Melchizedek na utata unaomzunguka

HaMachiach

HaMachiach

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2015
Messages
2,825
Points
2,000
HaMachiach

HaMachiach

JF-Expert Member
Joined Dec 15, 2015
2,825 2,000
Safi,fanya hivyo ili tupate faida.
Wimbo Ulio Bora:8.10
Mimi nalikuwa ukuta, Na maziwa yangu kama minara; Ndipo nikawa machoni pake Kama mtu aliyeipata amani.
Wimbo Ulio Bora:8.11
Sulemani alikuwa na shamba la mizabibu huko Baal-hamomi Akawakodisha walinzi hilo shamba lake la mizabibu; Kila mtu atoe vipande elfu vya fedha kwa matunda yake.
Wimbo Ulio Bora:8.12
Shamba langu la mizabibu, lililo langu mimi, li mbele yangu. Basi, Sulemani, wewe uwe na elfu zako, Na hao wayalindao matunda yake wapewe mia mbili.
 
zitto junior

zitto junior

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2013
Messages
10,626
Points
2,000
zitto junior

zitto junior

JF-Expert Member
Joined Oct 7, 2013
10,626 2,000
Mnajuaje kama iko sawa yaani mizani yenu ya usawa ni ipi ?

Je katika hiyo nyimbo marejeo yake ni katika Injili au Torati au Zaburi ?
Rejea ni vitabu vyote vya agano la kale kuanzia Torati hadi manabii Isaya hadi malaki.
 
zitto junior

zitto junior

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2013
Messages
10,626
Points
2,000
zitto junior

zitto junior

JF-Expert Member
Joined Oct 7, 2013
10,626 2,000
Mwandishi anatambulika sema wewe humtambui anaitwa mfalme Suleiman Mwana Wa Daudi
Hapana mkuu nitafutie scholarly Paper yoyote inayoprove hii..... Wimbo ulio bora ni classified as Pseudepigrapha same as Hebrews.

Kma ww ni mwanatheolojia utanielewa kuwa category hii ina maanisha uandishi na dating yake ni tofauti na content yake...... Yaani mwandishi tofauti ila anajitambulisha kma historical figure ili kupata uhalala.

Wimbo umeandikwa 200 BC thus miaka zaidi ya 600 toka Mfalme Suleiman afariki!! How can it be imeandikwa na solomon??

It's a Pseudepigrapha!!
 
HaMachiach

HaMachiach

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2015
Messages
2,825
Points
2,000
HaMachiach

HaMachiach

JF-Expert Member
Joined Dec 15, 2015
2,825 2,000
Ule wimbo ni Wa Suleiman mwenyewe au ni seme ni Maneno ya Suleiman nmeweka vifungu hapo juu pia Hebrew kiliandikwa na mtume Paul japo swali hili limeulizwa maranyingi
Hapana mkuu nitafutie scholarly Paper yoyote inayoprove hii..... Wimbo ulio bora ni classified as Pseudepigrapha same as Hebrews.

Kma ww ni mwanatheolojia utanielewa kuwa category hii ina maanisha uandishi na dating yake ni tofauti na content yake...... Yaani mwandishi tofauti ila anajitambulisha kma historical figure ili kupata uhalala.

Wimbo umeandikwa 200 BC thus miaka zaidi ya 600 toka Mfalme Suleiman afariki!! How can it be imeandikwa na solomon??

It's a Pseudepigrapha!!
 
HaMachiach

HaMachiach

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2015
Messages
2,825
Points
2,000
HaMachiach

HaMachiach

JF-Expert Member
Joined Dec 15, 2015
2,825 2,000
Conclusion
Melkizedeki, ambaye jina lake linamaanisha "mfalme wa haki," alikuwa mfalme wa Salemu (Yerusalemu) na kuhani mkuu zaidi wa Mungu (Mwanzo 14: 18-20; Zaburi 110: 4, Waebrania 5: 6-11, 6: 20-7: 28). Melkizedeki huonekana ghafla na kupotea katika kitabu cha Mwanzo ni ajabu kwa kiasi fulani. Melkizedeki na Ibrahimu walikutana kwanza baada ya Ibrahimu kushindwa kwa Kedorlaoma na washirika wake watatu. Melkizedeki iliwasilisha mkate na mvinyo kwa Ibrahimu na watu wake walokuwa wamechoka, kwa kuonyesha urafiki. Yeye alitawaza baraka kwa Ibrahimu kwa jina la El Elyon ("Mungu aliye juu zaidi") na kumsifu Mungu kwa kumpa Abraham ushindi katika vita (Mwanzo 14: 18-20).

Ibraham alimpokeza Melkizedeki na zaka ( fungu la kumi) ya vitu vyote alivyokuwa amesanya. Kwa kitendo hiki Ibraham alionyesha kuwa alitambua Melkizedeki kama kuhani ambaye nafasi yake ya kiroho ilikuwa juu kuliko yake.

Katika Zaburi 110, zaburi ya kimasihi iliyoandikwa na Daudi (Mathayo 22:43), Melkizedeki ametolewa kama aina nyingine ya Kristo. Mada hii imerudiwa katika kitabu cha Waebrania, ambapo Melkizedeki na Kristo wote wamechukuliwa kuwa wafalme wa haki na amani.Kwa kudondoa Melkizedeki na ukuhani wake wa kipekee kama aina, mwandishi anaonyesha kwamba ukuhani mpya wa Kristo ni bora kuliko mpangilio wa zamani wa Walawi na ukuhani wa Haruni (Waebrania 7: 1-10).

Baadhi hupendekeza kwamba Melkizedeki alikuwa amepata mwili ulionekana kama Yesu Kristo, au Kristofani . Hii ni nadharia inayowezekana, ikikumbukwa kwamba Ibrahimu alikuwa amepata ziara kama hizo hapo awali. Chukulia Mwanzo 17 ambapo Ibrahimu alimwona na kuongea na Bwana (El Shaddai) katika umbo la mtu.

Waebrania 6:20 inasema, "alimoingia Yesu kwa ajili yetu, mtangulizi wetu, amekuwa kuhani mkuu hata milele kwa mfano wa Melkizedeki." Tamko kwa mfano kwa kawaida laweza kuonyesha urithi wa kuhani wanaoshikilia ofisi. Hakuna waliotajwa kamwe, hata hivyo, katika kipindi cha muda mrefu kutoka Melkizedeki hadi kwa Kristo, kioja kinachoweza kusuruhishwa kwa kuchukulia kwamba Melkizedeki na Kristo kweli ni mtu mmoja. Hivyo "mfano wa" umekabidhiwa ndani yake na kwake pekee milele.

Waebrania 7: 3 inasema kuwa ”hana baba, hana mama, hana wazazi, hana mwanzo wa siku zake, wala mwisho wa uhai wake, bali amefananishwa na Mwana wa Mungu; huyo adumu kuhani milele.”Swali ni iwapo mwandishi wa waebrania anamaanisha hii halisi au kitamathali.

Kama maelezo katika Waebrania ni halisi, basi ni vigumu kweli kuona jinsi itakavyotekelezwa kamili kwa mtu yeyote ila Bwana Yesu Kristo. Hakuna mfalme wa duniani "atakayebakia kuwa kuhani milele, "na hakuna binadamu wa kawaida“ ambaye hana baba wala mama.” Kama Mwanzo 14 inaelezea kuhusu imani ya kumufahamu Mungu, basi Mungu Mwana alikuja kumpa Ibrahimu baraka zake (Mwanzo 14: 17-19),akionekana kama Mfalme wa Haki (Ufunuo 19: 11,16), Mfalme wa Amani (Isaya 9: 6), na mpatanishi kati ya Mungu na binadamu (1 Timotheo 2: 5).

Kama maelezo ya Melkizedeki ni mfano, basi maelezo ya kutokuwa na nasaba/kisasi, hakuna mwanzo au mwisho, na huduma isiyo na mwisho ni tu kauli inayotia mkazo asili ya kiajabu ya mtu ambaye alikutana na Ibrahimu. Katika kesi hii, kimya katika maelezo ya Mwanzo kuhusu maelezo haya yana kusudi yanahudumu bora kwa kuunganisha Melkizedeki na Kristo.

Je, Melkizedeki na Yesu ni mtu mmoja? Kesi inaweza kufanywa kwa njia yoyote. Kwa uchache sana, Melkizedeki ni aina ya Kristo, anayeonyesha huduma ya Bwana kabla yake. Lakini pia inawezekana kwamba Ibrahimu, baada ya vita vyake vya kuchosha, alikutana na kumpa heshima Bwana Yesu mwenyewe.
 
zitto junior

zitto junior

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2013
Messages
10,626
Points
2,000
zitto junior

zitto junior

JF-Expert Member
Joined Oct 7, 2013
10,626 2,000
Nakupata vizuri,je hao wenzake ni kina nani ? Na kwanini aisiwe Yesu mwenyewe ndio mizani yenu ?
Of course Yesu ni mizania lakini hakuandika kitabu so katumia waandishi kadhaa kufikisha mafundisho yake mfano vitabu vya injili hivyo kma Kitabu hiki hakikinzani na Injili ama vitabu ya agano la kale basi hawawezi kukiacha nje ya Biblia kisa tu hawana uhakika na mwandishi Alieandika
 
Loeb S Mpalasinge

Loeb S Mpalasinge

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2013
Messages
1,160
Points
2,000
Loeb S Mpalasinge

Loeb S Mpalasinge

JF-Expert Member
Joined Dec 1, 2013
1,160 2,000
Wewe unasema Yesu sio kuhani na unasema Yesu ni nabii.Hapo naona kama umenirudisha katika upande ambao Siwezi kukubaliana na wewe kabisa.
Ukisikia mysterious figure kwenye biblia ambao hawakuwa na baba wala mama kuna Yesu Kristo,,Adam na Melkizedech.Lakini tumekabili kuujua ukweli wa Melkizedech ni nani hasa.?? Niliwahi kuandika Yesu kamwe hakuwahi kuwa nabii wala sio alichokijia na ndio Maana anaitwa Yesu Kristo.
Yesu alikuja akaondoka kama alivyo tabiliwa na manabii walio kuja kabla yake huyo kuhani mkuu sio yesu chamsingi bible kuna vitabu vingi havipo so kuna mambo mengi hatuyajui
 
Kunde Ekeke

Kunde Ekeke

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2018
Messages
5,718
Points
2,000
Kunde Ekeke

Kunde Ekeke

JF-Expert Member
Joined Feb 5, 2018
5,718 2,000
Wewe unasema Yesu sio kuhani na unasema Yesu ni nabii.Hapo naona kama umenirudisha katika upande ambao Siwezi kukubaliana na wewe kabisa.
Ukisikia mysterious figure kwenye biblia ambao hawakuwa na baba wala mama kuna Yesu Kristo,,Adam na Melkizedech.Lakini tumekabili kuujua ukweli wa Melkizedech ni nani hasa.?? Niliwahi kuandika Yesu kamwe hakuwahi kuwa nabii wala sio alichokijia na ndio Maana anaitwa Yesu Kristo.
Yesu Maelezo yake yana jitosheleza sio kuhàni mkuu yesu ni mwana maana yake ana baba mbinguni pia ana mama duniani ndio maana yesu ana sema tutaketi pamoja kwa baba yangu
 

Forum statistics

Threads 1,334,210
Members 511,914
Posts 32,469,663
Top