MEDUSA: Shetani mwenye kichwa cha nyoka. Je, ni kweli damu yake ilitumika kufufua wafu?

Da Vinci XV

JF-Expert Member
Dec 7, 2019
3,837
6,372
Wasalaam

Binafsi wakati nakuwa nlipoanza kusikia myth za mataifa mbalimbali asa asa nchi za Latini ,misri,Babeli, na Ugiriki nikatamani sana kuelewa na kufahamu kuhusu tawala zao na miungu yao ya kale nikaanza kujifunza na kusoma kuwahusu
katika mengi niliyojifunza ,kidogo nikaona si haba kuwamegea wengineo kisa hichi ambacho ni maarufu na wengi wetu tunakifahamu, kisa cha MEDUSA

Medusa
alikuwa mmoja miongoni mwa gorgons (viumbe mashetani) watatu,viumbe hawa watatu walikuwa ni mabinti wa Phorcys na Ceto, dada zake Medusa walikuwa ni Graeae, Echidna, na Ladon Hawa wote ni viumbe wa kutisha kweli na wa Ajabu (gorgons)

Screenshot_20210204-123322.png


Medusa huyu alikuwa mrembo haswa Alibadilishwa kuwa monster mkali na mwenye nyoka wakali kwenye nywele zake Medusa aliuawa na Perseus kwa kukatwa kichwa chake, ambaye baadaye alitumia kichwa chake bado kama silaha, kabla ya kumpa Athena.

Screenshot_20210204-005526.png


FAMILIA YAKE

Medusa
,ambaye jina lake inaelezwa linatokana na neno la Kiyunani la Kale lenye maana ya "mlezi" ,alikuwa mmoja wa mashetani watatu, mabinti wa miungu ya baharini Phorcys na Ceto, na dada zake Medusa ni Graeae, Echidna, na Ladon. Ndugu wote wa Medusa walikuwa Monsters wa kuzaliwa , ingawa medusa hakuwa hivyo kabla, alikuja kuwa na bahati mbaya ya kugeuzwa kuwa hivyo na kufanya ukatili zaidi ya dada zake wote na kuwa mbaya zaidi ya wote

MEDUSA

Medusa alielezewa kwa namna ifuatayo kwamba alikuwa na mikono ya shaba na mabawa ya dhahabu. Washairi wengi walidai kwamba alikuwa na meno makubwa kama ya nguruwe na ulimi ukiwa umetokeza kati ya meno yake yanayotisha Nyoka wakali walikuwa juu ya kichwa chake badala ya nywele.

Uso wake ulikuwa wa kutisha sana na macho yake yalikuwa yakichoma sana hivi kwamba kumwona tu kulitosha kumgeuza mwanaume kuwa jiwe

Screenshot_20210204-005646.png


Ulikuwa ukimtazamana naye mwanaume basi papo hapo utageuka kuwa jiwe na kuganda nadhani hii wengi wetu wanaijua

POSEIDON na PERSEYUS

Medusa
ilijulikana kuwa kutoka kwao ukweli kwamba yeye peke yake alizaliwa akiwa na uso mzuri tofauti na dada zake.

Screenshot_20210204-005610.png


ikafikia mpaka Ovid mshairi mashuhuri kutoka roma Italy alimsifu sana utukufu wake na hata kuwa na nywele nzuri ambazo baadae zilikuja kubadilishwa

Ovid alimsifu Medusa kwa kusema katika moja ya mashahiri yake

"mzuri zaidi ya haiba zake zote."

Katika miungu hiyo mungu mkubwa wa bahari Poseidon anaonekana katika historia kudhihirisha simulizi za urembo wa medusa ,,,,,kwani mara moja hakuweza kusita kumjaribu na kumpa ujauzito Medusa katika hekalu la Athena.

Athena
Alikasirika sana kwa kitendo hicho, Huyu Athena alikuwa mungu wa kike aliye bikira na yeye ndiye aliyebadilisha nywele zake nzuri za Medusa kuwa Uchawi wa vichwa vya nyoka, akimgeuza binti huyo mdogo na mrembo kuwa monster...wa hatari aliyeyeteresha milki nyingi

Screenshot_20210204-123426.png

ATHENA

Polydectes, mfalme wa Seriphos, alimtuma shujaa Perseus huyo kwenye harakati ambayo aliamini lazima iwe ya mwisho kwa ajili ya kumtokomeza Medusa baada ya kusumbua sana

"Nileteeni kichwa cha Medusa,"

aliamuru Polydectes.

Na kwa msaada wa Athena na Hermes, na baada ya kumlazimisha na kumhadaa dada yake Medusa aitwaye Graeae aweze kuonyesha mahali alipo Medusa, hatimaye Perseus alifikia ardhi ya Gorgons, iliyoko magharibi kabisa,kwenye kisiwa cha miamba ya Sarpedon.

Perseus alifanikiwa kulala na Medusa,
Akitumia ngao ya shaba aliyopata kwa Athena kama mwongozo
(ili asitazame moja kwa moja Gorgons walio katika kichwa cha Medusa na kugeuzwa jiwe)

Aliweza kukata kichwa chake kwa panga Lake.

Screenshot_20210204-123626.png


Hatima ya baada ya kufa ya Medusa

Cha kushangaza ni kwamba, hadithi ya Medusa haiishii kwenye kifo chake tu
Screenshot_20210204-110237.png


WATOTO WA MEDUSA

Inaelezwa Medusa alikuwa mjamzito wakati wa kifo chake, na wakati Perseus alipokata kichwa chake, watoto wake wawili ambao walikuwa hawajazaliwa, Chrysaor na Pegasus, walitoka ghafla mwilini mwake.

Na walijitahidi kulipiza kisasi kifo cha Medusa wakishirikiana na Dada zake Medusa.., lakini hawakuweza kuona wala kumkamata Perseus, kwani inaelezwa alikuwa amevaa Kofia ya Kuzimu ya Kutoonekana na viatu vya mabawa vya Hermes. Kwa hivyo, waliendelea kuomboleza kifo Medusa.

Pindar, mshairi mkubwa wa Kale wa Uigiriki, anasema kwamba Athena yule mungu mwanamke aliposikia kilio chao cha kusikitisha, Athena aliguswa sana mpaka akaiga nyimbo hizo za maombelezo

Screenshot_20210204-123233.png


MIUJIZA YA MEDUSA NA KICHWA CHAKE

Sasa kwa kuwa Perseus alikuwa na kichwa cha Medusa kwenye mkoba wake, alirudi Seriphos. Walakini, wakati wa kupita eneo ambapo ipo Libya ya sasa, matone ya damu ya kichwa cha Medusa yalidondoka chini na mara kila tone moja likageuka kuwa nyoka; na wengine wamepata kusema ndiyo sababu ya kwamba, hadi leo, Libya imejaa nyoka.

Wakati Perseus alipofika Seriphos, alitumia kichwa cha Medusa kugeuza wabaya wake kuwa mawe;
Kisiwa hicho kilijulikana sana kwa muda mrefu kwa kuwa na mawe mengi ambayo Persus alitumia kuwabadili watu kuwa mawe

Baada ya hayo, Perseus alitoa kichwa cha Medusa kwa mfadhili wake Athena, kama zawadi...Athena huyu Mungu wa kike, Alikusanya pia damu iliyobaki na akampa Asclepius, ambaye alitumia damu kutoka upande wa kushoto wa Medusa kuchukua uhai wa watu na damu kutoka upande wake wa kulia wa Medusa, kufufua wafu.

Screenshot_20210204-123303.png


YAPO MAAJABU MENGI KUHUSU HADITHI ZA HUYU MEDUSA

LAKINI JE NI YA KWELI YANAYOZUNGUMZIWA IKIWEMO KUFUFUA WAFU

Vyanzo

Unaweza kusoma muhtasari , angalia mwisho wa kitabu cha nne cha "Metamorphoses" ya mshahiri Ovid. Kwa kawaida, nasaba ya Medusa imeelezewa kamili katika "Theogony" ya Hesiod.

Tazama pia: Perseus, Adventures ya Perseus, Pegasus, Gorgons, Phorcys, Keto

aVinci XV
 
Ile movie huwa inaanza kwa maelezo yafuatayo.

NARRATOR: the oldest stories ever told

Are written in the stars

Stories of time before man and gods.

When Titans ruled the earth.

The Titans were powerful...

But their reign was ended by their own sons

Zeus,Poseidon and Hades....

....to create a beast so strong
It could defeat their parents.

And from his own flesh. Hades gave birth to an unspeakable horror.
.....the kraken.

Zeus became king of the heavens.

Poseidon, king of the seas.

And Hades, tricked by Zeus....

....was left to rule underworld in darkness and in misery.

It was Zeus who created man....

....And man's prayers fed the god's immortality.

But in time,mankind grew restless.

They began to question the gods...

....and,finally rise up against them.

Into this world, a child was born(Perseus)

A boy who could change everything.

Bonge LA movie balaa
 
Ile movie huwa inaanza kwa maelezo yafuatayo.

NARRATOR: the oldest stories ever told

Are written in the stars

Stories of time before man and gods.

When Titans ruled the earth.

The Titans were powerful...

But their reign was ended by their own sons

Zeus,Poseidon and Hades....

....to create a beast so strong
It could defeat their parents.

And from his own flesh. Hades gave birth to an unspeakable horror.
.....the kraken.

Zeus became king of the heavens.

Poseidon, king of the seas.

And Hades, tricked by Zeus....

....was left to rule underworld in darkness and in misery.

It was Zeus who created man....

....And man's prayers fed the god's immortality.

But in time,mankind grew restless.

They began to question the gods...

....and,finally rise up against them.

Into this world, a child was born(Perseus)

A boy who could change everything.

Bonge LA movie balaa
Clash of the titans
 
Ile movie huwa inaanza kwa maelezo yafuatayo.

NARRATOR: the oldest stories ever told

Are written in the stars

Stories of time before man and gods.

When Titans ruled the earth.

The Titans were powerful...

But their reign was ended by their own sons

Zeus,Poseidon and Hades....

....to create a beast so strong
It could defeat their parents.

And from his own flesh. Hades gave birth to an unspeakable horror.
.....the kraken.

Zeus became king of the heavens.

Poseidon, king of the seas.

And Hades, tricked by Zeus....

....was left to rule underworld in darkness and in misery.

It was Zeus who created man....

....And man's prayers fed the god's immortality.

But in time,mankind grew restless.

They began to question the gods...

....and,finally rise up against them.

Into this world, a child was born(Perseus)

A boy who could change everything.

Bonge LA movie balaa
aisee
 
Back
Top Bottom