Membe akanusha kuitabiria CHADEMA ushindi 2015!!

Membe akanusha kuitabiria CHADEMA ushindi 2015!!

siasa za Tanzania bwana, yaani mh wangu huyu hakumbuki alichoongea na viongozi wa chadema huku ITV waki mrekodi? au kuna kitu kakiona hakijkaa vizuri? hebu ajaribu kurudi kwenye kumbu kumbu ya mkanda au Cd halafu aangalie na asikilize aliongeanini siku ili aweze kujua cha kuongea baada ya hapo.
 
Hivi anachokanusha hapa Membe ni kitu gani. Vyombo vya Habari vinavyoaminika viliandika na kutangaza maneno ya Membe. Wazi kabisa. Hawakuongeza wala kupunguza. Wangefanya hivyo wangekuwa wanakiuka misingi muhimu ya tasnia muhimu ya uandishi wa habari. Angekuwa na haki ya kuwashtaki (ofcourse MCT).

Kwa mtu yeyote makini hapa kaongeza tu stori nyingine, AMEPINGANA NA PROPAGANDA ZA HOVYO, CHEAP ZA CHAMA CHAKE CCM na wana CCM wenzake. Stori juu ya stori. Asante Membe. Tusubiri kesho watakuandikaje au leo jioni kwenye Tvs zetu.

Ofcoz with the coming back of Andrew Chenge on board and the like wakiendelea kujipatia nguvu katika Kamati za Bunge na sasa wakielekea kuliteka bunge, baada ya kuwa wameishaiteka ikulu, wakaiteka CCM na wameiweka mfukoni serikali ya CCM, watu kama Membe hawana namna sasa hivi isipokuwa kujionesha kuwa wako upande wa wanamabadiliko!

Mtu kama Membe na wenzake ni wa kuazimwa milango yote ya fahamu, kwa tahadhari kubwa hata wanachosema (kwa kuchelewa sana) ni ukweli.


Kama nimesoma na kuelewa vema kauli ya Membe, wengi wanaweza kukubaliana nami kuwa Membe hapa kajibu kisiasa huku akikubali yaliyotokea kwamba aliwakaribisha vijana wa Chadema na kwamba upinzani si uadui, na tusigenganishwe na ghiliba za ubaguzi.

Mimi sihitaji kudadisi zaidi kwani Membe kaongea wazi na mwenye kuijua falsafa hiyo anajua jibu alilotoa Membe.
 
He still adds no value. Ameendelea ku-cement tu yaliyoandikwa. Ok bado APRM hapa tunaipitia, je vipi kuhusu kuwa tunadaiwa Dola Laki 8...?

How long it took for him to comment on APRM & Tanzania mishap? Yaani waandishi wa habari waliamka asubuhi na kuamua kwamba report ya Tanzania haitosomwa kwa sababu ya deni? Wizara nyingi zinadaiwa TANESCO, NHC na Foreign Affairs wamo kwenye orodha ya wadaiwa sugu. Hivyo APRM ni mwendelezo only to find out kwa wenzetu hakuna ngonjera, pay your dues or else!
 
siasa za Tanzania bwana, yaani mh wangu huyu hakumbuki alichoongea na viongozi wa chadema huku ITV waki mrekodi? au kuna kitu kakiona hakijkaa vizuri? hebu ajaribu kurudi kwenye kumbu kumbu ya mkanda au Cd halafu aangalie na asikilize aliongeanini siku ili aweze kujua cha kuongea baada ya hapo.

Mbona maelezo yake ni kuwa chakula kililiwa nyumbani kwake sasa hao itv walirekodia wapi? Isitoshe amesema walipita kwake wakakuta ni wakati wa kula akawakaribisha, sasa hiyo itv ilikujaje kujaje na haukuwa mkutano rasmi
 
How long it took for him to comment on APRM & Tanzania mishap? Yaani waandishi wa habari waliamka asubuhi na kuamua kwamba report ya Tanzania haitosomwa kwa sababu ya deni? Wizara nyingi zinadaiwa TANESCO, NHC na Foreign Affairs wamo kwenye orodha ya wadaiwa sugu. Hivyo APRM ni mwendelezo only to find out kwa wenzetu hakuna ngonjera, pay your dues or else!

Unataka kusemaje? Kuna sifa gani katika kulipa madeni ya APRM ilihali hakuna fedha za kutosha za kulipia utilities na activities ubalozini? Kwanza the fact of the matter ni kuwa hakuna regulation wala rukes of procedures inayomnyima haki ambaye hajatoa mchango wake kushiriki vikao since APRM ni voluntary initiative. Point hapa ni kuwa, Tanzania haitawasilisha ripoti yake kutokana na APRM yenyewe kutokamilisha mchakato wao wa kuipitia hadi sasa mwezi Juni wakati ilitakiwa kuwasilishwa Julai. Hivyo, nilichopata kwenye press conference hii ni kuwa sio deni bali delay za kukamilisha ripoti
 
MEMBE+AKISALIMIANA+NA+WAJUMBE+NACHINGWEA.jpg

Na Mwandishi wetu



19th June 2012







Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe, amekanusha tuhuma dhidi yake kuwa amekitabiria ushindi Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wakati wa uchaguzi mkuu ujao.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam jana, Membe, alisema wakati ambao alikuwa Uingereza kuna maneno yaliyokuwa yakienezwa kwamba aliitabiria ushindi Chadema mwaka 2015.

“Napenda kusema kwamba sijatabiri ushindi kwa Chadema wala mtu yoyote na mimi siyo mtabiri” alisema Membe.

Alisema hajawahi wala haamini kama Chadema ndio waliosema jambo hilo ila kuna mkono wa mtu, ambaye ahata hivyo hakumtaja.

Alisema yeye ni mwanachama wa mtiifu kwa CCM na kwamba tuhuma hiyo ina lengo la kumtifitinisha na CCM.

Akizungmzia kuwakaribisha Chadema alisema: “Ni ukarimu tu na ukarimu hauna chama wala itikadi na pia naamini upinzani sio uadui bali ni ushindani wa nguvu za hoja.”

Alisema maadui wa CCM wako ndani ya chama chenyewe na wanafanya ni sawa na kujitafuna wenyewe.

Alisema alienda kwenye jimbo lake la Mtama ili kufukia mashimo yaliyokuwa yameachwa na Chadema na siyo kukiunga mkono chama hicho cha upinzani.

Pia Waziri membe alizungumzia swala la taarifa juu ya upotevu wa fedha katika wizara yake ambapo alisema Januari Mosi mwaka huu wakati yeye, Naibu Waziri, Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu na Afisa masuhuri hawakuwepo na waliokuwa wanakaimu nafasi zao waliidhinisha fedha za ziara ya Rais Sh. bilioni 3.5 na hivyo kuwepo kwa taarifa za kutoaminika juu ya matumizi na uwepo wa fedha hizo.

Waziri membe alisema kuwa wao kama wizara waliamua kufanya utafiti kama waliofanya hivyo walifuata taratibu za kifedha na kiutawala.

Alisema kamati hiyo kwa kushirikisha wakaguzi wa fedha, Takukuru,Usalama wa Taifa walibaini hakuna fedha yoyote iliyobainika kuwa kuibiwa.




CHANZO: NIPASHE
 
Back
Top Bottom