Membe: Malawi haiwezi kuishtaki Tanzania ICJ, Tanzania haiitambui ICJ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Membe: Malawi haiwezi kuishtaki Tanzania ICJ, Tanzania haiitambui ICJ

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sabayi, Oct 6, 2012.

 1. Sabayi

  Sabayi JF-Expert Member

  #1
  Oct 6, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 2,321
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb) amewambia waandishi wa habari kuwa Malawi haiwezi kuipeleka Tanzania katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) ili iamue mgogoro wa mpaka kwenye Ziwa Nyasa unaozozaniwa baina ya nchi hizi mbili.

  Mhe. Membe alibainisha hayo mbele ya Waandishi wa Habari jijini Dar es Slaam siku ya Jumamosi tarehe 06 Oktoba, 2012. “Tanzania ni mjumbe wa ICJ lakini bado haijatambua Mamlaka ya Mahakama hiyo, hivyo Malawi haiwezi kuipeleka Tanzania ICJ isipokuwa Tanzania inaweza kuipeleka Malawi”, alisema Mhe. Membe.

  Mhe. Waziri aliitolea wito Malawi irudi katika meza ya majadiliano na kuiomba Serikali ya nchi hiyo kutuma wawakilishi katika kikao walichokubaliana kufanyika Dar es Salaam kuanzia tarehe 07 - 10 Oktoba, 2012.

  Kikao hicho kinakusudia kupendekeza msuluhishi ambaye atakubalika na pande zote baada ya kubainika kuwa Tanzania na Malawi zenyewe hazitaweza kusuluhisha mzozo huo.

  Mhe. Waziri aliwafahamisha waandishi kuwa alipokea kwa mshtuko taarifa kwamba Malawi haitashiriki katika kikao kilichopangwa kufanyika Dar es Salaam kwa hoja kuwa lazima Serikali ya Tanzania itoe maelezo ya kina kuhusu boti ya kijeshi iliyoonekana kufanya doria kwenye Ziwa Nyasa ambayo inasemekana kuwaletea hofu kubwa wakazi wa maeneo ya Ziwa kwa upande wa Malawi.

  Aidha, Malawi inataka kupatiwa maelezo kuhusu toleo jipya la Ramani ya Tanzania lililotolewa na Mamlaka za Tanzania ambayo inaonyesha mpaka baina ya nchi hizo mbili umepita katikati ya Ziwa Nyasa.

  Akitolea ufafanuzi masuala hayo, Mhe. Membe alisema kuwa toleo hilo jipya lilikuwa na lengo la kuionyesha Mikoa mipya minne na Wilaya mpya 19 katika ramani ya nchi, na kuonyesha mpaka kupita katikati ya Ziwa, hilo si jambo jipya kwani ndivyo ramani ya nchi yetu ilivyokuwa katika matoleo yote manne yaliyotolewa na Serikali kabla na baada ya uhuru.

  Kuhusu boti ya kijeshi kufanya doria kwenye Ziwa Nyasa, Mhe. Waziri alisema taarifa hizo sio sahihi, ila kinachofanyika ni doria ya kawaida ambayo inaendeshwa na Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi kuwasaka wavuvi haramu na wale wanaotumia zana za uvuvi zilizopigwa marufuku.

  Mhe. Waziri aliwahakikishia wananchi kuwa Serikali ya Tanzania inapenda kuona mgogoro huo unamalizika katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Nne inayongozwa na Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete na kitendo cha Malawi kutishia kugomea majadiliano hakitarudisha nyuma dhamira ya Serikali.

  Alisema Serikali imejipanga vyema kuhakikisha kuwa inakuwa na hoja za kisayansi na kisheria ili ishinde katika mgogoro huo. Moja ya mikakati ya Serikali imeunda Kamati tatu ambazo zimeshaanza kazi na kazi yao inaendelea vizuri. Kamati hizo moja inahusika na utafutaji wa nyaraka kuhusu Ziwa Nyasa, ya pili inahusika na masuala ya kisheria na ya tatu inahusika na masuala ya majadiliano.

  Alidokeza kuwa katika kufuatilia kesi zilizohukumiwa na ICJ hakuna nchi iliyodai umiliki wa ziwa lote au mto uliopo mpakani baina ya nchi mbili ilishinda kesi. Hivyo, aliwataka Watanzania wasiwe na wasiwasi kwani Serikali yao itaibuka mshindi katika mgogoro huo.

  Alihitimisha mazungumzo yake kwa kuwataka Wananchi wanaoishi kando ya Ziwa Nyasa kufanya shughuli zao kama kawaida pasi na kuhofia chochote kwani hakuna tishio la vita kabisa baina ya Tanzania na Malawi.

  It's a good move kwa mtazamo wangu tusikubali kwenda huko ICJ tunaweza shindwa hii kesi
   
 2. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #2
  Oct 6, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,354
  Trophy Points: 280
  Now he is coming to his sense...Hayo majibu yalikuwa mazuri kwa wapenda taifa na tukiwa nje ya nchi tutakuwa wamoj ana kutumia lugha moja ila tukirudi nyumbani bado ni gamba tuu.Alipaswa pia wachomekee kwa kuwatupia mpira "Kuwa mwenye mali tuu ndie apataye uchungu waharibifu wakishambulia mali.Vipi malawi hajamawahi kuwa concerned kwa hilo?Kwa kiasi fulani ingepelekea fikra za kujiona wajinga.

  Kwa kiasi kikubwa kafunika makosa ya Mungai,muaribifu aliyeaharibu kuanzia michezo hadi elimu.
   
 3. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #3
  Oct 7, 2012
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Angalau Membe amenifurashisha katika majibu yake: Doria ziendelee kama kawaida, maana si jambo geni! Pia hizi ramani zinazoonesha mpaka kuwa katikati ya Ziwa letu Nyasa nazo si ngeni, why kuzigomea sasa kwa Serikali ya Malawi?
   
 4. Azipa

  Azipa JF-Expert Member

  #4
  Oct 7, 2012
  Joined: Mar 19, 2012
  Messages: 1,072
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Wamalawi wanatapatapa. Kwakweli Membe huu mgogoro ameupatia

  Hiyo patrol inaweza isiwe ya kijeshi ila bila shaka inafanya reconnaissance. Hapo tumewaweza
   
 5. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #5
  Oct 7, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  Waziri Membe amesema ameshtushwa na Malawi kusitisha ghafla meza ya mazunguzo kuhusu mpaka wa Tanzania-Malawi unaopita Ziwa Nyasa kwa kisingizio cha:
  1. Kukuta meli ya kijeshi upande wa Tanzania ikifanya doria ndani ya Ziwa Nyasa
  2. Tanzania kuandaa ramani mpya yanye kuonyesha mpaka kupita katikati ya ziwa.
  Waziri Membe amesema Malawi imekurupuka kupeleka mashtaka ICJ wakati si mwanachama wake isipokuwa Tanzania tu wanachama. Malawi wanatakiwa warudi meza ya mazungumzo kuchagua mpatanishi.
   
 6. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #6
  Oct 7, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Tumawezaje kuwa mjumbe katika kitu tusichokitambua? Naomba nielimishwe hapa.
   
 7. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #7
  Oct 7, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Malawi tunatakiwa tuwe makini ano maana wameolewa na UK ndio wanaowandanganya kuhusu swala la mpaka
   
 8. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #8
  Oct 7, 2012
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Inawezekana ndugu zangu wa Malawi wanaona kuwa mambo hayatawaendea vizuri. "My eyes!!"
   
 9. SALOK

  SALOK JF-Expert Member

  #9
  Oct 7, 2012
  Joined: Sep 20, 2011
  Messages: 2,674
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Wamalawi wanataka kutuchafulia historia yetu njema! Hawana lengo zuri nasi, uk inawatumia vibaya hawa jamaa! Ikishindikana mazungumzo, liwalo na liwe!!
   
 10. ndevu mzazi

  ndevu mzazi JF-Expert Member

  #10
  Oct 7, 2012
  Joined: Nov 6, 2011
  Messages: 688
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 45
  tunavyong'ang'ania huo mpaka na hayo mafuta kama tuna nia nayo nzuri?
   
 11. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #11
  Oct 7, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  taarifa ya membe ina akili..
   
 12. k

  kisimani JF-Expert Member

  #12
  Oct 7, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 553
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Amirijeshi mkuu Lowasa tueleze mmejipangaje?
   
 13. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #13
  Oct 7, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  kuliko kudai ziwa ni lao, basi wangeda hata wakazi wote wa eneo la ziwa la tanzania ni wa malawi kidogo ingeleta sense
   
 14. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #14
  Oct 7, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  hata na mimi nimejiuliza hivyo hivyo.
   
 15. S

  Sangomwile JF-Expert Member

  #15
  Oct 7, 2012
  Joined: Aug 17, 2012
  Messages: 3,090
  Likes Received: 145
  Trophy Points: 160
  Kuna kitu wanakitaka.
   
 16. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #16
  Oct 7, 2012
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,803
  Likes Received: 2,576
  Trophy Points: 280
  Kutambua na kuenzi mipaka ya Berlin scramble for Africa conference kweli ndio our greatest shame as a people. We a are people,Afrika ni moja.
   
 17. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #17
  Oct 7, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,905
  Likes Received: 2,334
  Trophy Points: 280
  Ni vema wewe uka- surrender nyumba yako , mkeo na watoto kwa jirani yako akidai ulipo wewe ni kwake!
   
 18. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #18
  Oct 7, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,943
  Likes Received: 1,818
  Trophy Points: 280
  lakin nafikir kuna mkono a mtu nyuma yake juu ya hili and i doubt kuna hao wanaojua kuvuna rasilimali za waafrika wanatoa msukumo huo kwa hao wamalawi ili tu kuisumbua tz. kwani si tuwape kichapo tu wasepe zao?
   
 19. Nicole

  Nicole JF-Expert Member

  #19
  Oct 7, 2012
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 4,284
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  kuhusu boti ya kijeshi yatz kuonekana mpakan juzikat nilimwona mama banda akilalama tv mozambique alisema watz wameshajipanga kwa vita wameweka boti za kijeshi mpakani then wanapretend kutaka diplomatic solution so wao wanakwenda ICJ wapate haki yao
   
 20. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #20
  Oct 7, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,905
  Likes Received: 2,334
  Trophy Points: 280
  Membe has played his cards brilliantly so far.
  Huu ni mgogoro ambao akili pamoja na msuli wa kijeshi vinaendelea kutumika.

  In short Joyce anacheza mchezo ambao kwake ni wa kike zaidi.
  Membe jana ni alisema sula la mpaka na Malawi itabidi litatuliwe once and for all.
  Very good to state the end game.

  Katika sehemu tunayoidai tayari kuna doria na ndege za "uchunguzi" za Malawi zilishapigwa marufuku, na Malawi ika backdown.
  Doria inayofanywa ni ya vyombo vya Tanzania, iwe fishing patrols au vya kijeshi.

  ICJ, Tanzania hatuitambui, kwa hiyo Malawi watazidi kubanwa kwa options za kutatua tatizo hili.
  Kimsingi Malawi ni lazima watambue kuwa mwaka 1978, Mwalimu wakati huo alilipuuzia tishio la uvamizi toka Uganda, naona JK kwa sasa fundisho hilo analielewa fika. Vijana wako mipakani na Joyce analitambua hilo.

  The maneuvres, both diplomatic and on the ground are commendable.
  Keep it up!
   
Loading...