Tetesi: Membe awakatalia Kardinali Pengo na Askofu Malasusa kumsamehe Musiba

2808007_IMG_20210613_182943.jpg
 
Wakati dalali wa Mahakama kampuni ya Yono (vijana wa kazi) ikihesabu siku zilizobaki katika 14 (siku za kazi) alizolewa mtukanaji Cyprian Majura Musiba kumlipa fidia Kachero Bernard Membe jumla ya shilingi 9.2 Bilioni, Bwana Musiba amewaangukia viongozi wa dini Askofu Alex Malasusa (KKKT Diyosisi ya Pwani) na Kardinali Porlycarp Pengo kumwombea msamaha kwa Membe asipige mnada mali zake.

Taarifa kutoka ndani ya familia ya Membe nyumbani kwake Mikocheni zinaeleza kwamba Jumatatu ya tarehe 24/4/2023 majira ya saa 10 alasiri mjumbe kutoka kwa Pengo alifika kwa Membe kumpa ujumbe wa Pengo kumsihi amsamehe Musiba.

"Alikuja hapa padre wa moja ya makanisa yetu kuleta ujumbe huo lakini naona Mzee alimkatalia na kumwambia 'namheshimu sana baba Askofu Pengo lakini kwenye hili anisamehe yeye (Pengo) huyu kijana lazima alipe gharama ya matusi yake' " anasema mwanafamilia aliyetajwa kwa jina la Colleta na kuongeza:

"Lakini jioni yake ya saa moja Askofu Malasusa naye alimpigia simu Mzee kuongelea suala hilo hilo lakini naye Mzee alimpa majibu yale yale aliyompa mjumbe wa Pengo." Hata hivyo kwa maelezo ya Colleta ni kwamba si tu ni msimamo wa Mwanadiplomasia huyo Bali ni msimamo pia wa familia.

Hii inakuja baada ya jitihada za Askofu Mwamakula pia kugonga mwamba baada ya kumwandikia barua Membe ya msamaha kwa Musiba.

Wakati hayo yakijiri hapa Mikocheni, tayari kampuni ya Yono imeshatua jijini Dodoma itakapoanzia kazi ya mnada kwa kuanza na apartments za Musiba zilizoko Ihumwa, nyumba yake ya Chamwino, guest house yake ya Msalato na shamba la hekari 10 njia ya Singida.

Baada ya hapo Yono atatimba apartment ya Kigamboni, shamba la hekari 5 Bagamoyo kabla ya kugeukia mitambo yake ya uchapaji iliyoko jengo la Exim ghorofa ya 8 jirani na Makao Makuu ya Polisi jijini Dar es salaam.

Ikumbukwe kwamba huko nyuma Musiba alichapa magazeti yake kampuni ya Malindi Printing huko Mbweni ambayo ni mali ya TISS. Jambo hili lilileta ukakasi wa kisheria kwani sheria ya vyombo vya habari (2016) inamtaka mlalamikaji kumshitaki Mwandishi, mhariri, mchapaji na msambazaji. Kwa mantiki hiyo DG wa TISS angetakiwa kusimama kortini. Ili kuokoa jahazi Musiba "alinunuliwa" mitambo mingine Mpya kutoka Ujerumani na kwa "huruma" mwana TISS Membe aliridhia. Nayo itanadiwa baada ya siku 14 kutamatika pamoja na nyumba na mashamba yake ya kijijini nakadhalika.

My take: Vijana tujifunze kitu katika sakata hili la Musiba na Membe kwamba tuwe na akiba ya maneno. Lakini pia akili ya kupewa changanya na zako. Waliokuwa wakimpa akili karibia wote wamemkimbia tena ndio wamekuwa jirani na Membe. Amtegemeae mwanadamu mwisho huwa kama hivi. Musiba kwishney!
Musiba nguvu za matusi yale alizipata wapi,most likely ni kutoka TISS ya Hayati Magufuli.Bahati yake mbaya Musiba ni kwamba hii ni TISS ya Samia.Kwa hiyo bad luck for him,sidhani kama itakuwa na msaada kwake.
 
Musiba hakuwa na kosa maana alichokuwa anakisema walikitenda ila kwa kuwa ndio wenye nchi hawataki kudhalilishwa hadharani kwamba walikengeuka. Akiendelea kulipiza kisasi juu ya Musiba Mungu naye atalipiza kisasi kwa kuwa baya halilipwi kwa ubaya ili umfundishe aliyekunda ubaya ajifunze kuwa na kiasi.
1. Musiba alimtenda vibaya mlalamikaji
2. Musiba aliwatendea wema Watanzania wengi kwa kuweka wazi uovu wa viongozi wa kisiasi wanapopewa dhamana ya kuwatumikia wanajinufaisha wenyewe
Mkuu,

Kwanza vitabu vinatuambia tutii mamlaka kama alijua Membe ni kiongozi mbona hakumtii?

Lakini mali zinauzwa kwa sababu alishindwa kutetea hoja(uozo) unasema Musiba aliwaambia wananchi. Kushindwa huko maana yake umemchafua mtu pasipo sababu, adhabu yake ndio hiyo. Na kwa sababu mali alizonazo amezipata kutokana na kuchafua watu wacha zichukuliwe walipwe waliochafuliwa. Hapo Karma ndio imefanya kazi. Umelipwa hela kwa kuwapakazia watu sasa fedha hizo zinaru kwa waliopakaziwa
 
Ungemuuliza Membe swali hili wakati kesi inaendelea. Lakini kama walivyofanya maaskofu ukaacha sheria ichukue njia yake kisha unatafuta dini ya Membe.!! Angeshindwa kesi hii bado ungetaka kujua dini ya Membe?

Lakini ningependa kukusaidia jibu. Membe ni mfuasi wa dini ya ukristo dhehebu la Roma. Kwa kufuata Imani yake akaomba amalize suala hili nje ya mahakama. Pia akaomba chama kisaidie kwa kuwaita yeye na Musiba. Katibu wa chama wakati ule Bashiru akagoma kukutana na Membe na akakataa kutomshirikisha Musiba. Badala yake Bashiru akatumia tuhuma za magazeti ya Musiba kumfukuza Membe chama, huku Musiba akiomba Membe akamatwe na avunjwe miguu kwasababu alikuwa anaandaa mapinduzi ya serikali ya mungu wa Chato.

Membe akabakiwa na risasi moja tu: mahakama. Mahakama ikamwona Musiba anakesi ya kujibu wakati mungu wake wa Chato akiwa hai. Musiba akasema mahakama isingeweza kumpa ushindi Membe labda mungu wake awe amekufa. Sasa Membe ameshinda wewe unauliza ni wadini gani? Ili iweje kwa wakati huu?
 
Membe itakua kafulia anataka hela hakuna kingine hapo nimemshtukia.
Naam. Nami nimewashtukia viongozi wa dini waliotumwa na Musiba kuwa ni wale wale waliotumika kipindi kile cha giza kumtukukuza mfalme na kuutakasa utawala wake wa giza! Bahati nzuri kachero anawafahamu fika.
 
Alifukarishwa kwa makusudi. Alipwe pesa zake kama wanavyolipwa wengine.
Yule ibilisi mwenye roho mbaya kuliko shetanj mwenyewe alimzuilia kuwa Katibu Mkuu wa Jumuia ya Madola kama alivyowazuilia marehemu Likwelile na Mulamula kufanya kazi Umoja wa Afrika! Badala yake akamtuma Musiba kumchafua. Achukue tu hizo mali; kwanza Musiba alifanya biashara gani kustahili kuwa na hizo mali? Hizo ni mali za nchi zilizoporwa kipindi kile cha giza kuwazawadia vichaa waliomtukuza na kumpigania mwenzao!
 
Hawa si Mungu, ni binadamu tu kama wengine......wasikataliwe wana nini cha kumzidi Membe?
Musiba amewacagua hao kwa kujua jinsi walivyokuwa pamoja kuupigania utawala wa giza. Kwa macho ya kibidamu bora hata Membe kuliko hawa kwani aliweza kujitenga na ubatili wa awamu ya tano; hawa waliwatelekeza kondoo na kusimama na shetani! Sijui hata wanapata wapi ujasiri wa kuwasiliana na Membe!
 
Yeye alidharau kumbe mwenzie yuko serious na anachokifanya. Sema una appeal vipi na records zipo. Utayakataaje maneno uliyoyasema au kuyaandika?

Kingine Membe ni mtu wa kuvimba na amepata chance ya kujivimbisha sababu utawala wa kwao huu. Alijitunisha kwa JPM ila hakufua dafu sababu system haikuwa upande wake. Karata zote ziko kwake sahizi alitingishwa sana ila nae amepata chance ya kumtingisha boya sasa
Siyo kweli kwamba Membe sasa amepata nafasi na kwamba walioko madarakani ni wezake! Ukweli ni kwamba vyombo vya nchi sasa angalau vimeanza kutekeleza wajibu wao. Kabla ya hapo vyombo vyote vilikuwa butu vikitumikia maslahi ya kisiasa ya mtu mmoja na genge lake la mashetani. Kesi kama hii ya Membe ingefutwa haraka kwa amri kutoka juu au angepangiwa wale majaji wa voda fasta wanaotoa hukumu bila kunukuu vifungu vya sheria.
 
Wacha historia iandikwe vizuri kijana huyu mjinga alitukana vibaya huku akitishia hata kuua hafai kabisa kuachwa hivihivi... Alipokuwa anatukana askofu hakuna na kukemea Leo anajiingiza kumwombea msamaha wanini?? Musiba anastahili kuvuna alicho panda!! Alitukana watu na kuwazushia mambo ya hovyo mitandaoni hadharani na mpaka Leo hajarudi mtandaoni kuomba msamaha na kufuta maneno machafu yaliyomtoka kisa kusaka umaarufu!!!
Viongozi wa makanisa wawe makini kabla ya kuingilia mambo au wataishia kutumika vibaya na kushusha heshma Yao.
TAFADHALI NDUGU MEMBE MIMI NIMMOJA YA WATU TULIOKUSAPOTI TOKA UKIWA WAZIRI MAMBO YA NJE,HUYU KIJANA ANADHARAU NA KIBURI KIBAYA MWACHE AWE FUNZO KWA VIZAZI VIJAVYO JINSI SHERIA INAWEZA KUMSHUKIA YEYOTE ANAYETUSI NA KUCHAFUA VIONGOZI WALIOIPIGANIA NCHI NA KUJITOA KUIJENGA...
 
Upuuzi tu sijaona sehemu Musiba ameomba radhi Nini kuhangaika viongizi wa dini Kuna wakati wanatakiwa kuacha unafki Musiba anatukana wako kimya Tena wanasifia tu,Musiba anaombwa aombe radhi wao kimya ,Musiba amepelekwa mahakamani kimya,mahakama inatoa hukumu kimya Membe anataka kukaza hukumu hao...kwani wametumwa na nani
 
Back
Top Bottom