Mechi ya Simba na Yanga CECAFA Mashabiki wasiende. Jeuri ndugu yake kusudi

GuDume

JF-Expert Member
Jan 18, 2015
6,652
14,247
Musonye anafanya mambo kiswahili sana. na inaonekana wazi jinsi ambavyo mara nyingi amekuwa akifanya mashindano haya kibiashara zaidi kuliko kimichezo. na hili jambo limekuwa likigharimu soka letu na centre africa kwa kiasi kikubwa sana. mara kadhaa kuna timu zimekuwa zikilazimishwa zifike fainali hata kama kiwango chao kidogo ili kuleta mapato makubwa katika mechi hizo.

sasa hili la kuzipanga simba na yanga kwenye kundi moja ili kulazimisha zikutane ni la kipuuzi. inakuaje kundi moja liwe na teamu mbili toka nchi moja wakati kulikuwa na uwezekano wa kuzigawa ili kuleta ushindani zaidi? nini kinampa mawazo kuwa team flan ikiwekwa kundi flani inawezekana isije kutana na kundi flani?

ni mawazo ya kipuuzi na tufikie wakati tuyakatae. mimi nashauri mechi ya simba na yanga mashabiki tuigomee wala tusiende uwanjani ili lengo lake musonya lisitimie. asitufanye sisi wapuuzi.na hii inajenga dhana mbaya kuwa mpira ni simba na yanga tu.. badala ya kuangalia namna gan ya kuhamasisha watu wapende kwenda uwanjani yeye anazidi kuendeleza dhana potofu kuhusiana na mechi ya team zetu.
 
jamaa anafanya uhuni sana ... mimi sijapenda uhuni wake...

Aliona akizitenganisha makundi, Yanga itatolewa mapema kwa hiyo haitawezekana kukutana na Simba ili mpunga ujae kwenye poochi. Sasa akaona dawa yake ni kuzikutanisha mapema tu asubuhi :D:D:D
 
Yanga mmeanza visingizio ili msije uwanjani.Mimi namshukuru MUSONYE mwaka huu tuwakomeshe kabisa sasa hapo mtakwepaje? Sport Pesa mmetukimbia hapa kundi moja
 
Kumbe Yanga akiwa kundi moja na Azam au JKU ndio sawa.. mbona zote timu za Tanzania hz.
Punguzeni ushabik mavi.
 
Kenya mmetukimbia...
hapa bongo pia mtukumbie??

kwa taarifa yako Sisi mashabiki ndio tumeomba iwe hivyo

maana mngekuwa kundi tofauti tutawakosa....tumejifunza kenya
 
Mkuu unalaumu lakini sijaona penye umeelezea mchakato mzima wa kupanga makundi unakuwaje?

Je ni mtu tu anaamua team fulani iwe kundi fulani au kuna mchakato maalum?
 
Yanga tuko busy na CAF confederation.. hayo mabonanza tunawaachia Simba na Azam wa mchangani...tutaleta kikosi under 20 kwenye Kagame
 
Back
Top Bottom