Mdogo wangu kabambikiwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mdogo wangu kabambikiwa

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Fidel80, Dec 18, 2009.

 1. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #1
  Dec 18, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Wapwazi na maguest members nina mdogo wangu mchunga kondoo alipata kifaa alipo kuwa katika harakati za kurudisha kondoo kundini huko Songea na wakaahidiana wataoana. Toka ampate yule binti ilipita miaka kama 2 kisha dogo akaja kwetu kutueleza nia yake hiyo thabiti nasi tukamuunga mkono akaenda Song kuonekana kwa wakwe wakataka mahali laki 5 basi sisi tukajipanga na kuchangishana fedha dogo akaenda kumaliza.
  Baada ya taratibu kukamilika dogo akamleta Dar yule binti na ikumbukwe dogo hajawahi mega alikuwa anasisitiza anataka harusi aje ajizindulie yeye mwenyewe. Sasa alipo kuja nae Dar katika harakati za kutambulisha kwa ndugu, jamaa na marafiki wale wenye macho makali kama renzi wakabaini yule binti mjamzito, ikabidi wamwite dogo na kumueleza dogo akawa ana bisha akasema mbona sijawahi mega! wakamshauri aende hospital wakampime lakini dogo hapo hapo aliingia na wasiwasi tokea afike yule binti alikuwa anataka wawe wanalala wote ili dogo amege lakini msimamo wa dogo ulikuwa mkali maana ameiva katika neno basi binti akawa ana lala na ndugu wengine huku yeye akiwa peke yake. Walivyo pima ikabainika binti ana mimba ya miezi 3 dogo alichanganyikiwa sana.
  Msaada kwenu wapwazi zile pesa tulizo toa kule 500,000/= tufanyaje kilicho enda kwa mganga kinaweza rudi kweli? maana wakati wanachumbiana alipo tajiwa kiasi kikubwa cha pesa hicho watu tulishtuka tulimshauri sana hakushaurika tukawa hatuna jinsi ni kuchangishana tu.
  Ni nn kifanyike wakuu msaada kwenye tuta.
   
 2. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #2
  Dec 18, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  kuna haja ya kumlaza 'mkwe' au wakwe polisi hapo. Huo pia ni Utapeli kama ule wa EPA, Lol!
   
 3. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #3
  Dec 18, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0

  huenda na hao wakwe hawajui kama binti yao ana hali hiyo.....nyie fanyeni tu kiendacho kwa mganga......
   
 4. JS

  JS JF-Expert Member

  #4
  Dec 18, 2009
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,065
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  nendeni mkadai mahari yenu
  mi ndo maana siku zote niko against na hii biashara ya mahari sijui kulipiwa mahari mambo yenyewe ndo kama hayo Fidel. Kaidaini hela yenu
   
 5. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #5
  Dec 18, 2009
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Fidel nafikiri kaeni chini kwanza mtulize munkali. Ni vizuri mkajua chanzo kabla ya kuanza kudai na mambo mengine.

  hakuna mzazi anaweza fanya utapeli wa aina hiyo, inawezekana huyo binti alimegwa na wengine wakati wazazi wake hawajui. Mdogo wako nae hakutaka mambo makubwa kwa sababu alihitaji kuishi na mke kihalali. Ninaamini kiumbe ndani ya huyo dada hakina makosa, pili kutoa mimba ni dhambi kubwa sanaaaaaa, tatu kama kijana bado anammpenda msichana waoane tu, huyo dada ni bahati mbaya kutokea hivyo hakudhamiria.

  Kikubwa muulizeni bwana mdogo bado anampenda binti kama ndiyo basi mwache mimba ikue, izaliwe mambo menggine yatafuata. Maamuzi ndani ya hili swala yanahitaji uwepo wa Roho mtakatafu kibinadamu hatuwezi. Nahisi bwana mdogo kwa sababu ni muumini safi ataelewa na Mungu atamuongoza kwa hili.

  Wish him all the best! Samehe saba mara sabini.
   
 6. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #6
  Dec 18, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Yaani nilijinyima pesa ya week end nikamchangia dogo alafu tumeuziwa mbuzi kwenye gunia.
   
 7. JS

  JS JF-Expert Member

  #7
  Dec 18, 2009
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,065
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Pole ndo mambo hayo
   
 8. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #8
  Dec 18, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Inauma sana yaani nawachukia sana wanawake wenye tabia kama hizi
   
 9. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #9
  Dec 18, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  No dis intended, lakini hayo ndiyo madhara ya kuwa deep kwenye neno bila street smarts.

  Having said that, namu admire dogo wako sana kwani ni watu wachache sana wanaoweza kuwa na msimamo thabiti kama huo. Na sasa on the flipside msimamo wake huo umemsaidia, kwani angekuwa na mapepe ya kumega angebambikiwa kitu si chake.

  Upande wa bibie, huyu wala si wifey material kabisa, kwani alifanya kuseebuka wakati yuko na mkali.

  Kuhusu mahari hiyo mbona kiafrika afrika inadaiwa kabisa, tena in full kwa sababu mkali hajaoa wala kumega, na sababu ni kubwa tu.Tena kama familia ya demu inajiheshimu ikipewa issue itataka kuwarudishia mara moja ili kusiwe na soo wala nini.Tena muwahi msije kuchelewa mkakuta zishalipiwa ada za shule na kununulia pembejeo etc, wengine wanataka kumalizia matatizo yao yote kwenye mahari.

  Nini huyu ambaye hajaolewa wala kuguswa, viwanja vya kati hapo watu wanaoa, wanamega, wanapiga, wanafukuza halafu wanadai mahari. Kinda primitive and all and it's not like I'm advocating lakini naonyesha jinsi gani kesi ya huyu mkali kama ilivyoletwa hapa ilivyo ya kistaarabu ukiilinganisha na washashi wengine wanaodai mahari.
   
 10. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #10
  Dec 18, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280


  ha ha ha ha bluray nimecheka sana..
  viwanja vya wapi huko ambako watu wanaoa na kumega na kufukuza
  na kudai talaka?middle easr sio?
   
 11. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #11
  Dec 18, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  halafu mahari ya lakitano mnadai?
  mngetoa milioni tano ingekuwaje?
   
 12. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #12
  Dec 18, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Mazee,

  Hata kama ni shilingi tano, wanayo haki ya kudai.Hapa kuna swala la principle pia.Wengine usipodai mahari wanaelewa kwamba unachumbia / umeoa bado, na hata mahari ulitoa wanaweza kusema.Kudai mahari kunaweza kuwa symbolic kuonyesha mnarudisha bibie bila kuoa.

  The whole mahari thing is outdated if you ask me, it commoditize a woman and create all these unnecessary issues.
   
 13. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #13
  Dec 18, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  ungenijibu hili....

  ha ha ha ha bluray nimecheka sana..
  viwanja vya wapi huko ambako watu wanaoa na kumega na kufukuza
  na kudai talaka?middle east sio?
   
 14. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #14
  Dec 18, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135

  Ha, mazee hili mbona bongo viwanja fulani vya kati watu wanafanya sana.

  I could name names lakini naogopa naweza kunyimwa uchumba, like I am the marrying type anyway.
   
 15. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #15
  Dec 18, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  but sijawahi sikia..
  au musoma????
  kwa tanzania kuoa na kumega na kupiga
  na kuacha?

  but huko misri na saudia arabia its common
  kama umeoa nakumega na kukuta sio bikira.
   
 16. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #16
  Dec 18, 2009
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,222
  Likes Received: 2,087
  Trophy Points: 280
  Pole sana man!
  Ningemshauri mtumie busara za kiutu uzima kutatua kadhia hii, msikurupuke kudai mahali. Sort out some matters first!
  Huyo dogo mmemuuliza kama anataka kuendeleza uhusiano na binti? Msimamo wake ni upi katika uhusiano huo? Huenda ukawa unamsemea kuwa amwache mtu anayemzimia ilhali yeye bado anataka kuishi naye hata kama demu si mwaminifu, hili lawezekana sana hapa duniani, mapenzi ni upofu bro!

  Njoo na jibu tuendelee kumega mada!
   
 17. p

  p53 JF-Expert Member

  #17
  Dec 18, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 613
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Haya mambo ya kubambikana mizigo ni noma.Yalitaka yanikute haya siku hizo bongo.Kuna kicheche kitaa kilipigwa na jamaa kikajifunga halafu kikajifanya demu zimikia.Bahati nikawa namega kwa mpira manake kilikuwa kama ki gf changu na kila mtu mtaani mpaka wazee wake walifahamu.Baadaye tukapoteana kama miezi saba hivi,nakutana nae tumbo kuubwa na kila mtu mtaani akawa anapakaza eti mzigo wangu.Nikaamuuliza vipi?Akakiri siyo yangu,ni ya msela mmoja konda wa hiace.Aliogopa kunichomekea manake nilikuwa navaa flana kila mechi hivyo mbilinge yake ingekuwa kubwa.Lakini watu hawakuamini na wakawa wanasubiri kwa hamu mtoto azaliwe ili wanifananishe kwa sababu inavyoelekea mimba ilitungwa wiki chache sana baada ya kutemana na jamaa na kuanza uhusiano na mimi.Nikasema duuh kama nisingekuwa navaa jezi kwenye mechi saa hizi yangekuwa mengine na huyu mtoto lazima ningebambikizwa tu.

  Mkuu Fidel poleni.Yanatokea sana haya na wengi wanalea mimba na watoto ambao siyo wao bila kujua.
  Kama walivyopendekeza wengine,muulize kwanza mdogo wako.Kama yuko tayari kulea mimba ya mtu,hamtakuwa na sababu tena ya kwenda kudai mali.
   
 18. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #18
  Dec 18, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,664
  Likes Received: 1,506
  Trophy Points: 280
  Mi nadhani kiutarayibu kwa vile mahari yalitolewa ili kupata mke na mke ameshaonyesha kukosa uaminifu hata kabla ya ndoa (na assume kuwa hakubakwa) basi mahari irudi fasta fasta la sivyo mumburuze mahakamani
   
 19. The Intelligent

  The Intelligent JF-Expert Member

  #19
  Apr 30, 2014
  Joined: Dec 27, 2013
  Messages: 2,488
  Likes Received: 256
  Trophy Points: 180
  Kachukueni chenu.
   
 20. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #20
  Apr 30, 2014
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,664
  Likes Received: 1,506
  Trophy Points: 280
  Mpwa hii issue iliishaje
   
Loading...