inasemekana MV seagul ikitokea Dar kuelekea zanzibar imezama. kila tupato habari tutazidi kuhabarishana
Update:
Ilikua na abiria 200 na juhudi za uokoaji zinaendelea na tayari baadhi ya watu wameokolewa wakiwa hai na wengine bado wanaelea wakiwa na maboya. Taarifa za vifo bado hazijathibitishwa japo ukweli ni kwamba vifo vipo. Meli hiyo imewahi kuripotiwa kuwa mbovu mara kadhaa.
View attachment 59156
Hivi huyu mzee ile kafara ya mwanzo aliyotoa haikutosha mpaka watoe tena kafara mara ya pili jamani??????????
Yani CCM imeona hili la kutoa roho za watu kwa njia ya kafara ndo suluhisho siyo. Toeni kafara rukeni juu ila chini mtatua tuu.
Mwenyezi mungu awajaze nguvu wote waliopatwa na mkasa huu. Uzembe wa serikali ya ccm ulaumiwe
Serikali isiyoweza kusomesha watu wake (failures kibao), isiyoweza kulinda watu wake hata dhidi ya ajali za Kizembe (ajali za magari na meli), isiyoweza kutibu watu wake(migomo ya Madakaktari) .Isiyoweza kulisha watu wake (kushuka kwa Tsh), Inaweza nini?
Mipango ya Mwenyezi Mungu bwana,haiepukiki..Tuzidi kusali tu.
Give me a break!!!
Zomba sio kwamba hiyo meli ilikuwa na shehena kubwa ya pombe na allah hapendi mambo ya kinywaji?
SUMATRA isilaumiwe katika hili. Zanzibar ina mamlaka yao ambayo inahusika na usafiri wa majini na pia usajiri wa meli. Ilifanya hivyo ili kuwa na mamlaka binafsi kwa Zanzibar na kuepuka kuingiliwa katika masuala ambayo wao wanaona si ya Muungano. Kwa nini basi hatari inapojitokeza suala linabadilishwa na kuwa la Muungano? Mchumia janga hula na wa kwao!
Meli iliosababisha ajali iko mahakamani naomba msiizungumzie...
Uliyopata ajali sio Meli ni Boti usichanganye mambo.
acha kumpotosha mwenzio! Ni sawa na kubisha kwamba imepata ajali Coster na sio Basi! Meli na Hiyo unayoita boti zote ni Marine Passengers' Vehicle. So umemwelewa ila unataka kujenga ubishi tu.
nadhani mkuu kama ulivyootea jana ndo hayo tunayashuhudia,takwimu hazieleweki.....tunaomba taarifa tuzipate hapa maana tukisuburi vyombo vya CCM vitatupa taarifa si za kweli kama kawaida yao
achana nae huyo ana mtindio wa ccm....acha kumpotosha mwenzio! Ni sawa na kubisha kwamba imepata ajali Coster na sio Basi! Meli na Hiyo unayoita boti zote ni Marine Passengers' Vehicle. So umemwelewa ila unataka kujenga ubishi tu.
wewe garasa una matatizo sana......Uliyopata ajali sio Meli ni Boti usichanganye mambo.
Hili swali ni la msingi kwa Waziri wa mambo ya Muungano. But siku tatu za maombolezo kwa Zanzibar si lazima zikawa sawa na zile za muungano. Hapa kuna Muungano na kuna Nchi.Hivi huu msiba wa Zanzibar peke ya au mpaka Tanzania bara, Zanzibar wametangaza siku 3 za maombelezo Tanzania bara wapo kimya au ndio nchi mbili kila moja na mamlaka yake.