Membe amshukia KITINE, amfananisha na "Kingwendu"


Duh, kumbe wala hujui kwanini aliita waandishi wa habari na bado unanguvu ya ku draw conclusion ya kwanini aliita waandishi! Unanikumbusha mtoto wa rafiki yangu moja, siku moja rafiki yangu akamwambia mtoto wake "vaa vizuri na ingia kwenye gari", mtoto akasema "sawa baba". Akaenda kuvaa vizuri na kurudi nakuingia kwenye gari, wakiwa wanatoka getini mtoto akamuuliza babake "hivi baba tunakwenda wapi?" Babake akasema "eboh! sasa wewe ulifikiaje hatua ya kuvaa, kuingia kwenye gari na kufunga mkanda bila kujuwa unakwenda wapi?"
 

Nahisi umekurupuka kujibu comment yangu nadhani WJM anajua nini nilikuwa namaanisha, ulichofanya wewe ni kujaladia tuhuma za kitine kwa kuziita facts ambapo sijui proof/details za uhakika nizipate wapi labda waweza kunisaidia,sakata hilo nalikumbuka ila sina kumbukumbu nzuri kuhusu undani wake, anyway let me do my homework!
 
Membe mnatuficha wewe na JK ndugu wa DAMU. Tunaelewa mamake Kikwete ni mama yako pia.
Tukikuchagua tutakuwa tumechagua msanii namba mbili!! HATUKUHITAJI JOKA LA MDIMU.

Kastarehe fanya homework kidogo basi kabla hujatapika. Membe hana chembe ya undugu na JK, au kama Elimu yako haitoshi kiganjani kwako basi uliza huko Rondo, Lindi anakotoka Membe au Msoga, Pwani kwa JK. Adithi za vijiweni vinashusha thamani ya JF na kutufanya tuwe mbali na great thinkers.
 

Mkuu, ni wezi wangapi ambao wametajwa waziwazi na vielelezo kuwekwa bayana (wizi wa EPA), lakini hakuna hatua zilizochukuliwa zaidi ya kusamehewa kabla hata ya kuhukumiwa??!!!!
Au unaizungumzia Tz ya kufikirika?
Wacha watu warushe mawe gizani, litakayempata atatoa kilio cha sauti na ndipo watu watamjua kwamba kumbe fulani naye alikuwemo!!!
 


Membe amewapa fact alizozipata kwa kukaa Canada...lakini you didn't do your home work properly......re seat!
 

Labda nikusaidie kwenye hiyo homework:

Juu ya PhD ya Kingwendu, hilo sio tatizo search kwenye shule aliyosema kasoma na watakupa facts, njoo zimwage hapa hata kama hazinogi

Juu ya kutimuliwa madarakani, hilo utahitaji msaada wa wanausalama wa taifa ili upate details za deal la magari aliyoiba. Ila facts amabayo iko wazi ni kwamba alifukuzwa kazi na Nyerere.

Juu ya Kingwendu kuiba $63,000 hii unaweza kuanza kumuuliza dokta msingiziwa, Doctor Charles Peter Arizona teaching hospital (ambaye wakati huo alikuwa mwanafunzi wa mwaka wa pili wa udaktari), ukitoka hapo muulize nurse msingiziwa, Stevenson White wa clinic moja huko Seattle jina sasa nimesahau (huyu masikini alikuwa mwaka wa kwanza nurse). Ukimaliza hapo check na Ulimwengu aliyekuwa anavujishiwa kila move za Kingwendu katika kukamilisha wizi huu kutoka kwa marehemu Ng'ittu wa usalama wa taifa (RIP)

Ukishindwa kupata data huko njoo kwangu
 
- Mkuu I like your arguments kwa sababu upo fair kidogo, lakini kama kweli Kitine amelipa the price na ameridhka kwamba alifanya makosa na ni lazima kulipa price, then asingekwua na visasi hivi, maana CAG imeonyesha wazi nani ni nani!

William.

Williama, hata kwenye legal system (including USA) mtuhumiwa/mwizi anaweza kupata huruma (i.e kupunguziwa muda wa kifungo) in exchange na information ambazo zitasadia kukamata wahalifu wengine. Kama Kitine alikamatwa na akalipa price (akapoteza uwaziri) leo hii tukatae taarifa za potential wizi kwa sababu huko nyuma yeye Kitine aliiba?

Ili hoja inayosema kwamba Kitine ni muongo ana analipa visasi basi ni vizuri tukapata evidence kwamba kati ya mawaziri/naibu mawaziri 51 wa Tanzania hakuna hata mmojawao aliyepokea hela toka huko kuliko tajwa! Na inakuwaje kati ya mawaziri/naibu mawaziri 51 Membe aamue kutunga kujibu tuhuma za Mzee Kitine? Membe ni msemaji wa mawaziri wote?

Hata kama waandishi wa habari walimuuliza swali linahusiana na madai ya Mzee Kitine, kama hafamu angesema hafamu, lakini story za king'wendu zinageuza the entire equation na innocence ya Membe inakuwa under the spotlight.

Hii movie wala haijaanza, ndio kwanza tuko kwenye foleni ya kununua popcorn!
 
Hii movie wala haijaanza, ndio kwanza tuko kwenye foleni ya kununua popcorn!

Husipoteze ela kununua popcorn, Kingwendu anakimbia waandishi wa habari, na soma Nipashe ya leo. Starling wa movie hii ametoweka na wala hutamsikia tena. Kwenye movie ukiona starling anajitundika juwa movie imeshafika mwisho na kinachofuata ni majina ya washiriki wa movie tu, kwa mfano utaona wameandika Philemon aikael Mbowe = mshika taa, nk
 
kitine alisema mawaziri wote ni wezi kwa hyo ni pamoja na membe lkn mbona wenzake wote hawajajibu kajibu yeye tuu.
 

afadhali ya wewe hoja zako seems palatable na sio yule frozen mind WJM!
 

Sidhani! Keshatoa matangazo na posters ziko kila mahali, movie lazima!
 
Mi nadhani membe alitakiwa ajibu kama anajenga hotel ya mabilioni huko Mtwara au hajengi. Maana hiyo hotel inayojengwa inatisha, amekuwa akiingia usiku huku akitumia gari ambalo ni tinted wakati anakagua. Aseme ukweli kama anasingiziwa.
 


- The ishu hapa ni Kitine sio EPA, halafu tizama huna uhakika na inaelekea meaning hujui unachosema, sasa naomba uulize wka wengine kwa nini Mkapa rafiki wa karibu sana wa Kitine, aliyemrudisha toka Canada, akamrundikia mivyeo kushoto na kulia, akafikia hatua ya kumfukuza mivyeo yote kwa ajili ya hii saga?

- Sasa nido utaijua JF, wacha kukurupuka!

William.
 
huyu william anapenda kujipendekeza kwa viongozi kama mwana mkeau anataka hurumaza kuteuliwa na wakuu? haoni hata ubunge wa kuteuliwa kaukosa? au kapewa u dc sijaona list
 
Mkuu wangu tuhuma ulizomshushia willy na wazazi wake ni kubwa sana inabidi uziletee ushahidi.

Kuhusu Anne Kilango na mumewe kupewa fedha za EPA, hayo yalizungumzwa na Sophia Simba kwenye kikao cha chama tawala wakati huo akiwa waziri wa utawala bora!! Kilango alitishia kwenda mahakamani kumshitaki lakini mpaka leo kimyaaa........ Sasa unataka ushahidi gani zaidi ya kauli ya waziri mwenye dhamana ya kusimamamia TISS na Takukuru?
 
..sidhani kama Col.Kitine amezusha tu suala hili.

..nadhani kinachokosekana ni watu wa ku-cooperate kuweka ushahidi hadharani.

..Membe naye anatumia mafumbo kujitetea kwasababu he doesnt know exactly Col.Kitine ana ushahidi gani dhidi yake.

..tatizo lingine la Membe ni kwamba yuko so incoherent. Yaani akielezea kitu chochote kile huzunguka wee mwisho hupotea kabisa na kusahau hata aliulizwa nini.
 
Haihitaji kwenda shule ili kujua kuwa serikali hii tangu mwanzo iliundwa na wezi, mtu yeyote mwadilifu asingekubali kuteuliwa kuwa waziri ktk serikali ya kijambazi kama hii, iliingia madarakani kwa hela za wizi (epa na ndugu zake wote), walipoingia tu kiongozi wao akapiga mchongo wa richmond, hakuna mwadilifu mwenye akili timamu atakubali kuwa waziri ktk serikali inayoundwa na wezi na vibaka watupu. Membe alishashindwa kazi tangu siku ya kwanza, ndo maana mishemishe zote za wizara ya nje zinafanywa na m-kwere. Kama membe angekuwa na ufahamu hata kdg angeshaachia ngazi zamani lkn yuko pale kwa sababu ya posho na michongo wanayopiga. Na kwa wanaong'ang'ania kuwa mzee Kitine amtaje waziri aliyemkusudia.... Wale mafisadi wote ambao mmeshatajiwa mmewafanya nini?!
 

Time well wasted
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…