!
 
taarifa ya membe ina akili..

Mkuu halafu nimeiamnia intelenjesia ya TZ kwani mama amemapiniki na kukurupuka kwa hisia zake, na sasa Tz wanapisha aanguke peke yake kwa majibu haya. Kweli wanawake bado hawafikia kuwa maraisi.
 
Malawi tunatakiwa tuwe makini ano maana wameolewa na UK ndio wanaowandanganya kuhusu swala la mpaka

Ndugu yangu waingereza ni washenzi sana - miaka yote ya utawala wao Tanganyika shule zote zikifundisha mpaka unapita ndani ya maji kati - leo wanajifanya hazimo. Ndo maana viongozi wapigania uhuru enzi hizo waliwakejeli kwa kuwaita MABEBERU au "washenzi tu hawa"
 
huyu mama kashalegea hii issue ni nzito kuliko alivyodhani, alikuja na mikwara na ma confidence sasa wanaishia kususia mazungumzo. alifikiri dhaifu ni dhaifu
 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb) amewambia waandishi wa habari kuwa Malawi haiwezi kuipeleka Tanzania katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) ili iamue mgogoro wa mpaka kwenye Ziwa Nyasa unaozozaniwa baina ya nchi hizi mbili.

Mhe. Membe alibainisha hayo mbele ya Waandishi wa Habari jijini Dar es Slaam siku ya Jumamosi tarehe 06 Oktoba, 2012. “Tanzania ni mjumbe wa ICJ lakini bado haijatambua Mamlaka ya Mahakama hiyo, hivyo Malawi haiwezi kuipeleka Tanzania ICJ isipokuwa Tanzania inaweza kuipeleka Malawi”, alisema Mhe. Membe.

Mhe. Waziri aliitolea wito Malawi irudi katika meza ya majadiliano na kuiomba Serikali ya nchi hiyo kutuma wawakilishi katika kikao walichokubaliana kufanyika Dar es Salaam kuanzia tarehe 07 - 10 Oktoba, 2012.

Kikao hicho kinakusudia kupendekeza msuluhishi ambaye atakubalika na pande zote baada ya kubainika kuwa Tanzania na Malawi zenyewe hazitaweza kusuluhisha mzozo huo.

Mhe. Waziri aliwafahamisha waandishi kuwa alipokea kwa mshtuko taarifa kwamba Malawi haitashiriki katika kikao kilichopangwa kufanyika Dar es Salaam kwa hoja kuwa lazima Serikali ya Tanzania itoe maelezo ya kina kuhusu boti ya kijeshi iliyoonekana kufanya doria kwenye Ziwa Nyasa ambayo inasemekana kuwaletea hofu kubwa wakazi wa maeneo ya Ziwa kwa upande wa Malawi.

Aidha, Malawi inataka kupatiwa maelezo kuhusu toleo jipya la Ramani ya Tanzania lililotolewa na Mamlaka za Tanzania ambayo inaonyesha mpaka baina ya nchi hizo mbili umepita katikati ya Ziwa Nyasa.

Akitolea ufafanuzi masuala hayo, Mhe. Membe alisema kuwa toleo hilo jipya lilikuwa na lengo la kuionyesha Mikoa mipya minne na Wilaya mpya 19 katika ramani ya nchi, na kuonyesha mpaka kupita katikati ya Ziwa, hilo si jambo jipya kwani ndivyo ramani ya nchi yetu ilivyokuwa katika matoleo yote manne yaliyotolewa na Serikali kabla na baada ya uhuru.

Kuhusu boti ya kijeshi kufanya doria kwenye Ziwa Nyasa, Mhe. Waziri alisema taarifa hizo sio sahihi, ila kinachofanyika ni doria ya kawaida ambayo inaendeshwa na Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi kuwasaka wavuvi haramu na wale wanaotumia zana za uvuvi zilizopigwa marufuku.

Mhe. Waziri aliwahakikishia wananchi kuwa Serikali ya Tanzania inapenda kuona mgogoro huo unamalizika katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Nne inayongozwa na Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete na kitendo cha Malawi kutishia kugomea majadiliano hakitarudisha nyuma dhamira ya Serikali.

Alisema Serikali imejipanga vyema kuhakikisha kuwa inakuwa na hoja za kisayansi na kisheria ili ishinde katika mgogoro huo. Moja ya mikakati ya Serikali imeunda Kamati tatu ambazo zimeshaanza kazi na kazi yao inaendelea vizuri. Kamati hizo moja inahusika na utafutaji wa nyaraka kuhusu Ziwa Nyasa, ya pili inahusika na masuala ya kisheria na ya tatu inahusika na masuala ya majadiliano.

Alidokeza kuwa katika kufuatilia kesi zilizohukumiwa na ICJ hakuna nchi iliyodai umiliki wa ziwa lote au mto uliopo mpakani baina ya nchi mbili ilishinda kesi. Hivyo, aliwataka Watanzania wasiwe na wasiwasi kwani Serikali yao itaibuka mshindi katika mgogoro huo.

Alihitimisha mazungumzo yake kwa kuwataka Wananchi wanaoishi kando ya Ziwa Nyasa kufanya shughuli zao kama kawaida pasi na kuhofia chochote kwani hakuna tishio la vita kabisa baina ya Tanzania na Malawi.

It's a good move kwa mtazamo wangu tusikubali kwenda huko ICJ tunaweza shindwa hii kesi

Speaker waweza kuwapelea huu ujumbe Wamalawi kwaneye kamtandao kao ili wajue tumeamua nini? Waweza kutumia Google kutafsiri katika kingeleza na kichechewa, lugha amabazo wanaweza kuelewa vilevile.
 
  1. watanganyika ni wezi na majambazi tu hakuna uthibisho wowote wa ziwa nyasa kuwa sehemu ya tanganyika na ndio maana hawataki kwenda mahakamani wamezoea kujidai kusuluhisha kutatua kero kama wafanyavo kwenye muungano huu feki wakati kidhati hawana nia hiyo.
    kiutaratibu hakuna nchi yoyote ambayo mpaka wake uligaiwa kupitia ziwa nalo likagaiwa,ziwa nyasa ni la wanyasa land (wamalawi) madhalim wanataka kupitisha udhalimu wao tu.
    pia kusema kuwa tanganyika ni mjumbe tu ila hawajatanbua mahakama ya ICJ ana maanisha nini? tanganyika ni mjumbe tu kufanya nini? wanaogopa kwenda mahakani sababu hawana uthibitisho wa kushinda kesi, pia anasema kuwa wameunda tume kutafuta nyaraka sasa si wanasema wanauthibitisho wa ziwa kuwa na sehemu tanganyika sasa izo nyaraka wanazitafuta wapi? na za nini?
    tatu nijuavyo mimi mahakama ya ICJ inakuwa na competency ya kusikiliza kesi ikiwa mmoja kati ya walalamikaji ni signatory wa mahakama hiyo hivyo ikiwa malawi ni mwanachama uwezekano wa kusikiliza kesi ICJ upo, membe anaogopa ameona ngoma inaelekea kubaya.
    NA INSHAALAH WATASHINDWA TU WATANGANYIKA WARUDI KWAO WAFE NA DHULMA ZAO.
    INSHAALAH, INSHAALAH, INSHAALAH

Hapo kwenye red , ninamashaka makubwa kumbe hata TZ hawana hizo nyaraka, waziri anapata wapi ubavu wa kuwahakikishia wa TZ ushindi mapema hii wakati bado wanatafuta nyaraka?
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Membe is right. Amejibu vizuri sana.

Wakati wa Nyerere kuna Wamalawi walokuwa wanatusaidia katika kumkabili Kamuzu Banda kwenye mzozo huu

Sitashanga uwezo na usahihi wa taarifa ya Membe umetokana na tip off kutoka kwa vyama vya upinzani vya Malawi. Yule mama alichemsha kuwashirikisha vyama vya upinzani. ADUI MUOMBEE NJAA
 
Wamalawi wanatapatapa. Kwakweli Membe huu mgogoro ameupatia

Hiyo patrol inaweza isiwe ya kijeshi ila bila shaka inafanya reconnaissance. Hapo tumewaweza
Huyu Membe mie namkubali sana, sio kwa hii ya wamalawi tu kwa kwa kweli katika mambo yote ya muhimu ya kigeni ukianzia kuhusu msimamo wa TZ kuhusu Libya enzi za Gadafi, Ushoga n.k. He deserve to be the next prezo
 
Hapo kwenye red , ninamashaka makubwa kumbe hata TZ hawana hizo nyaraka, waziri anapata wapi ubavu wa kuwahakikishia wa TZ ushindi mapema hii wakati bado wanatafuta nyaraka?
Ndugu yangu nyaraka ni nyingi hivyo ni lazima kuzipanga kilingana na mashtaka. we upo dunia gani ndugu hii ngoma inaenda kwenye mambo ya kisheria au unataka tushindwe kesi ulonge.
 
Wakati wa Nyerere kuna Wamalawi walokuwa wanatusaidia katika kumkabili Kamuzu Banda kwenye mzozo huu

Sitashanga uwezo na usahihi wa taarifa ya Membe umetokana na tip off kutoka kwa vyama vya upinzani vya Malawi. Yule mama alichemsha kuwashirikisha vyama vya upinzani. ADUI MUOMBEE NJAA
sio wamalawi wote wanataka ushoga, hivyo wale wote wanaopinga ushoga hasa Muluzi pros wanatutakia heri
 
  1. watanganyika ni wezi na majambazi tu hakuna uthibisho wowote wa ziwa nyasa kuwa sehemu ya tanganyika na ndio maana hawataki kwenda mahakamani wamezoea kujidai kusuluhisha kutatua kero kama wafanyavo kwenye muungano huu feki wakati kidhati hawana nia hiyo.
    kiutaratibu hakuna nchi yoyote ambayo mpaka wake uligaiwa kupitia ziwa nalo likagaiwa,ziwa nyasa ni la wanyasa land (wamalawi) madhalim wanataka kupitisha udhalimu wao tu.
    pia kusema kuwa tanganyika ni mjumbe tu ila hawajatanbua mahakama ya ICJ ana maanisha nini? tanganyika ni mjumbe tu kufanya nini? wanaogopa kwenda mahakani sababu hawana uthibitisho wa kushinda kesi, pia anasema kuwa wameunda tume kutafuta nyaraka sasa si wanasema wanauthibitisho wa ziwa kuwa na sehemu tanganyika sasa izo nyaraka wanazitafuta wapi? na za nini?
    tatu nijuavyo mimi mahakama ya ICJ inakuwa na competency ya kusikiliza kesi ikiwa mmoja kati ya walalamikaji ni signatory wa mahakama hiyo hivyo ikiwa malawi ni mwanachama uwezekano wa kusikiliza kesi ICJ upo, membe anaogopa ameona ngoma inaelekea kubaya.
    NA INSHAALAH WATASHINDWA TU WATANGANYIKA WARUDI KWAO WAFE NA DHULMA ZAO.
    INSHAALAH, INSHAALAH, INSHAALAH
Pole sana ndugu, kama ulikubali ushoga ili usaidiwe kumuliki ziwa lote pole. Kwani ninyi ziwa hili mlitokanalo mbinguni mpaka mdai lote lenu. Shame on you. Bwino Bwino
 
Hapo kwenye red , ninamashaka makubwa kumbe hata TZ hawana hizo nyaraka, waziri anapata wapi ubavu wa kuwahakikishia wa TZ ushindi mapema hii wakati bado wanatafuta nyaraka?

Wamalawi nao wanafanya hivyo hivyo mkuu, juzi tu tumesikia wamepata vielelezo toka Uingereza. Halafu ukivisoma vielelezo vyenyewe, ambavyo ilikuwa ni reports za colonial master wao, utakuta vyote vinatupa ushindi

Cha msingi hapa tuipe serikali ushirikiano kwa kuipa taarifa/vielelezo zaidi vinavyoweza kutupa ushindi wa kishindo
 
kama muingereza ndo supporter wa tanzania sina shaka mjerumani atakua anamsapoti malawi,na kama siyo mjeruman basi muingereza anaweza akawa anaplay cotradictory role ile ya devide and rule kama wailivyoitumia Kule Libya,wanagombanisha then wanakuja kama mediators huku wakichota hayo mafuta/gas,sina shaka kuna maslah yameonekana kwenye ziwa hilo so malaw wala tanz hawakotayari kuliachia ziwa hilo,hapa tuwe makin na hii kampuni ya mwingereza iliyokua ikifanya uchunguz,theres something behind in the next door

Mwingereza na tabia ya kula huku na huku ni sawa na kama nyama choma na beer. Kampuni ya Uingereza ndiyo ilipewa tender ya kufanya environmental impact assessment, ndiyo zile boti walizokuwa wanalalamika watu wa Kusini kuwa kuna watu toka Malawi wanafanya patrol kwenye ziwa Nyasa. Na kwa sasa tangu Wa Mutharike afe na ukata wa Malawi ni hawa Waingereza wameshikilia oxygen tank la hawa jirani.

Afadhali mara mia Wajerumani wanaangalika usoni, na kwa kiasi historia ya vita vya dunia & Hitler huwa bado ipo sana kwenye vichwa vyao (wajerumani) wakati wanafanya decision inayogusa nchi za nje.
 
ICJ- International Court of Justice, NewYork
ICC-International Criminal Court, The Hague

Nachanganyikiwa kidogo mkuu masopakyindi hivi ICC na ICJ kuna uhusiano wowote kati ya hivi vitu? Maana kuna mdau mmoja hapo juu amesema Jaji Chande alikuwa anagombea nafasi ya Ocampo huko ICC na akasema huu ni uzushi kusema Tanzania siyo mwanachama wa ICJ! Hebu niondoe tongotongo mkuu wangu hizi mahakama zinauhusiano wowote?
 
Kitu kilichonishtua ni Mh. Membe kusema kuwa hatuna nyaraka za mgogoro wa Ziwa Nyasa. Amesema kuwa katika kulivalia njuga suala hili Tanzania imeunda timu tatu. Alisema timu mojawapo ni ile ya wataalam ambao wanafanya kitu kinachoitwa "documentation" (kufuatilia nyaraka). Mh. Membe alisema kuwa timu hiyo ya wataalam inafanya "documentation" kwa sababu sisi Tanzania hatukuwa na documentation ya mgogoro wa ziwa Nyasa.

Kama alivyosema Mkali Tozz kuna mashaka makubwa kumbe hata hatuna nyaraka za madai yetu? Mh. Membe anapata wapi ubavu wa kutuhakikishia ushindi wa mapema wakati ndiyo kwanza tunatafuta nyaraka za madai yetu? Labda ndiyo maana anapendekeza zaidi mediation maana tukienda mahakamani tutakuwa hatuna nyaraka za kudhibitisha madai yetu?

kinja anadai kuwa "nyaraka ni nyingi hivyo ni lazima kuzipanga kulingana na mashtaka." Huu mgogoro umekuwepo zaidi ya nusu karne sasa lakini ndiyo kwanza tunaunda timu ya kufanya documentation? Inaonekana huko nyuma hatukutilia maanani kabisa implications za huu mgogoro? Mpaka gas ilipogunduliwa humo ziwani ndiyoo tukashtuka na kuja na excuses za kutokuwa na nyaraka?

Azipa anadai kuwa "Wamalawi nao wanafanya hivyo hivyo.., juzi tu… wamepata vielelezo toka Uingereza." Kwa vile wao walizubaa kufanya documentation ya madai yao basi inahalalisha uzembe wetu wa kuto-document huu mgogoro wa zaidi ya nusu karne? Kweli "tuipe serikali ushirikiano" kutatua tatizo hili, lakini sio kwa serikali kwenda kupayuka kwenye vyombo vya habari eti hatuna hata documentation ya huu mgogoro huku tukihaidiwa kuwa ushindi wa mapema ni lazima. How wakati hata nyaraka hatuna?
 
6membe.jpg

Waziri Membe amesema ameshtushwa na Malawi kusitisha ghafla meza ya mazunguzo kuhusu mpaka wa Tanzania-Malawi unaopita Ziwa Nyasa kwa kisingizio cha:
  1. Kukuta meli ya kijeshi upande wa Tanzania ikifanya doria ndani ya Ziwa Nyasa
  2. Tanzania kuandaa ramani mpya yanye kuonyesha mpaka kupita katikati ya ziwa.
Waziri Membe amesema Malawi imekurupuka kupeleka mashtaka ICJ wakati si mwanachama wake isipokuwa Tanzania tu wanachama. Malawi wanatakiwa warudi meza ya mazungumzo kuchagua mpatanishi.

Membe anaongea sana! Sasa hivi wamalawi washatuona irrelevant country kama alivyosema premier wa israel.
Nadhani wana uhakika wa wanachotaka kukifanya na wana backup ya kutosha from western. Hapa Ndo kipimo cha Dhaifu kitaonekana hadharan
 
Back
Top Bottom