Mdude Chadema awaanika waliomteka

Hizo ndizo akili za kiform 2 wanazosema. Yaani alitaka asikari akisikia kelele mitaani anatimuka tu kutoka ofisini kwenda kunako hizo kelele. Polisi hawafanyi kazi hivyo. Wakampime akili huyu!
 
Kuwataja kwenye nyaraka/hati ya mashtaka (yaan "PLEADING") sio udhalikishaji/kumshushia mtu heshima) ila kumtaja kwny media ni kinyume chake.
 
Kuwataja kwenye nyaraka/hati ya mashtaka (yaan "PLEADING") sio udhalikishaji/kumshushia mtu heshima) ila kumtaja kwny media ni kinyume chake.

..Kweli.

..Na Mdude aliwasilisha malalamiko yake kwa Tume ya Haki za Binaadamu lakini tume wamekuwa wakimzunguza tu.

..Tusubiri kesi yake itakapotajwa. Natumaini atapata HAKI yake.

NB.

..Mdude amewahi kushtakiwa mara mbili kuhusu uchochezi. Na mara zote ameshinda kesi, na serekali imeshindwa ku-prove madai yake dhidi ya Mdude.
 
Huyo ni kama marehemu kambona na zitto walivyotuahidi kutaja watu wenye account tukajazana kwenye mkutano hakuna la maana walilolisema. Kijana wameshamuharibu bora Nondo aliwahi kuachiwa akiwa na akili zake huyu ni msukule tayari

Yeye ametekwa na wasiojulikana; sasa atawatajaje watu asiowajua?
 
Hiki kikosi cha ulinzi wa heshima ya rais kinachohangaika na akina Mdude ni hovyo sana. Hivi hawajui kuwa matendo yao yanasababisha madhara makubwa mara elfu kwa nchi yetu kuliko madhara yanayosababishwa na maneno ya akina Mdude? Very primitive! Nchi ya Nyerere sasa imekuwa kituko katika jumuia ya kimataifa! Hope kuna siku hawa watapata haki yao.
 
Naona huijui maana halisi ya ushujaa
Yaani huyu bwana mdogo anatukana viongozi hovyo ndio mnamuita shujaa?
Tumieni basi hata akili kidogo jamani

Kwa hiyo adhabu ya kutukana viongozi ni kutekwa na kuumizwa? Very primitive.
 
Pole sana kijana ila Acha kuzunguka sana.....

Advice.
Weka wazi tukio la kutekwa kwako but with Evidence siyo mambo ya kuhis maana kwenye Taaluma ya Sheria Mambo yakuhisi sijui fulan...... Nilimshitaki hivyo huenda alihusika na tukio langu la kutekwa, hicho kitu hakipo!!!!


Endelea kutoa Maneno ya Mafumbo wakushughulikie jumla...

Nchi hii inajitaj mtu uishi kwa misingi ya kisheria na siyo kuropoka ropoka hovyo without evidence eti uwe Maarufu.

Tulia jenga hoja na uliza swali sehem husika na siyo mtandaoni utaonekana una MAJUNGU MKUU hata kama swali lako linamaana kwa Maslai Mapana ya Taifa...

Serikali haifanyi kazi informal angalia hoja zako unaziwasilisha wapi?
Je Kwenye Social Media(Fb etc) au unaandika document yako na kuiwasilisha OFISI husika...

Mytake. Watanzania wenzangu tujifunze namna bora ya kufikisha ujumbe/hoja/swali kwa wahusika ili upate ufafanuzi..
 
Atazunguuuka weee ila kuwataja kwa majina hatoweza japo ndio kiu yetu kubwa.....naweza sema atatupotezea muda tu.wabongo hawana ujasiri huo
Atajuaje majina yao?

Na kama kweli atayajua, kutoyataja majina hayo itamsaidia vipi, asitekwe tena?

Nadhani ni sahihi kusema, hayajui majina. Huyu kwa jinsi alivyo, sio mtu wa kutotaja.
 
Donc, il faut etre soigneux toujours quand on veut critiquer l'autorite....en utilisant une langue appropriee et convenable
Je valide .J'aimerais savoir ,où est ce que avez-vous apris le français ?
 
Unaonekana mtoto wewe . Mambo hayawagi rahisi hivyo. Labda kwa lugha kama za membe anaweza kupandikiza ujassusi wa namna hiyo . Ila sio logic yoyote hapo
Mshanza kuweweseka mara hii acha hawataje mnafikiri mdude Sawa na kina mo hyo kidume haswaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…