Membe kuwania urais 2015...

Namkubali
 
Yani atakayemrithi JK itakua ni chaguo la JK kwanini?? ndio kulindana huko sio....anamueka mtu wake ili amfichie madhambi na madili yake sio.....haya we!!
 

Bla bla
 
Wadau kama inavyofahamika Waziri Wa mambo ya Nje ndie anaekuwa Rais, Mhe. Maembe anajiandaa kumridhi JeiKei hapo 2015. imeshapangwa Kaarume ndo atakuwa Makamu wakati huo huo Mtoto wa Mkulima ataendelea kuwa PM. HABARI NDO HIYO
 
HAPO CHADEMA MLIE TU hamana chenu labda 2020.SLAA Kajipange upya kama 2020 utakuwa bado na nguvu ya kusimama jukwaani
 
Hivi na Membe anauota Uraisi? duuh! basi hata mimi nitakuja kuwa Rais 1 day.SERIOUS!
 
Ameshasikia sauti? maana amekaririwa mara kadhaa akisema kuwa bado hajasikia sauti ikimwambia agombee Urais
 
Tuache misimamo hasi na yenye harufu ya wivu.Dual Citizenship ni nafasi kwa watanzania wote waliopo hapa, waliopo nje badokama watanzania na walio na passport za nje, ni kwa wote hawa, ni kwawatanzania wote. Cho chote kizuri kwa mtanzania mwenzangu na ambacho ni halaikisheria yeye kupata hata kama sinufaiki nacho moja moja kwa moja ni wajibukukiunga mkono 100% (maana huenda rafiki au ndugu yangu akanufaika na kwa maanahiyo pia mtanzania yeyote ni ndugu). Ni wachache wanahitaji passport, mbonahatupingi uwepo wake ili iwe kwa safari za kiserikali tu. Tayari raia wa nje(ambao ndio wakuhofia au kuonea wivu) Tanzania inawapa uria (passport nimakaratasi ukweli tunamwamini tu kwa matumaini) - Sasa ni yupi wakuhofia kuwana passport ya Tanzania ni huyu mzawa wa nchi ya nje au huyu mzawa waMtanzania. Narudia tuache mtazamo hasi na wivu.
 

Mkandara,

Nadhani ugomvi mkubwa ni kwamba kiwanda kinajengwa jimbo la Membe wakati malighafi inapatikana Mchinga jimbo la Mudhihir kitu kama hicho..si unajua kila muamba ngoma
 
Mkandara,

Nadhani ugomvi mkubwa ni kwamba kiwanda kinajengwa jimbo la Membe wakati malighafi inapatikana Mchinga jimbo la Mudhihir kitu kama hicho..si unajua kila muamba ngoma

Maundumula hauko sahihi, Lindi mjini anakotaka Membe kijengwe kiwanda sio jimbo la Membe. Fanya utafiti kabla hujarukia keyboards!!
 
Maundumula hauko sahihi, Lindi mjini anakotaka Membe kijengwe kiwanda sio jimbo la Membe. Fanya utafiti kabla hujarukia keyboards!!

Ndio maana nilitumia neno "nadhani" kuonesha kwamba sipo certain.

Nashukuru kwa kunifahamisha.
 
Je anazo qualities zote za kiongozi? Ni zipi? Je ni kweli ana hasira? na itakuwaje watu ambao aliwakosea au walimkosea siku za nyuma? Maana mmoja kati ya sifa kuu za kiongozi ni kuwa mvumilivu ama sivyo itakuwa kila kukicha unanyonga watu.

Je wanaompinga wana mawazo gani kuhusu huyu mheshimiwa? Nazungumzia kuanzia akina Mudhihir mpaka waliopo madarakani juu.

Je tangu aingie Foreign kuna mabadiliko gani makubwa kashafanya?

Nauliza kwa sababu inaonekana kuwa kuna kila dalili anaweza kuwa rais wetu 2015 lakini je watanzania wategemee rais wa namna gani na presidency yake itakuwa ya namna gani?
 
Ameweza kufanya rais wetu atalii dunia nzima kwa kumuandalia safari hata ambazo hakustahili, kajenga hotel yake kule kwao, pia ni kiongozi ambaye yupo kuonewa huruma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…