PreGE2025 Mdomo huponza kichwa - Tundu Lissu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Tunazumgumza Lissu,Chadema,No Reform no Election Serikali ya Tanganyika,Katiba mpya CCM,G55,Mbowe,Raisi Samia kwa sababu kuna kitu au jambo la kuzungumza ambalo linataka attention.

Wengine wanakuja na maoni mbali mbali,wengine wanakuja na amri,au tii bila shurti.Na katika hayo yanazuka au yanazaa,maandamano,kejeli,uchawa,matusi ya nguoni mapatano,utengano,full shangwe,na wakati mwingine majeraha na misiba ambayo ingeepukika.

We are human beings sisi sio beast sisi binadamu hujifunza tokea anapozaliwa hadi anapofariki.Toka tukiamini the world is flat hadi kujua dunia ni sphere yaani mpira.

Katika malumbano ya Lissu wa Chadema vis Serikali ya CCM
Wananchi wanataka convincing language,na kama inashindikana to convince wananchi rudi kwenye drawing board ujipange upya.
 
Kama mtanzania ambaye nimempigia kura Mheshimiwa Lissu mara mbili kwenye chaguzi zilizopita (jimboni na uraisi), naamini hajafanya kosa la uhaini na hayo ni mashtaka ni ya kutengeneza na hewa, THAT BEING SAID sikubaliani na kauli ambazo Mh. Lissu amekua anazitoa kwenye mikutano hivi karibuni, sababu si za busara.

Naona kila mtu ambaye hakubaliani na umma wa mitandaoni anashambuliwa, tunakosa ukomavu kwa kisiasa wa kuchambua hoja bila kebehi na matusi. Mitandao ina tabia ya kutengeneza echo chambers za kusikia yale tu tunayotaka kusikia na kujiaminisha kuhusu usahihi wake.

Si lazima tuchukue yote wanayofanya viongozi wetu bila kuchuja, kukosoa, kushauri au kupinga.

Vitu viwili vinaweza kuwa sahihi kwa wakati mmoja.
  1. Mh. Lissu amefunguliwa mashtaka hewa ya kuzuia harakati zake kisiasa na hili si jambo sahihi wala la kufumbia macho. 

  2. Mh. Lissu akosolewe asiendelee kutoa kauli ambazo hazina afya kwa taifa letu, hasa kama kweli tunataka mabadiliko bila machafuko.

CCM wamefanya hizi siasa za uchawa na “ndiyo mzee” na sasa tunataka mbadala wao. Naona kuna watu wanalazimisha upande wa upinzani uelekea kule kule ambapo tumekua tunakupinga kwa chama tawala. 

Unakubaliana na haya au lah, jibu kwa hoja na si mihemuko. Kama unaamini mabadiliko lazima yaambatane na machafuko au vurugu, then tueleweshe kwanini ni lazima iwe hivyo!

Soma pia:
Uchambuzi wa Kisheria juu ya Hati ya Mashtaka ya Uhaini dhidi ya Tundu Lissu
WE NEED REFORMS.
 
Kimsingi Tanzania mabadiliko ya makubaliano kwa maongezi ya kisiasa hayawezekani.

CHADEMA wamejaribu hili wakaona ulaghai wa 4Rs.

Hivyo, kwa mtu anayetaka mabadiliko, habari za maongezi ya busara hazina tija.

Panahitajika timbwili kubwa sana, ambalo ndilo Tundu Lissu kalianzisha.

Tundu Lissu ni mwanasheria, alijua anachosema ni nini na kitasababisha nini. Na walivyomkamata ndicho alichotaka.

Wamemsaidia kuifanya "No Reforms, No Election" ya Tanzania kuwa hoja inayozungumziwa kimataifa kote huko BBC, Aljazeera, Amnesty International etc.

Nelson Mandela asingekubali kuwa tayari kufa katika "Rivonia Trials" ili kupigania kuondoa utawala dhalimu wa kibaguzi Afrika Kusini, angesema atumie mazungumzo ya busara tu na makaburu, unafikiri utawala wa kibaguzi ungeisha ulivyoisha Afrika Kusini?

Mazungumzo ya busara ndiyo yametufikisha hapa baada ya miaka 30 ya demokrasia ya vyama vingi Tanzania.

Sasa tunataka mazungumzo ya busara zaidi ili yatupe nini?

Albert Einstein alisema kufanya kitu kile kile mara nyingi na kutegemea matokeo tofauti ni ukichaa.

Tundu Lissu anakataa ukichaa huu.

Wanamfanya Lissu Mandela.
 
Hatma ya Chadema ni Nini?

Je yale Makaburi ya Kipanya, ndiyo yameshapata maiti ?
Kwa sasa ni mgumu kujua nini kitatokea, lakini kuikosa chadema bungeni na kwenye chaguzi zijazo za serikali za mitaa kutatengeneza pengo kubwa sana.
 
Kimsingi Tanzania mabadiliko ya makubaliano kwa maongezi ya kisiasa hayawezekani.

CHADEMA wamejaribu hili wakaona ulaghai wa 4Rs.

Hivyo, kwa mtu anayetaka mabadiliko, habari za maongezi ya busara hazina tija.

Panahitajika timbwili kubwa sana, ambalo ndilo Tundu Lissu kalianzisha.

Tundu Lissu ni mwanasheria, alijua anachosema ni nini na kitasababisha nini. Na walivyomkamata ndicho alichotaka.

Wamemsaidia kuifanya "No Reforms, No Election" ya Tanzania kuwa hoja inayozungumziwa kimataifa kote huko BBC, Aljazeera, Amnesty International etc.

Nelson Mandela asingekubali kuwa tayari kufa katika "Rivonia Trials" ili kupigania kuondoa utawala dhalimu wa kibaguzi Afrika Kusini, angesema atumie mazungumzo ya busara tu na makaburu, unafikiri utawala wa kibaguzi ungeisha ulivyoisha Afrika Kusini?

Mazungumzo ya busara ndiyo yametufikisha hapa baada ya miaka 30 ya demokrasia ya vyama vingi Tanzania.

Sasa tunataka mazungumzo ya busara zaidi ili yatupe nini?

Albert Einstein alisema kufanya kitu kile kile mara nyingi na kutegemea matokeo tofauti ni ukichaa.

Tundu Lissu anakataa ukichaa huu.

Wanamfanya Lissu Mandela.
Brilliant
 
Nyie mnajua huu ni uzi serious, acheni basi kuwaza vipochi manyoya 😂 😂
JF is a hell of a drug...

Ulituaga hapa kwa mbwembwe eti unaondoka sijui nini tunaojua saikolojia kidogo na ishu za dopamine tukawa tunakuzumu tu 😂😂😂

Hebu mada za kikombozi na kuinua jamii kama zile za kuifinyia kwa ndani na ziendelee...
 
Nakubaliana na wewe kuhusu nafasi ya mahakama. Ila wakati mwingine mahakama inatumiwa vibaya kupoteza muda na kupoza vuguvugu la kisiasa; na nafikiri hicho ndiyo kinachoendelea kwa sasa na Mh. Lissu.

Ila pia nafikiri kauli kama ile iliyowekwa kwenye hati yake ya mashtaka, haichochei amani wala mabadiliko bila machafuko.
Kipi hapo hakijawahi kufanywa kubadirisha msimamo wa kiditeta wa CCM. Hakuna dialogue ambayo CCM wamewahi kuja na amani. Ukifika wakati wanachomoa makucha openly.

Kauli kama ile. Ipi hiyo ambayo CCM hawawezi kuvumiliana na kuitisha dialogue? Watanzania wafanye machafuko? Kwa kauli gani?

CCM waoga, kwa sababu wako guilty
 
JF is a hell of a drug...

Ulituaga hapa kwa mbwembwe eti unaondoka sijui nini tunaojua saikolojia kidogo na ishu za dopamine tukawa tunakuzumu tu 😂😂😂

Hebu mada za kikombozi na kuinua jamii kama zile za kuifinyia kwa ndani na ziendelee...
Mkuu niliaga na niaisema sitakuwepo siku za wiki, au hadi weekend mnataka niwe kazini 😅😅 Sijaingia humu kwa wiki 2, leo nimepata wasaa.

Mada za kikombozi zitakuwepo sana weekends kuanzia leo 🤣🤣🤣
 
Najua hujui kuwa sa100 amechongewa mti mchongoka na akadanganyikq ameukalia kwenye ncha...unajua matokeo
 
Kimsingi Tanzania mabadiliko ya makubaliano kwa maongezi ya kisiasa hayawezekani.

CHADEMA wamejaribu hili wakaona ulaghai wa 4Rs.

Hivyo, kwa mtu anayetaka mabadiliko, habari za maongezi ya busara hazina tija.

Panahitajika timbwili kubwa sana, ambalo ndilo Tundu Lissu kalianzisha.

Tundu Lissu ni mwanasheria, alijua anachosema ni nini na kitasababisha nini. Na walivyomkamata ndicho alichotaka.

Wamemsaidia kuifanya "No Reforms, No Election" ya Tanzania kuwa hoja inayozungumziwa kimataifa kote huko BBC, Aljazeera, Amnesty International etc.

Nelson Mandela asingekubali kuwa tayari kufa katika "Rivonia Trials" ili kupigania kuondoa utawala dhalimu wa kibaguzi Afrika Kusini, angesema atumie mazungumzo ya busara tu na makaburu, unafikiri utawala wa kibaguzi ungeisha ulivyoisha Afrika Kusini?

Mazungumzo ya busara ndiyo yametufikisha hapa baada ya miaka 30 ya demokrasia ya vyama vingi Tanzania.

Sasa tunataka mazungumzo ya busara zaidi ili yatupe nini?

Albert Einstein alisema kufanya kitu kile kile mara nyingi na kutegemea matokeo tofauti ni ukichaa.

Tundu Lissu anakataa ukichaa huu.

Wanamfanya Lissu Mandela.
Mkuu Kiranga kama approach za busara na amani haziwezekani, Lissu anataka kufanya nini sasa? Hayo mabadiliko tunayapataje? au ndiyo kupigana wenyewe kwa wenyewe (civil unrest / war)
 
Tulia wewe, Lissu anagesabu kali sana na alijua ccm watajichanganya kumkamata.

Ona dunia nzina inamtaja.
Nani alitegemea kuwa Lissuvatatoboa January dhidi ya jabali Mbowe?

Niamini kila alisemalo Lissu ni mtego kw kenge wa Lumumba na dola.

Sasa wamejaa kwenye mfumo
Sawa, acha tuone 💯
 
Mkuu Kiranga kama approach za busara na amani haziwezekani, Lissu anataka kufanya nini sasa? Hayo mabadiliko tunayapataje? au ndiyo kupigana wenyewe kwa wenyewe (civil unrest / war)
Inawezekana likazuka timbwili la kisiasa tu ambalo kwenye civil war halijafika na kwenye mazungumzo ya busara halipo.

Ndiyo hayo maandamano mpaka kieleweke.

Ila hawa Watanganyika sijui kama wataelewa hili somo na kukubali gharama zake.

Nawaona kama wanapenda sana habari za hewala hewala na falsafa za funga kombe mwanaharamu apite.
 
Sawa, acha tuone 💯
Huyu mama hajui siasa, hajui mitego ya kisiasa, wala hajui madhara ya siasa za hovyo.

Ngoja wamfundishe hila za siasa.

Kibaya zaidi wenzage wote hadi waziri mkuu wameamua kuwa machawa...hiii ni hatari kwake.
Wanamwingiza mkenge ili aharibikiwe zaidi
 
No election imewavuruga vilivyo hadi mmeomba poo kwa mapori - ccm-

mwaka huu mtajichagua wenyewe. Siku ya uchaguzi itakuwa kama siku ya kawaida - vituo vyeupee pee. Watanzania washaamua ujinga tena baasii.
 
Mkuu niliaga na niaisema sitakuwepo siku za wiki, au hadi weekend mnataka niwe kazini 😅😅 Sijaingia humu kwa wiki 2, leo nimepata wasaa.

Mada za kikombozi zitakuwepo sana weekends kuanzia leo 🤣🤣🤣
JF hii uraibu wake hata kokeini ikasome. Wafanya masikhara nini!

Karibu tena bageshi 😂😂
 
Back
Top Bottom