Meli kubwa zaidi duniani Freedom Ship

Meli kubwa zaidi duniani Freedom Ship

Rugby Union

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2012
Posts
402
Reaction score
255
Moja kati ya kampuni nyiiingi iliyopo Florida nchini Marekani imekuja na wazo la kujenga meli iitwayo ‘Freedom Ship' itakayokuwa na kila kitu cha kuifanya iwe jiji linaloelea juu ya maji. Wabunifu wa wazo la meli hiyo wametoa michoro ya picha za meli hiyo itakavyokuwa pindi itakapokamilika.

meli-pic1.jpg


Roger M Gooch, ambaye ni mkurugenzi na makamu wa Rais wa kampuni ya Freedom Ship International ambao ndio wenye mradi huo, amesema hiyo meli itakuwa ndio meli kubwa kuwahi kujengwa, iliyo na muonekano wa jiji la kwanza linaloelea kwenye maji.

meli-pic6.jpg


Kutakuwa na uwanja wa ndege juu ya meli hiyo, uwanja utakaowezesha ndege kuruka na kutua wakati wakati meli inatembea Mkurugenzi na makamu wa Rais wa kampuni hiyo Gooch, amesema kampuni yake inaendelea kukusanya kiasi cha yuro milioni 600 ni sawa na dola bilioni moja zinazohitajika kuifanya ndoto hiyo iwe kweli aliongeza.

meli-pic3.jpg


Meli hiyo inayotegemewa kuwa na ghorofa 25, itakuwa na uwezo wa kuwapa makazi ya kudumu watu 50,000, lakini itakuwa na nafasi ya ziada ya kupokea wageni wengine 30,000, makazi 20,000 ya wafanyakazi wa meli, na mengine 10,000 kwaajili ya wageni wa usiku mmoja.

meli-pic4.jpg


Freedom Ship, itakuwa na huduma zote za jiji kama vile Shopping center, shule, hospitali, uwanja wa ndege, casino, maegesho ya magari na mengine mengi. Hii ndio njia inayotarajiwa kutumiwa na meli hiyo kuizunguka dunia Meli hiyo itakapokamilika inatazamiwa kuzunguka dunia nzima kupitia nchi moja hadi nyingine, bara moja hadi jingine Afrika ikiwemo na haitakuwa ikikaa sehemu moja kwa muda mrefu.

meli-pic5.jpg


Meli hiyo itakuwa na huduma zote za muhimu zinazopatikana katika majiji mbalimbali zikiwemo hospitali, shule, maduka, parks, casino, aquarium, kiwanja cha ndege chenye njia ya kuruka na kutua ndege ndogo zenye uwezo wa kubeba watu 40, kitakachokuwa juu kabisa kwenye paa la meli hiyo.

meli-pic7.jpg


Hii meli itakuwa ikitumia umeme wa solar pamoja na ule wa wave energy. Itakapokamilika, itakuwa na upana wa futi 750, urefu wa kwenda juu futi 350, pamoja na urefu wa futi 4,500 ikiwa ni mara nne ya Queen Mary II Cruise ship iliyokuwa na urefu wa futi 1,132.

meli-pic2.jpg


Cha ajabu zaidi wageni na wenyeji wanauwezo wa kuondoka na kuingia kwenye jiji hilo linaloelea majini kwa ndege au boti ziendazo kasi. Freedom Ship ni Meli kubwa kulikozote duniani itakayotumika kwa usafirishaji kama jiji linaloelea Meli hii inatarajiwa kugharimu dola bilioni 10 mpaka kukamilika kwake, na itakuwa na uzito wa tani milioni 2.5, lakini mpaka sasa bado ni wazo.

Chanzo: Bongo5
 
Wafanye tu.
Maendeleo yanakuja baada ya kugeuza impossibles kuwa possibles.
 
Duuu...ulaya kutabaki kuwa ulaya mpaka mwisho wa dahari.
 
Back
Top Bottom