Media, Tumedhalilishwa!, Tumejidhalilisha!. Ni Matokeo ya Sheria Mbovu, Umasikini, Dawa ni Kuunganisha Habari na UtangazajI, Tulipwe Fungu Nene!.

Wanabodi,

Japo dunia nzima inafahamika nchi kuendeshwa kwa mihilimili mitatu ya The Executives, The Legislature and The Judiciary, si wengi wanaotambua kuwa kuna mhilimili wa nne, The Media. Media ni mhimili, "The Forth Protocol, or The Forth Estate", waandishi wa habari ni mhimili, wanapaswa waheshimiwe, walipwe vizuri kama mihilimili mingine, wasidhauliwe na kutupiwa pesa kama mbwa, na kutokana na njaa, wakazigombea na kujidhalilisha,

Kumetokea tukio la udhalilishaji kwa waandishi wa habari kutupiwa pesa kama mbwa, na wao kuzigombania, kuzichana baadhi, kuharibu vifaa vyao vya kazi na kuonyesha picha mbaya kuwa waandishi wa habari wa Tanzania, ni watu wa hovyo kihivyo na ni watu wenye njaa ya ajabu hadi kuparurana kugombea noti zilizirushwa kwa mtindo wa sadakalawe.

Kabla sijaripoti kilichotokea, naomba kutoa utambulisho wangu mfupi ili haya nitakayo yasema, yatoke kwa mtu ambae ni authority of some sort.

Mimi Pascal Mayalla nilianza kazi ya uandishi Tarehe 02, January, 1990, pale Idara ya Habari Maelezo, wakati huo hapa nchini vyombo vya habari vilikuwa 8 tuu, Magazeti miwili ya Daily News/Sunday News na Uhuru Mzalendo. Gazeti moja la weekly Mfanyakazi. Redio moja ya Taifa, RTD, Redio moja ya dini kule Moshi, Sauti ya Injili, na mashirika miwili ya habari Shihata na Idara ya Habari Maelezo. Tulikuwa na sheria moja ya Habari, The Newspapers Act of 1976. Hatukuwa na sheria ya utangazaji, bali mambo ya habari yalikuwa chini ya Wizara moja ya Habari na Utangazaji. Wakati huo Tanzania tuna vyuo viwili tuu vya habari, TSJ cha Dar na Nyegezi cha Mwanza, hivyo waandishi wote wakongwe, ama wamepitia TSJ ama Nyegezi. Wakati huo ukimaliza tuu chou, unapangiwa ajira direct.

Mimi baada ya kumaliza form six, nilipania kujiunga na chou kikuu cha DSM kusomea sheria, Bahati mbaya baada ya kukosa DV 1 ya form six, huwezi kusoma sheria, hivyo nika opt kusomea uandishi TSJ. Kutoka TSJ nikatua Maelezo, kisha Daily News na kuishia RTD. Tangu hiyo 1990 mpaka leo 2019 ni miaka 29!, hivyo mimi ni authority kwa experience, ya News Agency, Print na Electronics, maoni yangu ni from experienced journalist.

Tulipoleta sheria mbili mpya za habari, mimi kama mwandishi mzoefu nilitoa maoni yangu, both kwa Vipindi vya TV, kuandika kwenye mitandao ya kijamii, na kutoa maoni yangu kwa maandishi kama mdau wa habari.
Nikasema sheria hii mpya ya habari, ni ile ile sheria ya Magazeti ya mwaka 1976, haiwezi kutusaidia sana katika dunia hii ya utandawazi.

Hiwezekani sekta moja ya habari, yenye vyombo vya habari vya aina tatu, vikaratibiwa na sheria tatu tofauti chini ya wizara mbili tofauti na tukabaki salama.

Sheria ya Habari iko chini chini ya Wizara ya Habari na inaratibu vyombo vya habari vya magazeti, yaani print chini ya Idara ya habari Maelezo. Vtombo vya Utangazaji viko chini ya sheria ya utangazaji inayoratibiwa na TCRA, chini ya wizara ya mawasiliao. Online media inaratibiwa na TCRA chini ya Sheria ya mtandao.
Zamani gazeti ni gazeti tuu kazi yake ni kutoa print out tuu, leo gazeti linafanya utangazaji na kuweka online, huwezi kuwaratibu hawa wote watatu kwa sheria tatu tofauti, mamlaka tofoati chini ya wizara tofauti na mambo yakawa shwari tuu, lazima kutatokea mikanganyika, na mimi katika maoni yangu kwa maandishi nilisema wazi hapa kuna mkanganyiko, hatutaouna mpaka matatizo yaanze kujitokeza ndipo tutafungua macho kuangazia na kuondoa mikanganyiko hii.
Sasa soma hiki kisa kilichotokea jana

Tukio hilo humu limeripotiwa na mwana jf huyu

Mkuu Mkongwe Mzoefu, kwanza asante kutuletea clip hii, hivyo mimi kama mwandishi wa habari, mkwongwe na mzoefu nina haya ya kusema.

  1. Kwanza ni kweli na kiukweli kabisa, waandishi hao habari, wamedhalilishwa kutupiwa fedha kama mbwa, Irene Uwoya amewadhailisha waandishi kuwatunza kwa kuwatupia fedha kama mbwa wanavyotupiwa nyama. Japo Irene Uwoya alifanya kitendo kile cha tunza kwa nia njema, tunza za waandishi zinafanywa kwa heshima maalum ikiwemo kuwawekea hizo tunza kwenye bahasha za khaki na waandishi kukabidhiwa kwa majina na waandishi kusaini. Irene Uwoya ni kiazi, she is imbecile, huwezi kuwatunza kuwatunza watu mtindo wa kuwatunza wasanii on the stage au zile tunza za kitchen party, alifanya vile kutafuta kiki. NB. Nasisitiza Bahasha za waandishi sio rushwa.https://www.jamiiforums.com/threads/waandishi-wa-habari-na-bahasha-sio-kila-bahasha-ni-rushwa-pasco-wa-jf.215720/#js-post-3196765
  2. Waandishi waiokuwepo kwenye tukio hilo pia wamejidhalilisha na kutudhalilisha sisi waandishi wengine wote kuonekana waandishi ndio tuko hivyo kitu ambacho sii kweli. Waandishi wa ukweli tuliopitia mafunzo hatuko hivyo. Kwenye kundi lile naamini kulikuwa na waandishi wa ukweli ambao wao hawakugombea lakini kwa vile lilikuwa zogo, wote wakaonekana waligombea, kwa mtindo wa samaki mmoja akioza, samaki wote wameoza. Haiwezekani mpiga picha mwenye camera ya million 20, agombee elfu 10,000 na kurisk kuharibu kifaa chake cha million 20!.
  3. Kwa jicho la haraka, wengi wa waandishi waiokuwepo pale ni waandishi wa michezo na burudani wakiwemo wale wa online media na ma bloggers. Hawa ni waandishi in a sense ya kuhabarisha jamii kupitia online platforms mbalimbali kama online TVs, blogs, forums, fb, insta, twitter etc. Hawa wanakuwa licenced na TCRA.
  4. Tukio hili ni blessing in disguise kuonyesha jinsi sheria mpya ya habari inavyotuetea majanga. Kwa mujibu wa sheria, waandishi wa habari wanasajiliwa na Idara ya Habari Maelezo na kupewa Press Cards baada ya kukidhi sifa na vigezo ikiwemo kuwasilisha vyeti vya kitaaluma. Idara hii ya Habari Maelezo iko chini ya Wizara ya Habari, hivyo wanaopata Press Cards za Idara ya Habari Maelezo ni waandishi kweli wenye sifa vigezo na weledi, hawawezi kugombea pesa kama mbwa.
  5. Wakati Maelezo chini ya Wizara ya Habari wanasajili waandishi wa habari wa ukweli wenye taaluma sifa na vigezo, Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA, chini ya Wizara ya mawasliano, wao wanasajili ma bloggers na online TV, sifa ya kusajiliwa ni kulipia ada ya usajili ya TZS 1,000,000. Baada ya kulipia ada hiyo, majina yao yanapelekwa Maelezo kuwa issued na Press Cards za Maelezo, hivyo tukikutana kwenye news events wote tunaonekana sawa ni waandishi wa habari wenye Press Cards, mmoja kasomea uandishi kama taaluma, mwengine katokea mtaani hana a wala b kuhusu fani ya habari, matokeo ndio haya sasa ya waandishi kutupiwa fedha kama mbwa na wao kugombea kisha wote kuonekana the same!.
  6. A way Forward. 1. Idara ya Habari isikubali kuletewa makorokocho ya TCRA na kuwapa Press Cards kama za waandishi. Maelezo watenganishe Press Cards kati ya waandishi wa habari wa ukweli waliosomea na hawa ma bloggers na online media ili ikitokea tukio la udhalilishaji wa mwandishi tujue ni mwandishi mweledi wa newsroom au wale wa mitaani wa TCRA. Kinachofanywa na Maelezo kwa sasa ni sawa na madakitari medical doctors kupewa same licenses sawa na waganga wa kienyeji, maana wote wanatibu, mmoja kasomea, mwengine anatumia maruhani and they are the same.
  7. Way Forward 2: Baraza la Idhibati kwa Waandishi wa Habari lianzishwe ili kutuondolea aibu hii na udhalilishwaji huu. Waandishi wajulikane ni waandishi kweli kama ilivyo kwa wanasheria, madakitari na ma engineer, kuwa wakili mtu lazima ahitimu LL.B, chini ya hapo ni paralegal, ili uwe daktari, lazima uhitimu MD, etc, sasa tufike mahali ili kuwa a licensed na accredited journalist lazima uwe na kiwango fulani cha elimu. Wale wasio kidhi vigezo nao watakuwa na utambulisho wao kama ni technical people ma cameraman, ma bloggers, waandishi wa mtaani wa online TV etc.
  8. A Way Forward 3: Turekebishe sheria kuunganisha habari na mawasiloano ambapo mambo yote media yawe chini ya sheria moja. Kwa sasa vyombo vya habari vya print media vinaratibiwa na kudhibitiwa na sheria ya habari chini Wizara ya Habari, na vyombo vyote vya utangazaji vinaratibiwa na sheria ya Utangazaji iko chini ya TCRA, iliyoko chini ya Wizara ya Mawasiliano
  9. A Way Forward 4: Media ni mhimili, waandishi wa habari ni watendakazi wa mhili huu wa nne, nao wanastahili kulipwa malipo mazuri kama kama watu wa mihimili mingine, kama mtu hana uwezo wa kuanzisha media na kuwalipa vuzuri waandishi, basi bora asianzishe, accredited media ziwe na waandishi wasomi, weledi, wanaolipwa vizuri, kama mbwa wa polisi au umbwa wa wazungu, analishwa vizuri na atakula chakula tuu kile alichowekewa na mlishaji wake wa kila siku, siku akitupiwa nyama yanye sumu, hali hata awe na njaa vipi, hivyo ndivyo inavyotakiwa kwa accredited media, waandishi walipwe vizuri, media ziwe na usafiri wake, waandishi wa accredited media hawahitaji bahasha ya yeyote kwa ajili ya lunch kwa sababu hawana njaa, wala kwa ajili ya usafiri kwa sababu wana unafiri wao, hivyo mtu kichaa kama yule, akiwatupia pesa kama alivyofanya jana, waandishi hao watamwangalia tuu, na pesa zake zitaishia kupeperuka, na kama ni kuokotwa, ziokotwe na wale makanjanja na waandishi wa mitaani wa social media na sio kwa accredited journalists.
  10. Mwsho sisi waandishi wenyewe, tujiheshimu, tuheshimiwe. Ningekuwa ni uwezo wangu, ningewaomba waandishi wote waige mfano wangu, mimi Pascal Mayalla, nikiitwa press conference yoyote, sipokei bahasha yoyote ya mtu yoyote, na hata kwenye events zenye lunch or dinner, mimi na team yangu huwa hatuli lunch ya yeyote wala dinner ya yoyote, hivyo kuendelea kuwa independent, ikiitwa popote, nauliza swali lolote kwa yeyote kwa sababu siwategemei wowote wala yeyote, sipokei bahasha yoyote hivyo kuendelea kuwa an independent journalist.

Paskali
Rejea za Nguli Pasco Kuhusu Tasnia ya Habari.

Mkuu sijakuelewa vizuri.ila kama mlidhalilishwa na Irene Uwoya ishu za sheria zitawabeba vipi? Maana hata kama ishu za sheria zikikaa vizuri inaonekana kama mtadhalilishwa tu.Bora angekuwa amewatupia pesa Zuberi (Zuberi Bus services Tajiri wa mza)
 
Yani ww mayalla huna tofati na msiba ni sawa na mbwa aliyepandishwa juu ya mti,nyinyi wandishi ni malofa na wenye elimu ndogo sana kwanza wengi wenu ni form four F.
 
Wiiivu unakusumbua baada ya MTATIRO kupata uteuzi.

Sasa mtatiro atakuwa anapata pesa nene!!!

Pambana yuneva no unaweza kuteliwa kuandika ilani ya uchaguzi Pascal Mayalla
 
Pascal Mayalla kudhalilishwa kule mnayataka wenyewe
Mzungu anasema 'show me your friends and I will tell who you are!'
Tasnia ya habari ni jalala wengi wanafanya kazi kwa mazoea elimu ya idara hiyo hawana ustaarabu hekima busara wengi hawana
Mnaacha kuandika mambo muhimu yanayohusu Taifa mnahangaika na hawa wazinzi matokeo yake ni haya. Wamewajua shida yenu ni pesa umaskini na umaarufu uchwara unawasumbua
Wasanii wa bongo ni watu wa ovyo sana nanyi mnaungana nao.

Maadili na wajibu wa kazi kwa baadhi ya wengi katika tasnia ya habari hamna kitu
Jipangeni upya la sivyo haya yataendelea kutokea
 
Wanabodi,
Mimi baada ya kumaliza form six, nilipania kujiunga na chou kikuu cha DSM kusomea sheria, Bahati mbaya baada ya kukosa DV 1 ya form six, huwezi kusoma sheria, hivyo nika opt kusomea uandishi TSJ. Kutoka TSJ nikatua Maelezo, kisha Daily News na kuishia RTD. Tangu hiyo 1990 mpaka leo 2019 ni miaka 29!, hivyo mimi ni authority kwa experience, ya News Agency, Print na Electronics, maoni yangu ni from experienced journalist.
Pascal Mayalla wewe mbona umeruka sehemu moja uliyopitia? Wewe si ulipitia JWTZ, tena Ukonga ukapiga depo mpaka ukamaliza na kuwa askari kamili?
 
Hi dunia ngumu Sana Tena yenye maajabu mengi imagine:

1. Hapo n wanaabari waandishi wenye weledi wa kutumia kalamu yao vizuri alafu tunawaona wanagombania sh 10,000/= Tena zinazorushwa huku wao wakizigombania hii inaleta picha unaeza ita waandishi wa habari ukawapa pesa na ukawaambia wakaandike kile kisichofaa na kuja kuharibu taifa maana MWANDISHI YAKE KALAMU ASIPOOTUMIA KWA WELEDI ULIINGIZA TAIFA KWENYE MACHAFUKO ndo Mana hatuon habari za kujenga jamii na uchumi Kama makala za ubunifu, kilimo huwez kuta front page Zaid ya habari zenye maslai ya watu wachache au kikundi kidogo WAANDISHI WA HABARI MMEJIZALILISHA MNO MBAYA ZAID KAMERA ZENU WENYEWE NDO ZIMEWAUMBUA

2. Hawa wacheza nusu uchi sijui waigizaji saa zingine mtafute watu wenye weledi na Mambo ya public wamasaidie kuwaongoza mkumbuke nyie ndohuwa wakwanza kuomba mchangiwe matibabu sijui msiba hamkumbuki mnajianika kwenye lininga mnajisahau mnajileta kwenye maisha halisi ilihali mkijua kuwa mnafake maisha kwann msiwe real uzur nimekaa nanyie sinza ile wakati sinza sio sinza ya Sasa hvyo nawajua mno badiliken mtakuja kujuta
 
Pascal Mayalla wewe mbona umeruka sehemu moja uliyopitia? Wewe si ulipitia JWTZ, tena Ukonga ukapiga depo mpaka ukamaliza na kuwa askari kamili?
Mkuu Macho Mdiliko, kwanza ni kweli, mimi ni mjada kamil gado, baada ya JKT, niliunga JWTZ moja kwa moja na kupiga deppa Airwing had ku pass out na kuajiriwa joshing na MT number yang ninayo, ikitangaza too vita, mimi ni reserve soldier nadir tunaitwa mstari wa mbele, hata hivyo, huwa sijitaji, hata kenye CV yang siweki, kwa sababu sipendi kutisha watu humu, ili wanaonijua, na waliofanya Kazi na mimi na wanaondelea kumanya Kazi na mimi, wananijua sinsi ninavyofanya Kazi kijeshijeshi.
NB. Kuna kitu kinaitwa the right to privacy, hata kama unamjua otu fulani ni mjeshi, mwenyewe hajataka kujitambulisha ni mjeshi, wewe kumtambulisha ni mjeshi ni kuingilia uhuru wake wa the right to privacy.
P.
 
unachokisema ni kweli ila huoni siku hizi wewe mwenyewe unaitwa mzee wa pambio!? Umegeuka msifiaji sana, hii ni baada ya kutoka kuhojiwa na ile kamati uchwara!😬
Mkuu Kigogo Warioba, kwanza ile kamati ipe heshima sake, sio kamati uchwara. Mimi sio mzee wa pambio, siku zote nimekuwa mkweli kwenye mazuri, napongeza, kwenye mabaya, nakosoa.
P
 
Ila haya mambo mnayataka wenyewe..kwa vikao vizito nilivyowah kuhudhuria niliona njaa kali sana ya waandishi kwa hyo ya uwoya nikwakua aliamua kuwadhalilisha but in other side huo ndo uhalisia
 
Pascal Mayalla,
Kuna shida kubwa ya wasomi wa kiTanzania wakati wakiongea na umma kama mfano kupitia vyombo vya media kama JamiiForums n.k, wanashindwa kutumia lugha rahisi na taarifa fupi kuwakilisha wanachofikiri. Hupenda sana kunukuu vifungu vya sheria ,kanuni, marekebisho n.k

Ukiwasikiliza wasomi wengine wa nchi zingine ktk bara mengine, wakiongea ktk media huwakilisha moja kwa moja changamoto zao bila kuingiza makando kando niliyoyataja kama vile wapo shule wanatahiniwa kupata diploma, digrii au kutaka kutambuliwa na chama cha wataaluma wa fani husika.

Tubadilike maana wanaotusoma, kutusikiliza(Radio) au kututazama(TV/YouTube) katika media mbalimbali huchoka kuwafuatilia kwa kuchanganya masuala mengi na siyo ku-focus ktk katika changamoto husika wanayotaka kuizungumzia kwa lugha rahisi kuwakilisha ujumbe.
 
Nimependa tu huu mstari......
Asante Mkuu Idawa, watu tuna CV za kutisha ila hatuzitumii kutishia watu, haswa kwa kuzingatia baadhi ya fani ukiingia umeingia hakuna kutoka, hivyo ukitoka bora unyamaze.
P
 
Back
Top Bottom