Habari wakuu. Nimepita maeneo ya Ubungo leo nikapita Landmarks Hotel nikakutana na bango la kubadilishwa kuwa hostel kuanzia September. Kwa hali hii sijui ni akina nani hawataisoma namba.
Nadhani kalenga sana soko la wanafunzi wa Udsm lakini sijajua gharama zake kama zitakuwa affordable, labda watu wa masters au foreigners.
Ina maana chumba kimoja walale watu sita!Kodi ni 160000/#Tsh per bed per month 1 room ina double deka 3 means vitanda 6.mi jamaa namsifu sana kwa majengo yake yamekaa design flan hivi ambayo yanaweza kuwa changed kwa matumizi mfano yanaweza kuwa hata hospitals
Utakua mburula sana kama utawekeza kikubwa vivo halafu ushindwe kucontrol mapatoJamaa atakuwa amechoka kumnufaisha meneja wa hoteli. Unaambiwa leo watu hawajajaa kumbe vyumba vyote vimejaa full.
yani mkuu hicho tu kinanifanya niogope kufanya biashara bongo. Uaminifu ni sifuri. Ndugu ndio kabisa ukimuweka akisimamie yani atakupiga panga vbaya sana. Kamwe hatutaendelea tusipoacha hii tabia. Kuna jamaa alimtumia bro wake hiace flan yani wee acha hadi imeharibika jamaa hajaona hata buku na mizinga haishikumpiga. Inakera sometimes nasemaga CCM ipo sahihi tu kutuoneaJamaa atakuwa amechoka kumnufaisha meneja wa hoteli. Unaambiwa leo watu hawajajaa kumbe vyumba vyote vimejaa full.
wanaocheka ni wapumbavu, jamaa atapiga hela nzuri mno kwa wastani wa vyumba kumi tu hawezi kosa 35mil ndani ya miezi minne sasa ni hela ndogo hio!?Ni upumbavu kuchekelea matatizo ya watu!kumbuka nawe huko uliko soon utavunjiwa nyumba kwasababu umejenga kwenye hifadhi ya barabara !pia wewe mfanyakazi soon muajiri wako atapunguza wafanyakazi na wewe ni miongoni mwao!
Lazima hali itakuwa mbaya.....hakuna wateja ndio maana mmiliki ameona bora iwe hostel mpangaji anakaa zaidi ya miezi 6. Sasa hivi business ya hotel (pamoja na utalii) imeshuka sana. Hela imeshuka thamani, uchumi wa mtu mmoja mmoja nao unadidimia......nchi ikikurupuka kwenye sera zake za kiuchumi na kisiasa mambo ndiyo anavyokuwa.