Melchizedek na utata unaomzunguka

Msingi wa hoja yangu ni kukataa kumsingizia roho mtakatifu kwamba wasioelewa jambo basi hawana huyo roho mtakatifu, huenda kuna wasioelewa kwa sababu "wanafalsafa" wamewachanganyachanganya kwa falsafa zao badala ya ukweli ulio wazi na ulio simple kabisa aliofundisha Yesu Kristo wa Nazareti
Okay basi naomba unisaidie Yesu anaposema ametumia mafumbo (Parables) ili "kuficha" alimaanisha nni?? Je ili uweze unlock hizo siri ufanyeje??

Huo mstari unasema Roho mtakatifu anafahamu kila kitu hivyo hata hizo parables cjui unabii, ndoto utaweza zitegua ukimshirikisha maana sio kila kitu kimeandikwa kwenye Biblia.

Hakuna mwanafalsafa anayepotosha, bali kwa mujibu wa Biblia Lucifer ndio anayepotosha Ufunuo 12:9,18:2 hivyo njia pekee ya kuepuka kudanganywa ni kupima hiyo Roho/fundisho kama limetoka kwa Mungu au shetani 1 Peter 4:1-8.

Ni hayo tu
 
Mungu wa kwenye Biblia huwaweza kujigeuza Binadamu anapopenda Kama alivyomtembelea IBRAHIMU
Soma
Mwanzo Sura ya 18 yote.
Jambo ambalo halijawahi kutokea kwenye Imani nyingine.
Kumbuka hii no kwa mujibu wa Biblia.
Ujajibu swali langu je kuna Mungu mmoja ambaye ndie Yesu au kuna zaidi ya mmoja
 
Melkizedeki
Anaonekana kuwa na sifa za Kimungu.
Mfano.
Kwanza tunaona IBRAHIMU anamtolea Fungu la kumi la Mapato yake na anabarikiwa naye.
Pili tunaona anaitwa majina Kama.
1. Asiye na Mwanzo Wala Mwisho Eb 7:3
2.Yaani Alfa na Omega
3.Yaani Niko Ambaye Niko

Haya Majina tunaona yametumiwa pia na Mungu mwenyewe wakati akijitambulisha kama
Baba- {Niko Ambaye Niko}
Mwana- {Alfa na Omega}
Kama Kuhani mkuu Melkizedeki
-{Asiye na Mwanzo Wala Mwisho}
 
Ujajibu swali langu je kuna Mungu mmoja ambaye ndie Yesu au kuna zaidi ya mmoja
Usihofu na Majina
Kwa mfano
Nasikia Mungu wa Waislamu ana Majina 99.
Je Mungu wa Waislamu wapo 99 ?

Turudi Kwetu.

Hapo zamani Za Musa, Mungu ambaye Yupo katika Asili Ya Roho Ambaye haonekani kwa Macho, wakati Mwingine alitaka amwoneshe Mtumishi wake Musa Uwepo wake kwamba yupo.
Sasa atajioneshaje ?
Akijitokeza Katika Utukufu wake Musa atakufa.
Kwani Binadamu hawezi kuhimili Utukufu wake.
Kwakuwa yeye ni Mungu ikabidi auoneshe Uwepo wake kwa Musa ili amwamini kuwa yupo.

Hivyo akaamua wakati Mwingine ajionesha kwa umbo la Moto unaowaka Kama kule mlimani Sinai alipompa Amri Kumi.
Sehemu nyingine alijionesha Kama Nguzo ya Wingu mchana na Nguzo ya Moto usiku, pale alipowaongoza Waisraeli kuihama nchi ya Misri.
Zama hizo alijiita kwa majina Kama.
+Niko Ambaye Niko
+Baba wa MILELE
+Mfalme wa Amani
Nk.
Sasa katika Zama za Agano Jipya, Mungu alikuja kuzungumza na watu wake, hivyo akaamua auvae mwili wa Binadamu (Kama alivyofanya katika Kitabu cha Mwanzo Sura ya 18 alipomtembekea IBRAHIMU kumweleza Kilio cha Sodoma na Gomora)
Katika Agano Jipya Mungu alishuka katika Mwili wa Binadamu aliyeitwa Yesu Kristo Muisraeli.
Na alijitambulisha kwa majina ya
+Alfa na Omega
+Mwanzo na Mwisho
+Neno
Nk.
Na alipouvaa Mwili wa Binadamu Yesu, Binadamu huyo alijitambulisha Kwetu kwa Jina la .
Mwana wa Mungu.

Kwa Zama hizi Mungu huyohuyo Mmoja anajitambulisha kwetu kwa Jina la
+Roho Mtakatifu.

NB.
Kama utamwangalia Mungu Kama Mungu utaelewa nilivyojaribu kukueleza.
Lakini Kama utamwona Mungu Kama Binadamu itabidi uendelee kujifunza tena.
Rudia tena kusoma taratibu ili upate kuelewa.

Kumbuka yale Majina 99.
Yote ni Ya Mungu mmoja.
 
haleluya ubarikiwe kwa kutaka kujua ukweli juu ya melkizedek mfalme wa wa Salem yaani mfalme wa amani
ujue tangu mwanzo MUNGU hajawahi kumuacha mwanadamu peke yake kwa ufupi melkizedek ndiye yesu mwenyewe kwa sababu biblia imeelezea mambo mengi kimafumbo hivyo inahitaji maarifa ya kimungu ili kuyaelewa vzuri (yohana mtakatifu 8:51-58 ) Wayahudi wakamwambia YESU ibrahimu amekufa na manabii wote wamekufa nawe wasema mtu akishika neno lako hataonja mauti wewe u mkuu kuliko baba yetu ibrahimu ambaye amekufa? na manabii waliokufa? wajifanya uu nani ibrahimu alishangilia kwa vile atakavyoiona siku yangu naye akaiona akafurahi Amin amin nawaambia yeye ibrahimu asijakuwako mimi niko) ibrahimu kama tunavyosoma alikutana na melkizedek akamtolea kikumi kama ulivyosema hapa ndipo alipofurahia siku ya yesu akampa moja ya kumi ya nyara zake ( melkizedek ni yesu)
 
Usihofu na Majina
Kwa mfano
Nasikia Mungu wa Waislamu ana Majina 99.
Je Mungu wa Waislamu wapo 99 ?

Turudi Kwetu.

Hapo zamani Za Musa, Mungu ambaye Yupo katika Asili Ya Roho Ambaye haonekani kwa Macho, wakati Mwingine alitaka amwoneshe Mtumishi wake Musa Uwepo wake kwamba yupo.
Sasa atajioneshaje ?
Akijitokeza Katika Utukufu wake Musa atakufa.
Kwani Binadamu hawezi kuhimili Utukufu wake.
Kwakuwa yeye ni Mungu ikabidi auoneshe Uwepo wake kwa Musa ili amwamini kuwa yupo.

Hivyo akaamua wakati Mwingine ajionesha kwa umbo la Moto unaowaka Kama kule mlimani Sinai alipompa Amri Kumi.
Sehemu nyingine alijionesha Kama Nguzo ya Wingu mchana na Nguzo ya Moto usiku, pale alipowaongoza Waisraeli kuihama nchi ya Misri.
Zama hizo alijiita kwa majina Kama.
+Niko Ambaye Niko
+Baba wa MILELE
+Mfalme wa Amani
Nk.
Sasa katika Zama za Agano Jipya, Mungu alikuja kuzungumza na watu wake, hivyo akaamua auvae mwili wa Binadamu (Kama alivyofanya katika Kitabu cha Mwanzo Sura ya 18 alipomtembekea IBRAHIMU kumweleza Kilio cha Sodoma na Gomora)
Katika Agano Jipya Mungu alishuka katika Mwili wa Binadamu aliyeitwa Yesu Kristo Muisraeli.
Na alijitambulisha kwa majina ya
+Alfa na Omega
+Mwanzo na Mwisho
+Neno
Nk.
Na alipouvaa Mwili wa Binadamu Yesu, Binadamu huyo alijitambulisha Kwetu kwa Jina la .
Mwana wa Mungu.

Kwa Zama hizi Mungu huyohuyo Mmoja anajitambulisha kwetu kwa Jina la
+Roho Mtakatifu.

NB.
Kama utamwangalia Mungu Kama Mungu utaelewa nilivyojaribu kukueleza.
Lakini Kama utamwona Mungu Kama Binadamu itabidi uendelee kujifunza tena.
Rudia tena kusoma taratibu ili upate kuelewa.

Kumbuka yale Majina 99.
Yote ni Ya Mungu mmoja.

Je YESU ndiye yule yule MUNGU BABA?
Na Je YESU ndiye huyohuyo ROHO MTAKATIFU?
 
Je YESU ndiye yule yule MUNGU BABA?
Na Je YESU ndiye huyohuyo ROHO MTAKATIFU?
Asante kwa kuuliza kwa busara Sana
Mimi hapo sitaki kusema sana.
Naomba nikupe Unabii wa Nabii Isaya kuhusu swali
hili
Nabii alitabiri hivi.

Isaya 9:6-7
" Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa,
Tumepewa mtoto mwanamume;
Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu,
Mungu mwenye nguvu,
Baba wa milele,
Mfalme wa amani.
Maongeo ya enzi yake na Amani
Hayatakuwa na Mwisho kamwe,
Katika kiti cha enzi cha Daudi na ufalme wake;
Kuuthibitisha na kuutegemeza
Kwa hukumu na haki,
Tangu sasa na hata milele.
Wivu wa BWANA wa majeshi ndio utakaotenda hayo. "

Hapo tunaona Nabii Isaya anavyo bashiri Kuzaliwa, Uweza, Sifa na Majukumu ya Mwanadamu Yesu atakaye zaliwa hapo baadae.

YESU KRISTO ni Mwanadamu Ambaye ndani yake kulikuwa na utimilifu kamili wa Mungu.
Kwakuwa Mungu ni ROHO hawezi kuonekana kwa Macho yetu.
Kumbuka siku ya kwanza Yesu kuruhusiwa kusoma andiko la Torati Sinagogini alisoma andiko linalomtambulisha katika Kitabu cha Isaya
linalosema
{(ROHO YA MUNGU i juu yangu)
amenituma ili niwafungue mataifa vifungo vyao.
Vipofu wapate kuona,
Viziwi wasikie
Viwete na watembee,
Habari njema itangazwe kwa mataifa yote}
Baadhi ya waumini na wazee wa Sinagogi walikasirika na kumburuta ili wakamtupe ktk bonde ikiwezekana afe kwakuwa alionekana ameyakufuru maandiko pale alipokiacha Kitabu na kuwaeleza kuwa andiko hili ndio limetimia kweke yeye. Yaani yeye ndiye Kristo Masihi.

Hivyo basi
MUNGU BABA hiyo ni moja ya Sifa ya Mungu ya uumbaji yaani yeye ndiye Mzazi wa viumbe vyote.
Kibaiolojia Mzazi ni Baba,
Ndiye mwenye Mbegu za Kike na Kiume.

ROHO MTAKATIFU Huo ni UWEPO wa Mungu.
Yaani Mungu ni
ROHO TAKATIFU
Sasa kwakuwa ROHO ya Mungu ni HAI na ndicho chanzo cha Uhai wa Kila kitu basi haiitwi tena ROHO TAKATIFU Bali
ROHO MTAKATIFU.
au ROHO YA MUNGU Kama anavyojitambulisha katika Kitabu cha
Mwanzo 1: 1
"Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi. Nayo nchi ulikuwa ukiwa, tena utupu, na Giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji;
Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji. "

{ NB}
Hayo maelezo ni jinsi nilivyoelewa Mimi. Tunasahihishana pia.
 
Asante kwa maelezo marefu lakini

JE YESU ndiye MUNGU BABA?
na JE YESU ndiye Roho Mtakatifu?
 
Ufafanuzi mzuri
Usihofu na Majina
Kwa mfano
Nasikia Mungu wa Waislamu ana Majina 99.
Je Mungu wa Waislamu wapo 99 ?

Turudi Kwetu.

Hapo zamani Za Musa, Mungu ambaye Yupo katika Asili Ya Roho Ambaye haonekani kwa Macho, wakati Mwingine alitaka amwoneshe Mtumishi wake Musa Uwepo wake kwamba yupo.
Sasa atajioneshaje ?
Akijitokeza Katika Utukufu wake Musa atakufa.
Kwani Binadamu hawezi kuhimili Utukufu wake.
Kwakuwa yeye ni Mungu ikabidi auoneshe Uwepo wake kwa Musa ili amwamini kuwa yupo.

Hivyo akaamua wakati Mwingine ajionesha kwa umbo la Moto unaowaka Kama kule mlimani Sinai alipompa Amri Kumi.
Sehemu nyingine alijionesha Kama Nguzo ya Wingu mchana na Nguzo ya Moto usiku, pale alipowaongoza Waisraeli kuihama nchi ya Misri.
Zama hizo alijiita kwa majina Kama.
+Niko Ambaye Niko
+Baba wa MILELE
+Mfalme wa Amani
Nk.
Sasa katika Zama za Agano Jipya, Mungu alikuja kuzungumza na watu wake, hivyo akaamua auvae mwili wa Binadamu (Kama alivyofanya katika Kitabu cha Mwanzo Sura ya 18 alipomtembekea IBRAHIMU kumweleza Kilio cha Sodoma na Gomora)
Katika Agano Jipya Mungu alishuka katika Mwili wa Binadamu aliyeitwa Yesu Kristo Muisraeli.
Na alijitambulisha kwa majina ya
+Alfa na Omega
+Mwanzo na Mwisho
+Neno
Nk.
Na alipouvaa Mwili wa Binadamu Yesu, Binadamu huyo alijitambulisha Kwetu kwa Jina la .
Mwana wa Mungu.

Kwa Zama hizi Mungu huyohuyo Mmoja anajitambulisha kwetu kwa Jina la
+Roho Mtakatifu.

NB.
Kama utamwangalia Mungu Kama Mungu utaelewa nilivyojaribu kukueleza.
Lakini Kama utamwona Mungu Kama Binadamu itabidi uendelee kujifunza tena.
Rudia tena kusoma taratibu ili upate kuelewa.

Kumbuka yale Majina 99.
Yote ni Ya Mungu mmoja.
 
Asante kwa maelezo marefu lakini

JE YESU ndiye MUNGU BABA?
na JE YESU ndiye Roho Mtakatifu?
Yesu ni Mwanadamu Kama wewe kwa kuwa wote mna Mwili wa nyama.
Ila yeye Yesu alikuwa na
Mungu Baba au
Roho Mtakatifu
ndani yake.
Kama yule Binadamu aliyemtembelea IBRAHIMU ktk Mwanzo 18.
Na IBRAHIMU akamtambua kuwa ni Mungu.

Mungu Baba au
Roho Mtakatifu
sio Binadamu.
Hana Mwili wa nyama kama Yesu, ila anaweza kujibadili ktk umbile lolote analotaka yeye.

Yeye ni Roho Takatifu.

Soma tena hapo Isaya 9:6

.
 
Kuhusu Yesu kuwa binadamu hilo nakubaliana na wewe mia kwa mia

Hata hivyo, Ibrahimu hakuwahi kumtambua Melkizedeki kama Mungu na ofcourse Melkizedeck siyo Mungu
Alimtambua kama Mtu, Kuhani wa Mungu na ndiyo maana akampa fungu la kumi, maana fungu la kumi hulipwa kwa makuhani/viongozi wa kiroho ili zikafanye kazi iliyokusudiwa kama vile kusaidia masikini etc
 
Habari za masiku wanajukwaa wote, leo ningependa tujadili watu mysterious kwenye vitabu vyetu vya dini kama ilivyo kawaida yetu. Hivyo twendeni pamoja ili tusolve mystery hii, kubwa ya yote tuongeze tu maarifa na kujibu maswali ambayo yameonekana magumu kwenye vitabu hivi.

Niweke rai mapema pamoja na kwamba inaongelea mtu wa kwenye imani zetu ila mada hii isijengwe kidini yaani kukashifiana bali ijikite kwenye mrengo wa kuelemishana. Karibuni

UTANGULIZI
Melchizidek anaongelewa kwa mara ya kwanza ndani ya Biblia kwenye kitabu cha mwanzo 14:18 ambapo baada ya Abraham kutokea vitani alikutana na Mfalme wa eneo la Salem (Jerusalem ya leo) ambapo alimbariki na Adam alimpa kikumi cha kila alichokuwa nacho wakati huo.

Kwahiyo kitabu cha mwanzo kinamueleza kama MFALME WA SALEM na kuhani wa Mungu YAHWEH

View attachment 1176929
AGANO JIPYA
Upande wa agano Jipya Melchizedek anaelezwa kuwa ana uhusiano ma Yesu.

Waebrania 5
6 kama asemavyo mahali pengine,Ndiwe kuhani milele Kwa mfano wa Melkizedeki

Zaburi 110:4, Waebrania 5:10,6:20 zote zinaeleza kuwa Yesu ni kuhani kwa mfuatano na huyu melchizedek. Ikumbukwe Makuhani wengi wamepita hapo kati na Yesu ametokea kwenye uzao wa Abraham sasa iweje afananishwe na melchizedek na sio kuhani yeyote yule??

Je huyu melchizedek ni nani hasa?

UTATA ZAIDI
Utata zaidi unaibuka pale ambapo muandishi wa kitabu cha waebrania (ambaye mpaka leo hafahamiki ni nani) anaandika haya
Waebrania 7
3 hana baba, hana mama, hana wazazi, hana mwanzo wa siku zake, wala mwisho wa uhai wake, bali amefananishwa na Mwana wa Mungu); huyo adumu kuhani milele.

Tunaambiwa huyu ''Jembe'' hakuwa na baba wala mama na anaishi milele hata sasa???

Ukisoma sura yote inamsifia mtu huyu wa ajabu (mysterious) na kusema licha ya ukuu wa Abraham kama Baba wa wayahudi ila haoni ndani kwa huyu Melchizedek!!

Book of Enoch
Muandishi wa kitabu hiki anajaribu kutupa mwanga kidogo kuhusu utata huu. Ukisoma Enoch 2 sura ya 71 inaeleza kuwa Kuhani Nir (Kaka yake Nuhu) alikuwa na mke ambaye hakulala naye toka alipoteuliwa na Mungu kuwa kuhani. Siku moja anagundua mke wake ana mimba, hivyo ukazuka ugomvi mkubwa mwishowe yule mama akapata presha akaanguka akafa, sasa cha ajabu walipotaka kuizika maiti haraka haraka ''kuua soo'' Wakashangaa mtoto ametoka tayari!!!. Yaani maiti imezaa!!!
Hivyo ikawa concluded kuwa kazaliwa bila baba wala mama.

Ikumbukwe alizaliwa kabla ya gharika, hivyo ili unabii utimie kuwa atakuwa kuhani wa makuhani wote ikabidi Malaika Gabriel amchukue na kumficha bustani ya Eden hivyo akapona gharika na akarudishwa baada ya gharika kupita.

HITIMISHO
Katika pekua pekua zangu sijakutana kabisa na maandiko yeyote kwenye biblia na pseudepigrapha (vilivyoachwa) ambacho kinagusia mwisho wake zaidi vyote vinasema anaishi milele ingawa havisemi wapi ama lini aliacha kuwa mfalme wa Salem.

Sasa wajuvi wa Historia na Dini mtusaidie je mtu huyu alikua nani hasa??

Pia kma alikuwa mkuu kuliko Abraham na amefananishwa na Yesu kwanini hajaongelewa sana kwenye Bible??

Je historia yake ni ipi??

Je mwisho wake ni upi hapa duniani? Au bado anaishi na sisi kwa sura tofauti?

Karibuni....
Ukimfuatilia kwa umakini mkubwa huyu Melchizedeck ni Mungu mwenyezi(baba). Huyu sasa ni mfalme na kwamba sii Prince(mwana).
Bwana Yesu yeye amefananishwa na mwana yaani katika huduma yake ya dhabihu ya damu yake mwenyewe amekuja na mwili wa damu na nyama. Ambao mwili huu una baba ambaye ni Mungu na mama ambaye ni Maria. Mwili huu wa damu na nyama una mwanzo na hivyo chenye mwanzo kina mwisho.
Mungu katika mwili ule wa Roho yani logos(theofania) ndio uliokutana na Abraham. Huu hauna mwanzo wala mwisho, wala hauwezi kufa. Mwili huu wa kiroho ndio uliojiumbia mwili wa nyama na damu katika tumbo la Maria kwa ajili ya kazi ya dhabihu ya damu na ndio njia Mungu aliyojipatanishia mwenyewe katika kukishinda kifo kilichoingia kwa uzao wa Adamu hapo mwanzo.
Sasa nafsi isiyo na mwanzo wala mwisho ya Mungu baba mwenyewe ndiyo iliyokuwa ndani ya ule mwili wenye kufa wa mwana Yesu.
Kazi ya ukuhani Mungu baba mwenyewe aliwahi kuifanya huko mwanzo katika wakati wa Adamu. Wakati adamu na Eva walipoanguka , Mungu aliwafunika utupu wao kwa ngozi ya mnyama. Sasa ngozi ilipatikana wapi wakati kulikua hamna mnyama aliyekuwa amekufa bado?Mungu alimchinja mnyama kondoo kwa kufunika dhambi ya kina Adamu.

Mbeleni katika hii historia utamwona Habili kwa ufunuo alitoa dhabihu ya damu na sadaka yake ikapata kibali tofauti na mboga mboga na matunda aliyotoa Kaini.
Agano la kale kabla ya Yesu lilikua ni kwa kafara ya damu za wanyama.
Kwa hiyo niseme Melchizzedeck ni Mungu mwenyezi katika hali ya ubaba kabla ya kuja duniani na mwili ambao ndio ulikuwa mwana.
 
1.Mkuu maandiko yanasema Yesu alikuwa.na Mama , lakini Melkizedeki hakuwa na mama sasa vip wawe sawa ?
2. Vilevile maandiko yanasema " amefananishwa na mwana wa Mungu ", lakini Yesu alikuwa mwana wa Mungu kamili , sasa vip wawe sawa ?

Rejea mstari wa 3:
mtatuua jamani
 
Yesu hakuwa na mama yeye mwenyewe alikataa alipoambiwa anatafutwa na wazazi wake
Iko Hivi
Kuna watu wanamwona Yesu Kristo katika umbo lake la nje la Kibinadamu.
Wanamwona hivyo katika macho yao ya nyama.
Hao kwao Yesu ni Binadamu Kama wao.
Na kwao, wao wako sahihi maana hawaoni zaidi ya hapo.

Kuna watu wanamwona Yesu Kristo kwa macho ya ndani ya Kiroho.
Uono huo unahitajia karama ya Kiroho.

Hao pamoja na mimi tunamwona Yesu Kristo kuwa ni Mungu kamili ambaye amekuja kwetu na kuzungumza nasi katika umbo bora kabisa la Kibinadamu.

Kama alivyozungumza na Nabii Musa katika umbo la Moto unaowaka.
Uono huu wa Kiroho tumeurithi kwa Babu yetu wa Imani IBRAHIMU.

Yeye ndiye mtu wa kwanza wa kujiwa na Binadamu na akamwona katika macho ya Kiroho kuwa ni Mungu Mwenyezi.

{Hebu Soma hapa.
Mwanzo 18:1

Bwana akamtokea Ibrahimu karibu na mialoni ya Mamre, alipokuwa ameketi mlangoni pa hema yake mchana wakati wa hari.
2 IBRAHIMU Akainua macho yake akaona, na tazama, WATU watatu wamesimama mbele yake. Naye alipowaona alipiga mbio kuwalaki kutoka mlangoni pa hema, akainama mpaka nchi}

Hapo juu tunamwona Baba wa Imani anamwona mtu mwenye Mwili Kama Yesu Kristo lakini anatambua kuwa huyo sio Binadamu Bali ni Mungu Mwenye enzi,

Uono huo ni wa Kiroho na wanaoutambua na kuutaka wanaupata.

Hii ndio maana wengine Wanasema Yesu ni Binadamu na sisi tunasema Yesu ni Mungu.

Ni Kama wale Majirani wa Nabii IBRAHIMU waliwaona watu wakimtembelea IBRAHIMU na hawakujua lolote zaidi ya hapo.

Ni Kama wale watu wa Sodoma na Gomora waliwaona wageni wa Lutu kuwa kama wanadamu vijana watanashati vile kwa macho yao ya nje.

Lakini Lutu mwenyewe aliwaona wale vijana kuwa ni Malaika halisi waliotumwa na Mungu Mwenye enzi.

NB
Sasa hapa nadhani mmefahamu kuwa watu wanaomwona Yesu Kristo Kama Mwanadamu ni watu wa aina gani.

Halikadharika
Watu wanaomwona Yesu Kristo Kama ni Mungu ni watu wa aina gani.

Hilo Ndilo Jibu
 
Similar Discussions

35 Reactions
Reply
Back
Top Bottom