Kiganyi
JF-Expert Member
- Apr 30, 2012
- 1,242
- 765
Bernard Membe
Nimefafanua kuhusu uvumi uliotolewa na vyombo vya habari kuhusu kukutana kwangu na vijana wa CHADEMA waliofika nyumbani kwangu jimboni
Bernard Membe
Nimewaeleza kuwa upinzani si uadui na wapinzani si maadui zetu.
Bernard Membe
Sijawahi kuitabiria CHADEMA ushindi kwa kuwa sina kipaji hicho ambacho kinapatikana kwa Synovate, Mtoto wa Sheikh Yahya na TD Joshua
Bernard Membe
Upinzani upo kwa mujibu wa kanuni, sheria na Katiba hivyo hauwezi kuwa uadui. Wapinzani wako ndani ya vyama vyetu wenyewe
Bernard Membe
Nina imani uvumi huu haujaenezwa na CHADEMA bali watu nje ya CHADEMA wenye malengo ya kisiasa haswa kunifitinisha na wana CCM na CHADEMA
Bernard Membe
Kamwe watanzania tusikubali kulishwa kasumba ya kuwa Upinzani wa kisiasa ni uadui. Tusigawanywe kwa itikadi wala dini
Bernard Membe
Nawapenda watanzania wote bila kujali itikadi zao, dini zao, makabila yao na marika yao. Umoja wetu ndio nguvu yetu.
MY TAKE; Nyoka ya MDIMU haiaminiki au Magazeti yalizusha hizo taarifa??
Magamba wengine igeni toka kwa Membe kuwa na political tolerance!

Bahati nzuri mimi nimeshiriki press Conference hii. Mhe. Membe alitumia fursa hiyo kutoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali kuhusu Wizara ambayo yamekuwa yakiandikwa na kutangazwa na vyombo vya habari isivyo.
Masuala hayo ni pamoja na taarifa kuhusu uwasilishwaji wa Ripoti ya Tanzania kuhusu Mpango wa Nchi za Afrika Kujitathmini Kiutawala Bora (APRM).
Katika suala hili Mhe. Membe alitoa ufafanuzi kuwa, ni kweli Mhe. Rais hatoweza kuwasilisha ripoti ya tathmini ya Tanzania katika Mkutano ujao wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) unaotarajiwa kufanyika mjini Addis Ababa mwezi Julai, 2012 kwa kuwa Timu ya Umoja wa Afrika chini ya APRM inayopitia ripoti hiyo ya Tanzania haijakamilisha kazi hiyo. Hivyo Tanzania itawasilisha ripoti yake Januari 2013baada ya timu hiyo kuipitia na si kwa sababu Tanzania inadaiwa Dola za Marekani laki nane (800,000) kama mchango wake kwa mpango huo.
"APRM ni chombo kilichoanzishwa na Serikali za Afrika na kwa hapa Tanzania kinaratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje, ni chombo cha hiari kwa nchi za Afrika kujitathmini zenyewe kiutawala bora, si kweli kuwa Rais atashindwa kuwasilisha Ripoti ya Tanzania AU kwa sababu hatujalipa deni, bali ni kwa sababu timu inayopitia ripoti hiyo ya Tanzania haijakamilisha kazi yake hivyo tunatarajia kuwasilisha ripoti yetu mwezi Januari 2013 wakati wa kikao kingine cha Wakuu wa nchi wa AU," alisema Mhe. Membe.
Kuhusu suala la fedha zilizotoweka Wizarani, Mhe. Membe alieleza kuwa hakuna fedha zilizopotea isipokuwa Wizara imewasimamisha kazi Watumishi watano waliofanya mchakato wa kuhamisha kiasi cha shilingi bilioni 3.5 kutoka Hazina kuja Wizarani kwa ajili ya ziara za Mhe. Rais za Addis Ababa, Geneva,…na Arusha bila kibali cha Afisa Masuuli yaani Katibu Mkuu ambaye hakuwepo wakati mchakato huo unafanyika.
Aliongeza kuwa, Watumishi hao wamesimamishwa kazi ili kupisha uchunguziunaofanywa na kamati iliyoundwa ili kujiridhisha kama taratibu za kifedha zilifuatwa au kukiukwa katika mchakato huo mzima.
"Tarehe 1 Machi, 2012 wakati mimi sipo Wizarani wala Naibu Waziri, Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu na Mhasibu Mkuu kuna mchakato wa kuhamisha fedha kiasi cha shilingi bilioni 3.5 ulifanywa kutoka Hazina kuja Wizarani kwa ajili ya safari za Mhe. Rais za Geneva, Addis Ababa,…..na Arusha bila kibali cha Afisa Masuuli. Timu inayojumuisha watu kutoka TAKUKURU, Usalama wa Taifa, Wizara na Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali imeundwa ili kuchunguza suala hilo ili kujua kama taratibu za kifedha zilifuatwa au kukiukwa na uchunguzi ukikamilika tutaweka hadharani hakuna cha kuficha," alisema Mhe. Membe.
Vile vile, Mhe. Membe alipinga uvumi unaoenezwa kuwa amekitabiria ushindi Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015 kwa kusema kuwa yeye si mtabiri na kwamba yeye ni mwanachama halisi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa maneno na kwa matendo.
Mhe. Membe aliongeza kuwa alichokifanya ni ukarimu kwa kuwakaribisha Vijana wa CHADEMA jimboni kwake Mtama mkoani Lindi na kushiriki nao chakula nyumbani kwake.
"Ukarimu hauna udini, rangi wala itikadi, vijana wa CHADEMA walikuja nikawakaribisha kwa chakula nyumbani, na leo nataka niwape somo kidogo, upinzani sio uadui, nchi inayoona upinzani ni uadui haiko salama wala haitaendelea,"alisisitiza Mhe. Membe.