Mei Mosi 2018: Rais Magufuli atapandisha Mishahara miradi mikubwa ya Serikali ikikamilika, Mwaka jana alinukuliwa Vibaya

Jamani wajuvi wa mambo mniweke sawa,kuna manufaa gani yatapatikana kwa wafanyakazi endapo hii mifuko ya hifadhi itaunganishwa? Naona kauli mbiu inalipigia chapuo hili.
 
Mkuu hata mimi nashngaa, Rais anaongelea mambo ya uzinduzi wa miradi ya serikali kwenye sikukuu ya wafanyakzai, siku pekee kwa mwaka kwa wafanyakazi kutoa yao ya rohoni.
Watu kibao wanamshangaa huku, kila siku hotuba zake ni zile zile, badala atatue kero za wafanyakazi anaanza kujisifia mwenyewe
 
Mkuu, kama wewe ulibahatika na upo kwenye system basi usitubeze wenye njaa...isitoshe tupo wengi. Wanasema unaweza kuwadharau siafu lakini huwezi kuwakalia. Mimi nimezungumzia wafanyakazi kuminywa kutowasilisha kero/mabango yao na yasomeke, wewe unaninambia nikasomee jinsi Taasisi ya Rais inavyofanya kazi...then? hiyo taasisi ittanipa chakula? itaniongezea mshahara?

Nimejibu ' Hoja ' yako hasa juu ya kile ulichokiuliza na narudia tena kusema kwamba hicho ulichokiuliza hasa yale ' Mabango ' kupitishwa haraka kama ulivyosema ungekuwa angalau tu umepata hata a, b. c's za mambo ya ' Itifaki ' ya Rais wala usingepata nalo tabu hivi. Siku zingine usiwe unakimbilia kunijibu kwa hasira au kunikasirikia bali jaribu tu kuchukuwa na kujifunza yale ambayo kidogo nami najitahidi ' Kushea ' nawe kuhusiana na ' issues ' mbalimbali. Hayo ' Mafumbo ' yako ya Uswahili wako sijui ya Siafu mara nini hayanihusu sana ila ni imani yangu kuna kitu umejifunza juu ya niliyokuambia. Rais hajiongozi Yeye bali anongozwa na ' Itifaki ' ambayo inajumuisha mambo mengi sana ya msingi ikiwemo kuanzia Ratiba zake, Utaratibu mzima wa Siku na Tukio lililopo lakini kubwa suala zima la Usalama huwa linachukua nafasi kubwa sana. Naomba niishie hapa tafadhali.
 
Back
Top Bottom