Mdude ni mwanasiasa mzuri wa upinzani aliyepuuzwa na chama chake

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
10,241
22,318
Tukisoma Biblia tunaona kwamba hata Mwenyezi Mungu wakati anachagua Manabii, Mitume na watu wa kufanya kazi zake hakuwa akichagua watu legelege na waoga. Nabii Musa kwenye ujana wake aliona ndugu yake anaonewa na Mmisri akachukia na kumpa kipigo hadi kumuua yule Mmisri kisha kumfukia.

Yakobo imeandikwa alipambana na Malaika. Mtume bora wa muda wote Paulo kabla ya kuwa Mtume alikuwa mtu hatari asiyeogopa lolote na katili haswa. Hata Yesu hakuwa mwoga, alikuwa akiwapa majibu ya shortcut wale Mafarisayo. Mifano ni mingi sana.

Hata hapa Tanzania tumeona Baba wa Taifa kupitia kauli zake alionyeshwa kukerwa mno na vijana waoga. Nikirudi kwenye mada ni kwamba kijana (anayeelekea uzeeni) Mdude Nyagali amekuwa ni miongoni mwa vijana wachache kwenye siasa za upinzani ambaye neno uoga kwake ni haramu.

Misukosuko aliyopitia kwa siasa zake ni mingi na mizito. Kwenye utawala wa awamu ya tano Mdude alikiona cha mtemakuni. Inasikitisha sana ila ndio imeshatokea.

Misukosuko yote anayopata Mdude inasababishwa na yeye kujiamini kupita kiasi na kushindwa kuhimili hisia zake hadi kujikuta kutoa matusi na maneno mengine ya kuudhi kwa viongozi wakubwa wa nchi.

Mdude ni miongoni mwa Watanzania wachache wasio na nidhamu kiasi kwamba kwenye maandishi yake huwa haandiki Mh. Rais au hata Mama Samia badala yake huandika Samia kama vile ni kijana mwenzake. Mbaya zaidi huandika "rafiki yangu".

Baada ya kutafakari kwa makini sana nimeona Mdude kama mtu aliyeingia kwenye siasa kwa juhudi zake binafsi bila kuwa na mjomba wala baba mdogo, sio mtu wa kulaumiwa sana kwa upuuzi anaofanya.

CHADEMA ndio wa kulaumiwa kwa madhaifu yote ya Mdude. Yule kijana ambaye ni asset muhimu ya upinzani ilibidi achukuliwe na hata kupelekwa kwa wataalamu wa mambo ya siasa kwenye vyuo bora akajifunze namna sahihi ya kufanya siasa makini.

Chama kimempuuza na kushindwa kuwekeza kwa vijana wake ambao ndio viongozi watakaowarithi kina Mbowe na Lissu.

Kwa ile confidence ya Mdude angeweza kuji-control upande wa hisia zake angekuwa bora kuliko kina Malisa, Yericko, Pumbulu, na wengine. Mdude ni "Pure Mpinzani".

CHADEMA iache kuwabeba watu wasio na sifa za kuitwa wanasiasa wa upinzani na kuwapuuza makada wake aina ya Mdude.

Ni kweli Mdude anakera sana ila chama kingemsaidia kujirekebisha angekuwa bora hata CCM wangeweza kumchukua.
 
Tukisoma biblia tunaona kwamba hata Mwenyezi Mungu wakati anachagua manabii, mitume na watu wa kufanya kazi zake hakuwa akichagua watu legelege na waoga. Nabii Musa kwenye ujana wake aliona ndugu yake anaonewa na mmisri akachukia na kumpa kipigo hadi kumuua yule mmisri kisha kumfukia. Yakobo imeandikwa alipambana na malaika. Mtume bora wa muda wote Paulo kabla kuwa mtume alikuwa mtu hatari asiyeogopa lolote na katili haswa. Hata Yesu hakuwa mwoga.. alikuwa akiwapa majibu ya shortcut wale mafarisayo. Mifano ni mingi sana...

Hata hapa Tanzania tumeona baba wa taifa kupitia kauli zake alionyeshwa kukerwa mno na vijana waoga. Nikirudi kwenye mada ni kwamba kijana (anayeelekea uzeeni) Mdude Nyagali amekuwa ni miongoni mwa vijana wachache kwenye siasa za upinzani ambaye neno uoga kwake ni haramu. Misukosuko aliyopitia kwa siasa zake ni mingi na mizito. Kwenye utawala wa awamu ya tano Mdude alikiona cha mtemakuni. INASIKITISHA sana ila ndo imeshatokea. Misukosuko yote anayopataga Mdude inasababishwa na yeye kujiamini kupita kiasi na kushindwa kuhimili hisia zake hadi kujikuta kutoa matusi na maneno mengine ya kuudhi kwa viongozi wakubwa wa nchi. Mdude ni miongoni mwa watanzania wachache wasio na nidhamu kiasi kwamba kwenye maandishi yake huwa haandiki Mh. Rais au hata Mama Samia badala yake huandika Samia kama vile ni kijana mwenzake. Mbaya zaidi huandika "rafiki yangu".

Baada ya kutafakari kwa makini sana nimeona Mdude kama mtu aliyeingia kwenye siasa kwa juhudi zake binafsi bila kuwa na mjomba wala baba mdogo sio mtu wa kulaumiwa sana kwa upuuzi anaofanya. CHADEMA ndo wa kulaumiwa kwa madhaifu yote ya Mdude. Yule kijana ambaye ni asset muhimu ya upinzani ilibidi achukuliwe na hata kupelekwa kwa wataalamu wa mambo ya siasa kwenye vyuo bora akajifunze namna sahihi ya kufanya siasa makini. Chama kimempuuza na kushindwa kuwekeza kwa vijana wake ambao ndo viongozi watakaowarithi kina Mbowe na Lissu.

Kwa ile confidence ya Mdude angeweza kuji-control upande wa hisia zake angekuwa bora kuliko kina Malisa, Yericko, Pumbulu, na wengine. Mdude ni "Pure Mpinzani". CHADEMA iache kuwabeba watu wasio na sifa za kuitwa wanasiasa wa upinzani na kuwapuuza makada wake aina ya Mdude.. ni kweli Mdude anakera sana ila chama kingemsaidia kujirekebisha angekuwa bora hata CCM wangeweza kumchukua.
Eti hata CCM wangeweza kumchukua, yaani CCM unaona ni bonge la chama. Chama kina miaka 50+ bado kinategemea vyombo vya dola kukaa madarakani nacho unasema kingemchukua Mdude?!
 
Eti hata CCM wangeweza kumchukua, yaani CCM unaona ni bonge la chama. Chama kina miaka 50+ bado kinategemea vyombo vya dola kukaa madarakani nacho unasema kingemchukua Mdude?!
Kabla ya ku-comment soma kwanza uzi uelewe. CCM haina ubaguzi kwa mtanzania yeyote. Si unaona cream yote ya CHADEMA imekula vyeo kwenye serikali ya CCM huku CHADEMA ikibakiwa na wapuuzi kama wewe na kina Lema?
 
Kabla ya ku-comment soma kwanza uzi uelewe. CCM haina ubaguzi kwa mtanzania yeyote. Si unaona cream yote ya CHADEMA imekula vyeo kwenye serikali ya CCM huku CHADEMA ikibakiwa na wapuuzi kama wewe na kina Lema?

Kula cheo kwenye serekali ya Tanzania nayo ni sifa? Je ingekuwa kwenye serekali ya US si ungeona yuko kwenye serikali ya mbinguni? Hakuna sifa yoyote kuwa kwenye serikali hizi za shithole countries.
 
Kula cheo kwenye serekali ya Tanzania nayo ni sifa? Je ingekuwa kwenye serekali ya US si ungeona yuko kwenye serikali ya mbinguni? Hakuna sifa yoyote kuwa kwenye serikali hizi za shithole countries.
Kwahiyo kuna sifa kuwa na cheo kwenye chama cha walamba asali CHADEMA?
 
Sahihi!

Emotional intelligence yake ipo low.
Mtu aliyehimili na kuvumilia kutekwa na kuteswa na watu wenye hasira na silaha, na yeye akabaki composed and collected, bila kuwatukana, ku crack, kulia, kuuza siri, kuhama chama, huwezi kusema ana low emotional intelligence.

Aliweza kutulia mpaka wauaji wakatulia na kumtupa mzima, akatoka salama. Hiyo ni stupendously high degree of emotional inteligence.


You must be nuts.
 
Back
Top Bottom