Me and my story, the love life | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Me and my story, the love life

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Sophie_scated, May 7, 2012.

 1. S

  Sophie_scated Member

  #1
  May 7, 2012
  Joined: Mar 20, 2012
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Heshima kwenu wandugu, nimekuja na maada inanihusu mimi nitajaribu kuifafanua ili mpata uelewa zaidi na muweze kunipa ushauri wenu, najua wapo watako kebehi lakini mungu anajua nini nia yangu.

  Mimi ni msichana naenda in my 30s, makuaji yangu yamekuwa ya simanzi somehow maana baba tulikuwa tunamwona part time, nikisema hivyo nikuwa ilikuwa ni nyumba ndogo licha ya hivyo lakini alijitahidi sana kwenye upande wa malezi yetu mimi na ndugu zangu na alijitahidi kutupa elimu ya kutosha na kuweza kutufungulia mlango mzuri wa maisha. Nikiwa bado nakua ndoto yangu ni kuwa na family bora na maisha bora not as much as I had

  Nimebahatika kupata kazi nzuri na nafanya idara fulani hapa nchini na kipato changu naweza kusema kinaweza kukidhi mahitaji yangu ya kila siku. Tatizo linakuja ni kuhusu my love life, sometimes I think I’m cursed, I could say I haven’t got the man who value me or see me or I see him as soul mate. Ninahakika I am wife material lakini sijui kitu gani ninachopongukiwa. Wale ninaowataka/wapenda na ningetamani wawe wangu, hawaonyeshi mapenzi kihivyo kwangu na niliowahi kuwa nao naona they’re here for something else than what I want . Na wale ambao sina mpango nao ndio huwa wananishobokea, fahamu kuwa kundi hili ni wale waume za watu zile njemba simply we don’t just click for different reason. Kwa maana hiyo walionipiga chini ni wengi sana all I can say WANAUME WAMENIUMIZA sana moyo wangu, nimelia mpaka sasa nami nimekuwa jasiri, no more crying. Nikishaamuona au nikihisi zile dalili namimi napiga chini, bora nusu shari kuliko shari kamili. Kitu ambacho nimejifunza na kuapply ITS ALL FAIR IN LOVE AND WAR!!

  Sasa nimekuja na sera mpya, nishakata tama na wanaume wa hapa mujini, wakweli wachache waliobaki sijui ni category gani, nafikiria kuhama mji naona kuzidi kuishi kunazidi kuweka negativity ya waume, ukianzia malezi ya kuwa na baba parttime maybe if I change environment and surroundings will bring back my love interest or atleast will look a man differently. Maana upweke unanimaliza, I need to start chapter mpya, umri unayoyoma sitaki 15 years later to come nijilaumu why I didn’t try. I want to be love and love in return.

  Tatizo ni kuwa huko ninakoenda sijui nitafanikiwa na huku ninakotoka nisije nikaharibu kabisa maana nishaanza kujizatiti kikazi.

  Naomba ushauri nini nifanye
   
 2. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #2
  May 7, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,431
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  sijakuelewa vizuri ? so unataka kujaribu waume za watu?
   
 3. LD

  LD JF-Expert Member

  #3
  May 7, 2012
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Sikia dada angu, neno la Mungu linasema hivi, Mpende jirani yako kama unavyojipenda wewe mwenyewe. Kwa neno hilo basi, naomba kwanza uanze kujipenda mwenyewe, kama ukijipenda mwenyewe utakuwa unajua unachotaka......Unataka mwanaume au unataka FURAHA. Kuna kitu nadhani unatakiwa kukielewa, hutakiwi kuumizwa mara 2, kuumia ni mara moja tu...baada ya hapo unajifunza unasonga mbele.

  Wewe ulipomizwa kwa mara ya kwanza ulichukua muda kutulia na kumuomba Mungu akusaidie? Mambo ya mahusiano yasichukue sehemu kubwa ya maisha yako. Usijiwekee dead line kwenye maisha yako. Ishi leo, furahia maisha yako leo, mengine yanakuja tu my dada.

  Wala hupangi, muombe Mungu akusaidie, tulia, jipange vizuri na Mungu wako.......fanya mambo kwa faida ya nafsi yako na ndugu zako na rafiki zako. Hayo mapenzi yatakufata tu.

  Usipojipenda mwenyewe utahangaika mwisho uumizweeeeeeeeeeeeeee, hadi ukajiue kabisa.

  Mwamini Mungu, jua kila jambo lina sababu chini ya jua hili.......Chagua kuwa na Furaha na Amani.
   
 4. KOKUTONA

  KOKUTONA JF-Expert Member

  #4
  May 7, 2012
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 8,344
  Likes Received: 391
  Trophy Points: 180
  Huko unakotaka kwenda unaenda tafuta mwanume wa kukuoa au unataka mwanaume wa kukupenda tu? Hebu fafanua kidogo
   
 5. LD

  LD JF-Expert Member

  #5
  May 7, 2012
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Dah, naombeni kuuliza hivi mwanaume wa kuoa anatafutwa je? Hizi mambo mbona mi sielewi. Yani unatoka tu na mission natafuta mwanaume wa kunioa? Halafu anapatikana au...manake hata ninaowasikiaga wanatafuta wake wakuoa....naonaga hawapati. Wanakuja kupata wakati ambao hawatafuti. Au akipata ndio ile mradi liende "NDOA"

  BUT....unaweka maisha yako, Furaha yako, na Amani yako kwenye kitanzi cha ndoa? Khaaaaa God help!!!!
   
 6. P

  Pokola JF-Expert Member

  #6
  May 7, 2012
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Mwenyezi Mungu mwenye Neema nyingi AKUSAMEHE na akupe AKILI. (Apparently, HUNA AKILI).
  :flypig:
   
 7. Billie

  Billie JF-Expert Member

  #7
  May 7, 2012
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 5,321
  Likes Received: 2,308
  Trophy Points: 280
  Pole sana ila jaribu kuchukua notebook uandike wote ambao wamewahi kukupiga kibuti alafu kila jina COMMENT ni nini kilikusababisha uachane nae hiyo itakusaidia kujiSCAN mwenyewe ujue ni sababu ukilipata litafutie sulushen kama linawezekana maana kwa ufahamu wng mdogo ni kuwa mwanamke mwenye kazi kwa hapa bongo yupo marketable sana hasa kupata mume wa kudumu.Inawezekana ukafikilia kuama nchi kwenda kutafuta bwana wa kutulia nae huku kitu au tabia kinachowafanya waage hujakitatua itakuwa kama mtu aliyekuwa anateka maji kwa kutumia pakacha akalitupa ili atumie tenga.Wa pwani wataelewa nin nazungumzia.
   
 8. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #8
  May 7, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Unahama mji kutafuta love or fresh beginning?
   
 9. zimwimtu

  zimwimtu JF-Expert Member

  #9
  May 7, 2012
  Joined: Mar 7, 2012
  Messages: 1,887
  Likes Received: 609
  Trophy Points: 280
  unahangaika bure tu dadaangu.... mume huja kwa wakati wake, wala si kuhama mji kwenda kumtafta.
  Kinachokumbua ni nini? Umri, Upweke, Shinikizo la wazazi au nini?. kaa utulie hapa mjini, kuwa bize na mambo yako then tatriiiiiibu utaanza kusahau na kufungua moyo kwa atakae onesha nia. utaolewa na kuwa na furaha.
   
 10. Ndechumia

  Ndechumia JF-Expert Member

  #10
  May 7, 2012
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 1,015
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  dada pole sana!!
  mi nakushauri usihame mjin kwa ajili ya kutafuta mtu wa kukuoa!
  endelea na kaz unayofanya ongeza maombi naamini mungu atakusikiliza.

  mume/mke huwa anakuja automatikal bila hata kujua au kuplani.
   
 11. Lord K

  Lord K JF-Expert Member

  #11
  May 7, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 213
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  USHASEMA UMEKUWA SUGU EEEE, HAYA! UNAPENDA KI SISTADUU NDO MAANA UNABWAGWA AU UNAKUWA NA Matarajio makubwa kwa mwanaume na kujisahau kuwa uhusiano bora na imara hujengwa na nyie wote na sio mwanaume pekee....Fuata ushauri wa Billie hapo juu utakusaidia kujitafakari upya na kukufanya ujue udhaifu wako ulipo na kujirekebisha.
   
 12. K

  Kidzude JF-Expert Member

  #12
  May 7, 2012
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 2,707
  Likes Received: 322
  Trophy Points: 180
  Aisee punguza standard za kidunia ongeza standard za kimungu utapata mume. Mumeo atakuona kwa macho ya rohoni wala si haya ya kibinadamu yaangaliayo external and phsyicaly appearance. Jaribu kuwa mweli kwa mungu wako si machoni pa binadamu just for three months utaona matokeo.
   
 13. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #13
  May 7, 2012
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Ulichoongea nimekielewa sana, na ninajua jinsi unavyoweza kuwa unaumia. wanawake wengi wakichelewa kuolewa, huumia sana moyo. hii pia ni mbaya kwasababu uchungu ukizidi sana huwa inapelekea hata kukosa mtoto wakiolewa, ndio maana unatakiwa kutake things easy tu...yaani ukiwa frustrated hata cycle yako inakuwa frustrated alafu huwa inaunda utomvu fulani kwenye mlango wa kizazi unaokuwa na acid inayoua mbegu zinazoelekea kwenye uterus...uchungu wa moyo siku zote ni hatari ndo maana tunashauriwa kufanya lolote ili kuepuka stress. kwa ushauri wangu, jaribu kutulia, fanya kazi kwa bidii ndani ya miaka hii miwili kuanzia leo, una unashiriki shughuli za kijamii yaani ujiassociate na jamii kila mtu awe anakuona. jitahidi usifanya uzinzi kuanzia leo, yaani utulie kabisaa...akija mme wa mtu mkimbize hadi watakaojua wakusifie, mwombe Mungu akupe mwanaume anayeona anafanana na wewe kuanzia kila kitu, Mungu anakupenda hivyohivyo ulivyo, hata kama ulishafanya mbwembwe nyingi za kujichanganya na maisha pengine, atakupa mwanaume ndani ya miaka hii miwili. ukimpata, mshukuru Mungu na umfuate katika imani...yaani ukaokoke. wakati mwingine pia huwa kuna nuksi...unapozini na mtu wakati mwingine unachukua nuksi zake kwasababu mnakuwa mnaungana naye kimwili mnapoingiliana, spiritual nuksi zinakuingia, nenda kanisani kaombewe, pengine una mapepo, nuksi, majini mahaba yaliyokuoa bila wewe kujijua na yanazuia na kukimbiza wanaume etc....nenda kanisani kaokoke na uombewe, utakuja hapa kutoa ushuhuda. huu ndo ukweli wangu naweza kukuambia.
   
 14. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #14
  May 7, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,260
  Trophy Points: 280
  Kuna thread nyingine kule inasema eti kuna Dada yeye bila kuwa na Degree au Masters kwake huna vigenzo!! mna mambo sana nyinyi kina Mama, Ukitaka a perfect Man unapaswa kumuumba wewe mwenyewe.

  Jiangalie sana huo umri ulionao ndio unapaswa kupata Mume wa Maisha yako unconditional love, otherwise ukishafikisha miaka 35 utakuwa kwenye option ya kugeuzwa nyumba ndogo au kuolewa na mtu aliyefiwa na mkewe au someone who Divorce.

  Watu wengi ambao kwa umri wako wanapaswa kukuoa either wengi wameshaoa au wako kwenye stable Relationship kwahiyo nakushauri uwe makini sana, maana unahitaji kuzaa ili ujenge Familia bora na muda wa kufanya hayo ndio huu unayoyoma.
   
 15. Zabibu

  Zabibu JF-Expert Member

  #15
  May 8, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 256
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  pole san ,zidi kumwomba MUNGU naye atakusaidia
   
 16. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #16
  May 8, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Jamani pole sana ..Ngoja tutafute mbinu za kusaidiana hapa...mungu akusaidie
   
 17. Edward Teller

  Edward Teller JF-Expert Member

  #17
  May 8, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,818
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  huna haja ya kuhama mji-kuna mdada niliwahi msikia naye yupo wilayan anataka kuhamia dsm ili naye apate mume hapo-
  ni kama hakuna sehem yenye manufaa kuliko nyingine-wewe jipange vyema tu utampata
   
 18. Freema Agyeman

  Freema Agyeman JF-Expert Member

  #18
  May 8, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,267
  Likes Received: 1,419
  Trophy Points: 280
  uko desperate tayari, ni vigumu sana "kupata mwanauma". Ukiwa desperate ni rahisi kwenda na mwanaume yeyote na kuishia kuangukia wrong choice mwisho wa siku unawachukia. Inawezekana tatizo sio wanaume isipokuwa wewe. Kibaya zaidi ni kwamba, unavyozidi kusample ndio unavyopunguza probability ya kupata right choice; kila anayekuja anajua umeshatumika sana, anakuogopa, anakutumia akichoka naye anakuacha.

  Mume mwema hutoka kwa Mungu, kama kakuandikia atakuja tu, tulia subiri.

  Halafu kama haijatokea kuwa na mwanaume umtakaye, ni afadhali uishi mwenyewe. Inakera kumpenda asiyekupenda au kupendwa na usiyempenda.
   
 19. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #19
  May 8, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  Pole, ila bado uko ndotoni ukiamka uniPM.

  Ishi uhalisia, na si matamanio.

  Hata kama una matamanio jaribu kuyafanya yatokee, unaweka embe zako chumbani wanunuzi watoke wapi?

  Unauza embe bei kubwa labda, zitakudodea shosti.

  Ukiona vipi, review vission yako naona kwa sasa imejikita kwenye kuolewa.
   
 20. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #20
  May 8, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  JIHESHIMU na UJIPENDE huku ukikazana kumwomba MUNGU utapata mume mwema.
   
Loading...