Melchizedek na utata unaomzunguka

Ukiangalia sifa za huyo Melkisedeck jinsi zilivyotajwa ni Mungu pekee mwenyesifa sifa hizo. Zaidi aliwekwa hapo katika kitabu cha mwanzo kupokea sadaka ya Ibrahimu tena kabla ya uduma ya kikuhani kuanza (huduma ya kikuhani ilianza miaka ya baadaye kwa kutumia damu ya wanyama kwa utaratibu na mafundisho ya Mungu). Sasa hapa ilihitajika huduma ya kikuhani na hapakuwepo wa kuifanya, hivyo, ilimlazimu Yesu mwenyewe akaifanye kwa kujifunua kwa mfano wa Melikisedeck. Hivyo melikisedek alikuwa Yesu mwenyewe
Kwa ushahidi upi? Yesu ni uzao wa Abraham, (Mariamu ni uzao wa Abraham ila Wayahudi wanachukua uzao kwa baba, hii ndio moja ya sababu Wayahudi hawamtambui Yesu) sasa huyu alikuwepo kabla ya uzao rasmi wa Israil jambo ambalo linaenda kinyume na utabiri, au vipi ? Naomba elimu.
 
habari ndugu,

japo nimechelewa kusoma uzi huu naomba nikujibu kwa ninavoelewa. kabla sijaandika chochote naomba niwie radhi kama maelezo nitayoyaandika yalishatolea na mdau mwingine maana ndio niko page ya pili kati ya nyingi za hii page. huenda ushajibiwa.

muandishi wa waebrania ni nani na kwa nini hajulikani?

kama unavyojua waebrania/ hebrews ndio waisraeli wenyewe waliyemsulubisha Yesu. Hiyo ilikuwa clear sign kuwa hawamtaki hata kidogo na wanafunzi wake wengi walikua prosecuted. Imagine wewe ni mwebrania, je ungesign your name kwenye manuscript ambayo walengwa wanaweza kukupiga mawe mpaka ufe? exactly...

kumbuka hata kwenye bible Yesu alikuwa na wanafunzi wengi wa siri ikiwemo baadhi ya mafarisayo na kuhani kama kina nikodemo kama sijakosea. yeyote anaweza kuandika hiki kitabu.

Muandishi mwingine anayesadikika kuandika ni paul. kama unaijua historia ya huyu mwamba ni obvious asingeweza kuandika jina lake. Paulo alikuwa jasiri hakuogopa kuuawa ila wayahudi hawakumkubali hata kidogo. walimuona farisayo aliyeasi, kumbuka alijiita farisayo wa mafarisayo, myahudi wa wayahudi myahudi kweli. hii betrayal ingefanya kitabu kisiwe credible kwa wengi. Wengi walimjua kama muderer na some of them walimuexperiance kwa udhalimu mkubwa aliofanya hapo awali.

mwandishi mwingine inasemekana alikuwa ni mwanamke. kitabu kilichoandikwa na wanawake kisingebeba uzito mkubwa. Hata vile vya agano la kale kina ester havikuandikwa na wanawake ila na waandishi ambao walipenda historia za wanawake hawa zisipotee.


kuhusu kitabu chenyewe. ebwana ni kitabu kitamu sana jamaa yangu ukikisoma utaona mambo makuu sana ya Mungu yalioandikwa kwa undani kidogo kwani waliandikiwa kitabu hicho walikuwa wataalamu wa agano la kale. huandiki tu kizembe zembe ndio maana kulikuwa na references nyingi sana za matukio agano la zaman na jipya.

food for thought:

1) je wajua kuwa waebrania ndio kitabu pekee kilichoandikwa kwa ajili ya watu ambao tayari wanaijua agano la kale? vingine vyote vilikuwa ni kwa gentiles, na gentiles hawakuwa expected kuwa wamesoma torati na manabii. in other words unaweza kumuamini Yesu na kwenda mbinguni bila torati. just faith.

2) inasemekana kabla ya umri wa miaka saba watoto wakiebrania wote walikuwa wameshakariri torati yote.

3) makuhani wa agano la kale walikariri vitabu vyote vya sheria na manabii.

ahsante.
Aiseee hii post imetosheleza kuwa thread kabisa.

Long live JF
 
Mkuu kabla hatujatanua mada elewa hivi.
1. Yesu anaitwa mwana wa Mungu sio sababu alizaliwa kutoka viunoni kwa mtu bali sababu ana ROHO wa Mungu ndani yake same as sisi wanadamu tukiwa na ROHO wa Mungu basi tunaitwa wana wa Mungu Johana 1:12, 1 Petro 1:23.

2. Kwa muktadha huu inaua hoja huko juu kwamba ''Yesu ana Baba kama Sisi wanadamu ila melchizedek hana Baba''.

3.Hapa tuelewane kwanza then ndio tuje why Yesu anaitwa first born

4.Kiufupi tu Yesu ndio Kivuli/copy/Kioo cha Mungu hapa duniani kupitia hilo fungu so licha ya kwamba wote tutakuwa wana wa Mungu tukimpokea ila Yesu (Ambaye alishuka duniani kama mwanadamu) anakuwa Top ya wote maana ndio kuhani wetu kutupatanisha na Mungu. Hyo ndio distinguishing factor ila kama angekuwa tu Nabii kama Nabii mwingine basi angekuwa mwana wa Mungu tu ila sio FIRST BORN..... Hii ni kwa muktadha wa hilo fungu.

5. All in all inaonyesha superiority yake dhidi ya wote waliowahi kuishi duniani

Ni kweli lakin.kawa zama za kwetu ila zama ile alikua huyu melkizedeki
 
Sasa huyo Melkizedeki ni tofauti na Yesu maana maandiko yanasema kuwa pamoja na huyo Melkizedeki kuwa hapa duniani, hata hapahapa duniani kwenyewe hakuwa na mama, wakati kwa upande wa Yesu ni tofauti yeye alipokuwa hapa duniani, alikuwa na mama!

Halafu si maandiko yanasema Yesu ni mwana wa Mungu?, sasa vipi mnasema hana baba?

Melkizekedi yeye si mwana wa Yeyote maana maandiko yanasema hana baba wala mama
Hakuna mtu ambaye hajakutana na mbegu za kiume akawa mama ,mama ni hadhi anayopewa mwanamke ambaye gumbolake limetunza mbegu ya mwanaume tuu ikiwa ya jini au asie mwanaume huyo sio mama
 
Mada Nzuri sana.
Big up kwa wote mlioshiriki kikamilifu kabisa.
Mada kama hizi hazitakiwi kuchangiwa kwa mihemuko ya Kidini.
Nimechelewa kuiona hii mada na kutoa mchango wangu.
 
Safi Sana!

Kristulojia inakujakuwa maarifa muafaka humu JF...

Inaweza kuwa mapana ya somo na visomo bora kuliko yote humu JF.

Humu nimeona mengi na nimeona wengi ambao uwezo wao kuja kufanyika 'Walawi' wa siku za leo ni mkubwa.

Tutamulika kuhusu hili la Melkizedeki, Mungu Aliye Juu Kabisa, Miungu, Malaika, Uumbaji, na Viumbe watu --mahala fulani muafaka katika uzi wa 'Kusafiri Kiwakati 101...'

Kwa kuwa haya yote ya Melkizedeki ni mfano wa mengi yaliyo ni mafundisho yalivunjikavunjika katika biblia kuhusiana na Roho, nafsi na mwili...

Haleluya!
Kama Mkufunzi mose, ametia mguu katika hii mada.
Basi viwango vya hii mada vimekuwa vya juu sana.
Karibu sana mheshimiwa mose, katika michango ya mada zetu zile zenye mashiko.
Uwepo wako utatupatia maarifa mengi ya Hekima zako nyingi ulizojaliwa na Mungu Mwenye Enzi.
Nimefurahi sana kusikia kutoka kwako.
 
Maisha ya Wairani ni ya kikuani, maana kuna rais ambaye ni mtawala, alafu kuna Ayatolah ambaye kwao ni kama kuhani mkuu, uenda Salem ilikuwa Iran. Anyway dunia imeinama, mifumo imekengeuka, hakuna cha kuhani wala kuwadi, wote ni ubatili mtupu.
 
Yesu alipokufa alishuka kuzimu na Baadae akapaa mbinguni,,kule mbinguni aliipeleka damu yake kwenye madhabahu ya mbinguni.Alichofanya kilikuwa ukuhani.

Kwenye Revelation1:5-6 mstari wa sita unaongelea lengo lake la kuwafanya waamini kuwa Ufalme na makuhani...ila jambo hili kwa sasa likitimizwa kiroho...Safari nzima ya wana wa Israeli kutoka misri kwenda caanan ilikuwa imebebwa na dhumuni la wao kwenda caanan na kufanywa kuwa Ufalme na makuhani.Na utaona kabla hawajalilia mfalme walikuwa wakiongozwa na kuhani mkuu ambae alikuwa akipata mwongozo direct kutoka kwa Mungu.

Na hata walipokuja kuwa na mfalme kuhani mkuu alikuwa na nafasi kubwa sana kwenye maamuzi makubwa katika nchi.

Sasa Yesu amechukua nafasi ile ya ukuhani mkuu kwa maana anasimamia agano la damu yake ambalo ni jipya tofauti na lile la kutumia damu ya wanyama.

Mimi sidhani kama yeye melkzedech aliwahi kuwa mzao wa wanadamu ila tubakie na neno moja kwamba "he is mysterious person"

Labda kuelezwa kwake ni ili tujue kwamba Kuna watu wanaishi maisha ya kiroho katika ukweli halisi ulioonyeshwa kwa kuwakilisha/kuashiria au ulionyeshwa kwa ishara katika maisha walioishi wana wa Israeli pale caanan.

Kwa hio sasa nafasi alionayo melkizedech/Yesu haiko kwenye kuwakilisha tena au kuashiria ila ipo na ikitumika katika uhalisia wake na kanisa(watu wa imani kiroho) limechukua nafasi na hatma iliokusudiwa ya kuwa ufalme na makuhani.

Ukizingatia ishara zilizotokea wakati Yesu akiwa msalabani utaona kiza,,pazia la hekalu kupasuka/kuchanika.Maana ya pazia la hekalu kuchanika ilimaanisha kwa kupitia Yesu kuwa kuhani kila mmoja hapa duniani aliemwamini Yesu anaweza kufanya ibada na kuingia sehemu ya tatu ya hekalu ya kuhani mkuu kufanya ibada au kumkaribia Mungu kwa sadaka/dhabihu yoyote yenye kukubalika.

Mwisho kama kitabu cha waebrania haijulikani mwandishi wake inatosha kukidisqualify?
Mwandishi wa kitabu cha Waebrania ni Paulo
 
Mwanzo 14:18
Na Melkizedeki mfalme wa Salemu akaleta mkate na divai, naye alikuwa kuhani wa Mungu Aliye juu sana.

Zaburi 110:4
Bwana ameapa, Wala hataghairi, Ndiwe kuhani hata milele, Kwa mfano wa Melkizedeki.

Waebrania 5:6
kama asemavyo mahali pengine, Ndiwe kuhani wa milele Kwa mfano wa Melkizedeki.

Waebrania 5:10
kisha ametajwa na Mungu kuwa kuhani mkuu kwa mfano wa Melkizedeki.

Waebrania 6:20
alimoingia Yesu kwa ajili yetu, mtangulizi wetu, amekuwa kuhani mkuu hata milele kwa mfano wa Melkizedeki.

Waebrania 7:1
Kwa maana Melkizedeki huyo, mfalme wa Salemu, kuhani wa Mungu aliye juu, aliyekutana na Ibrahimu alipokuwa akirudi katika kuwapiga hao wafalme, akambariki;

Waebrania 7:10
kwa maana alikuwa katika viuno vya baba yake, hapo Melkizedeki alipokutana naye.

Waebrania 7:11
Basi, kama ukamilifu ulikuwapo kwa ukuhani wa Lawi; (maana watu wale waliipata sheria kwa huo); kulikuwa na haja gani tena ya kuhani mwingine ainuke, kwa mfano wa Melkizedeki, wala asihesabiwe kwa mfano wa Haruni?

Waebrania 7:15
Tena hayo tusemayo ni dhahiri sana zaidi, ikiwa ametokea kuhani mwingine mithili ya Melkizedeki;

Waebrania 7:17
maana ameshuhudiwa kwamba, Wewe u kuhani milele Kwa mfano wa Melkizedeki.
 
1.Mkuu maandiko yanasema Yesu alikuwa.na Mama , lakini Melkizedeki hakuwa na mama sasa vip wawe sawa ?
2. Vilevile maandiko yanasema " amefananishwa na mwana wa Mungu ", lakini Yesu alikuwa mwana wa Mungu kamili , sasa vip wawe sawa ?

Rejea mstari wa 3:
Uzao wa mwanamke YESU
Uzao wa nyoka shetani
Melichzedeck alifananishwa na mwana wa Mungu
Yesu Ni mwana wa Mungu
 
Habari za masiku wanajukwaa wote, leo ningependa tujadili watu mysterious kwenye vitabu vyetu vya dini kama ilivyo kawaida yetu. Hivyo twendeni pamoja ili tusolve mystery hii, kubwa ya yote tuongeze tu maarifa na kujibu maswali ambayo yameonekana magumu kwenye vitabu hivi.

Niweke rai mapema pamoja na kwamba inaongelea mtu wa kwenye imani zetu ila mada hii isijengwe kidini yaani kukashifiana bali ijikite kwenye mrengo wa kuelemishana. Karibuni

UTANGULIZI
Melchizidek anaongelewa kwa mara ya kwanza ndani ya Biblia kwenye kitabu cha mwanzo 14:18 ambapo baada ya Abraham kutokea vitani alikutana na Mfalme wa eneo la Salem (Jerusalem ya leo) ambapo alimbariki na Adam alimpa kikumi cha kila alichokuwa nacho wakati huo.

Kwahiyo kitabu cha mwanzo kinamueleza kama MFALME WA SALEM na kuhani wa Mungu YAHWEH

View attachment 1176929
AGANO JIPYA
Upande wa agano Jipya Melchizedek anaelezwa kuwa ana uhusiano ma Yesu.

Waebrania 5
6 kama asemavyo mahali pengine,Ndiwe kuhani milele Kwa mfano wa Melkizedeki

Zaburi 110:4, Waebrania 5:10,6:20 zote zinaeleza kuwa Yesu ni kuhani kwa mfuatano na huyu melchizedek. Ikumbukwe Makuhani wengi wamepita hapo kati na Yesu ametokea kwenye uzao wa Abraham sasa iweje afananishwe na melchizedek na sio kuhani yeyote yule??

Je huyu melchizedek ni nani hasa?

UTATA ZAIDI
Utata zaidi unaibuka pale ambapo muandishi wa kitabu cha waebrania (ambaye mpaka leo hafahamiki ni nani) anaandika haya
Waebrania 7
3 hana baba, hana mama, hana wazazi, hana mwanzo wa siku zake, wala mwisho wa uhai wake, bali amefananishwa na Mwana wa Mungu); huyo adumu kuhani milele.

Tunaambiwa huyu ''Jembe'' hakuwa na baba wala mama na anaishi milele hata sasa???

Ukisoma sura yote inamsifia mtu huyu wa ajabu (mysterious) na kusema licha ya ukuu wa Abraham kama Baba wa wayahudi ila haoni ndani kwa huyu Melchizedek!!

Book of Enoch
Muandishi wa kitabu hiki anajaribu kutupa mwanga kidogo kuhusu utata huu. Ukisoma Enoch 2 sura ya 71 inaeleza kuwa Kuhani Nir (Kaka yake Nuhu) alikuwa na mke ambaye hakulala naye toka alipoteuliwa na Mungu kuwa kuhani. Siku moja anagundua mke wake ana mimba, hivyo ukazuka ugomvi mkubwa mwishowe yule mama akapata presha akaanguka akafa, sasa cha ajabu walipotaka kuizika maiti haraka haraka ''kuua soo'' Wakashangaa mtoto ametoka tayari!!!. Yaani maiti imezaa!!!
Hivyo ikawa concluded kuwa kazaliwa bila baba wala mama.

Ikumbukwe alizaliwa kabla ya gharika, hivyo ili unabii utimie kuwa atakuwa kuhani wa makuhani wote ikabidi Malaika Gabriel amchukue na kumficha bustani ya Eden hivyo akapona gharika na akarudishwa baada ya gharika kupita.

HITIMISHO
Katika pekua pekua zangu sijakutana kabisa na maandiko yeyote kwenye biblia na pseudepigrapha (vilivyoachwa) ambacho kinagusia mwisho wake zaidi vyote vinasema anaishi milele ingawa havisemi wapi ama lini aliacha kuwa mfalme wa Salem.

Sasa wajuvi wa Historia na Dini mtusaidie je mtu huyu alikua nani hasa??

Pia kma alikuwa mkuu kuliko Abraham na amefananishwa na Yesu kwanini hajaongelewa sana kwenye Bible??

Je historia yake ni ipi??

Je mwisho wake ni upi hapa duniani? Au bado anaishi na sisi kwa sura tofauti?

Karibuni....
Melchizedek alikuwa malaika
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom