Mei Mosi, Sekta binafsi bado ipo gizani Totoro

Mei Mosi, Sekta binafsi bado ipo gizani Totoro

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
16,247
Reaction score
16,169
Wakati wenzao wa Sekta ya umma wakifurahi na kurukaruka kwa nyongeza ya mshahara wenzao wa Sekta binafsi hawajui la kufanya. Bidhaa zimepanda kwa watumishi wote na wote wanaishi kwenye mitaa ileile na kukua kwenye maduka yaleyale; wanachekana.

Bodi fanyeni hima kunusuru Sekta binafsi ambao ni watia huduma wazuri na walipa Kodi pia.
 
Hiyo sekta binafsi dawa yao ni kukosa wafanyakazi wa kuwaajiri. Watashika adabu na kutoa mshahara mkubwa kuliko wa serikali ili wakimbiliwe na waajiriwa
 
Shida sekta binafsi huwa hawasemi kuwa wanateseka.

Huwa wanasema sekta ya umma, mishahara kidhchu, wavivu, hawana KPIs na hawazalishi.

Sasa shida nini?
 
Sekta binafsi ukulipe mamillion umeufanyia nn kampuni?

Afu ukizingua wenzio wanaohitaji kazi wanachukuliwa, kule ni ushindani nje nje huko sio kwa bi kizimkazi
 
Hiyo sekta binafsi dawa yao ni kukosa wafanyakazi wa kuwaajiri. Watashika adabu na kutoa mshahara mkubwa kuliko wa serikali ili wakimbiliwe na waajiriwa
una nafasi za ajira kuwaajiri Watanzania wote wenye uhitaji wa ajira au umeropoka tu kwa kuwa wewe umejiriwa na serikali? uñafahamu hizo sector binafsi wanachopitia?
 
Sekta binafsi ukulipe mamillion umeufanyia nn kampuni?

Afu ukizingua wenzio wanaohitaji kazi wanachukuliwa, kule ni ushindani nje nje huko sio kwa bi kizimkazi
Lakini pia Sector binafsi wana matozo mengi ambayo huwezi kuyajua, kama hauna roho ngumu unafunga, Tanzania bado hakuna mazingira mazuri kwa sector binafsi, kama unafikiri uongo Weka kibanda cha mpesa hapo uone, TRA wanakuja, Manispa wanakuja, Brela wanakuja wote wanataka hela,
 
Kama ukilipwa chini ya laki 5 sector binafsi kuanzia july una haki ya kwenda mahakama ya kazi.

Wahindi inabidi waongeze mishahara.....walinzi waongezewe mishahara.
 
Dawa ni kujiajiri wakuu. Sema huku napo changamoto kibao makodi utitiri bidhaa hazina faida Tena si kama zamani.
 
Kwa uwingi wa watu waliopo haliwezekan tena, zamani ndio walikuwa wako tayari wakulipe pesa ndefu. Sahiz wana option nyingi
Serikali haina ajira na wameacha uholela Sekta binafsi. Haina mwenyewe, wanachotaka ni PAYE yao tu.
 
una nafasi za ajira kuwaajiri Watanzania wote wenye uhitaji wa ajira au umeropoka tu kwa kuwa wewe umejiriwa na serikali? uñafahamu hizo sector binafsi wanachopitia?
kwa hiyo ndio walipe mshahara kiduchu?
 
Back
Top Bottom