Mdogo wangu anakaribia kukosa mke kisa dini tofauti

Mdogo wangu anakaribia kukosa mke kisa dini tofauti

hao ni SABBATARIAN wanaosali siku ya kwanza ya juma .....si christians.....

Hii post haijapata msabato hata mmoja walau kurudisha kombora?...
I will try..

Yesu mwenyewe alikwenda sinagogi na akafundisha, by then ilikuwa jumamosi.

Alikufa siku ya maandalio ya sabato (ijumaa), akapelekwa kaburini jioni muda wa kuandaa maiti ulikosekana akazikwa hivyo hivyo.

Jumapili asubuhi wakawahi kwenda kumpaka mafuta waliyoshindwa kumpaka ijumaa ndio wakakuta tayari kashafufuka

Sasa hawa jamaa wanasema kama mungu aliheshimu hiyo siku akaitenga siku alipoumba dunia na mpaka akaiandikia amri enzi za musa na wakati ule wa kuokota mana hakushusha mana jumamosi, yesu nae akaja akaiheshimu mpaka kaburini.... inakuwaje wewe mwanadamu utafute ya kwako? Halafu unaendelea kusema unafuata yesu basi mfuate kweli kwa kila alichofanya na alichoagiza vinginevyo fata wanadamu waliobadilisha.

Ndio wasabato ni wakristo kabisa lakini huo msimamo wao unawafanya watofautiane na wakristo wengine wote
 
ukweli ni kwamba jambo la dini katika maisha ya ndoa linaumuhimu mkubwa sana kwa mustakabali wa maisha ya usoni , katika hatua za awali uonekana ni jambo la kawaida na halipaswi kuwa kikwazo katika mapenzi , baada ya kitambo kidogo madhara yake hujitokeza hasa kwa wale wanaotambu dini yao na umuhimu katika maisha yao , waambie wafikiri chanya na kuamua kwa dhati na si kwa msukumo wa kihisia itakuwa shida baadae
 
Mapenzi ya kweli yakihusika, zingine zote ni kelele za chura ambazo hazimzuii ng'ombe kunywa maji. Namaanisha binti kama kakolea anabadilika yeye na nyumbani anatoroka ili kuwakomoa wazazi wake mpaka mwisho wanakubali mabadiliko, kwa upande wa pili man akikolea ndugu zake na kelele zao zote anawaona feki anabadilika anaozeshwa hata na kanisa maana ndugu wamesusa.

Familia ikiendelea imara waliosusa wote wanajirudi maisha yanaendelea. Mabadiliko ya aina yoyote ile si mepesi lakini yakifanywa kwa moyo huwa marahisi lakini yakifanywa kwa ajili tu ya kutimiza lengo fulani huwa magumu sana maana hufanyika nusunusu na kinafiki. Hii ni kwa madhehebu na dini pia

Yani hata mimi naona tatizo dogo sana ilo mkuu wanalikuza wenyew hawajaamua tu yan kufunga iyo ndoa
 
Hii post haijapata msabato hata mmoja walau kurudisha kombora?...
I will try..

Yesu mwenyewe alikwenda sinagogi na akafundisha, by then ilikuwa jumamosi.

Alikufa siku ya maandalio ya sabato (ijumaa), akapelekwa kaburini jioni muda wa kuandaa maiti ulikosekana akazikwa hivyo hivyo.

Jumapili asubuhi wakawahi kwenda kumpaka mafuta waliyoshindwa kumpaka ijumaa ndio wakakuta tayari kashafufuka

Sasa hawa jamaa wanasema kama mungu aliheshimu hiyo siku akaitenga siku alipoumba dunia na mpaka akaiandikia amri enzi za musa na wakati ule wa kuokota mana hakushusha mana jumamosi, yesu nae akaja akaiheshimu mpaka kaburini.... inakuwaje wewe mwanadamu utafute ya kwako? Halafu unaendelea kusema unafuata yesu basi mfuate kweli kwa kila alichofanya na alichoagiza vinginevyo fata wanadamu waliobadilisha.

Ndio wasabato ni wakristo kabisa lakini huo msimamo wao unawafanya watofautiane na wakristo wengine wote
Aliyekudanganya Wasabato ni Wskristo ni nani..??

The Four Cults Religion on Earth
Seventh Day Adventist
MOrmon
Jehova Witness
Christian Scientist
 
Weweee mwanamke anamfata mwanaume!!ulisikia wapi mwanaume akabadili dini sababu ya mke xo kama wazaz hawataki waoe wenye mtt wao

Furaha;
we ni me au ke??? Mawazo yako mbona yako mbaaaali sana mwaka 47????? Ati mwanamke anamfuata mwanamme. Ka huyo mwanamke ana msimamo thabiti, utamfuata tuuuu. Kipenda roho hula nyama mbichiiiii mchana peupeee tena mbele ya kadamnasi.
Hapo ni wawili wamependana, sio wao na wazazi wao, sasa hilo la wazazi sijui linatoka wapi. Kwani wao ndo waliwashauri hao wazazi wawazae?? Wataenda kuishi na hao wazazi??
Ushauri ni huu:
Mnapendana? Angalieni yenyu basi. Msichana anunue marlboro, aweke humo nguo zake zoote, aondoke kwenda kwenye kituo cha bus, kijana naye vivyo hivyo, wakutane kituo cha bus, watokomee kusiko julikana. Wakautane na mchungaji wamwombe awafungie ndoa saa hiyo hiyo tangazo baadayeeee. Lakini wawe above 18.
Ndoa ni makubaliano kati ya wawili walio amua kuishi pamoja kwa kusudi la kuwa mtu mume na mkewe. Hayo mengine ni nyongeza zisizo na umuhimu. Ni sawa na video kwenye mazishi, ikikosekana kaburi lazima lifukiwe tu kwani marehemu kishawekwa humo.
 
Hii post haijapata msabato hata mmoja walau kurudisha kombora?...
I will try..

Yesu mwenyewe alikwenda sinagogi na akafundisha, by then ilikuwa jumamosi.

Alikufa siku ya maandalio ya sabato (ijumaa), akapelekwa kaburini jioni muda wa kuandaa maiti ulikosekana akazikwa hivyo hivyo.

Jumapili asubuhi wakawahi kwenda kumpaka mafuta waliyoshindwa kumpaka ijumaa ndio wakakuta tayari kashafufuka

Sasa hawa jamaa wanasema kama mungu aliheshimu hiyo siku akaitenga siku alipoumba dunia na mpaka akaiandikia amri enzi za musa na wakati ule wa kuokota mana hakushusha mana jumamosi, yesu nae akaja akaiheshimu mpaka kaburini.... inakuwaje wewe mwanadamu utafute ya kwako? Halafu unaendelea kusema unafuata yesu basi mfuate kweli kwa kila alichofanya na alichoagiza vinginevyo fata wanadamu waliobadilisha.

Ndio wasabato ni wakristo kabisa lakini huo msimamo wao unawafanya watofautiane na wakristo wengine wote


Naomba kufahamu jambo. Kalenda ziligunduliwa Lini? Na kabla ya kalenda kuwako Jumamosi ilijulikana vipi? Halafu, Jumamosi ni siku ya kwanza ya wiki au ya mwisho?
 
2 Wakorintho 6:14-15

14 Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza?
15 Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini?

Masuala ya imani japo wengine wanadhani si ya muhimu katika ndoa, lakini ukipuuzia usilalamike mbele ya safari. Usibadili dini kwa sababu tu nataka kuoa/olewa. Badili dini kwa kuelewa na kuamini hicho kilichokufanya ubadili.

Ndio maana Mungu akasema usifungiwe nira na wasioamini. Muktadha hapa ni kuwa wote muwe mnaamini kitu kimoja katika masuala ya dini.Kwa hiyo kama wewe ni RC oa RC, KKKT oa KKKT n.k. kwa sababu wote mna imani inayofanana. RC akioa KKKT hapo ni shida mtatofautiana tu mbele ya safari. RC au Muislam akio/olewa na SDA hapo ujue ni mtafaruku tu mbele ya safari. Mtakuja kugombana wakati wa malezi ya watoto. Lakini la Muhimu ndoa ni kuambatana, kuambatana kanisani na watoto kama famila ni kuweka msingi m zuri wa malezi. Baba au Mama unaenda kanisani peke yako then mna gombania watoto wawe dini ya nani.

Ukiamua kubadili dini uamue kwamba hutarudi kwenye dini yako ya zamani, ukioa kisha ukarudi ujue umeanzisha mgogoro usioisha katika ndoa na ndoa yaweza vunjika.
 
Wawasikilize wazazi tu , sasa hivi wanaweza wakaona wanapendana Sana hlf kwenye ndoa ikawa chenga tu.
Na wakiwasikiliza wazazi watapata baraka.
Kila mmoja atafute wa dhehebu lake tu, hamna namna nyingine hapo.
 
Naomba kufahamu jambo. Kalenda ziligunduliwa Lini? Na kabla ya kalenda kuwako Jumamosi ilijulikana vipi? Halafu, Jumamosi ni siku ya kwanza ya wiki au ya mwisho?

Sitaenda na kalenda labda mwanahistoria mzoefu alete maujuzi...
Nitaenda na mifano halisia tu ya bible na baadhi tu ya kawaida...
Kwanza neno jumamosi lisikuchanganye sana kwavile ni tafsiri kutoka lugha ya kiarabu likimaanisha siku ya kwanza ya juma which means alhamisi ni siku ya maandalio na ijumaa ni ndio yenyewe siku ya wenzetu.
Huu mfumo ni urithi rasmi wa wayahudi ambao wao mpaka leo wanautumia na walikuja nao wakitokea misri...
Hata leo hii dini ya kiyahudi ambao zamani walitambulika kwamba bado wanamsubiri masihi wao (siku hizi wamebaki na sheria zao lakini wanamtambua yesu), bado wangali endelea na jumamosi yao na hao ndio kielelezo kikuu kwako maana wao wana vitabu vyao vyenye sheria ya musa na wameendelea na utaratibu huo.

Kama siku zinakuchanganya we fuata yesu alifanya nini hutapata shida hata kidogo..

Tusiibe uzi wa watu, tuendelee kuchangia ndoa na tofauti za madhehebu na dini, nilijitosa kujibu kwa vile wasabato walishambuliwa sana humu uzini....
 
Aliyekudanganya Wasabato ni Wskristo ni nani..??

The Four Cults Religion on Earth
Seventh Day Adventist
MOrmon
Jehova Witness
Christian Scientist

Biblia ndio imenidanganya... nilidhani wakristo ni wale wanaomfuata kristo kumbe sivyo?
 
Wawasikilize wazazi tu , sasa hivi wanaweza wakaona wanapendana Sana hlf kwenye ndoa ikawa chenga tu.
Na wakiwasikiliza wazazi watapata baraka.
Kila mmoja atafute wa dhehebu lake tu, hamna namna nyingine hapo.

Kuna baraka myingi sana kwenye kuwasikiliza wazazi lakini kuna furaha tele kupata mwenza mnaependana kwa dhati bila kujali dini yake, dhehebu lake au kabila lake....
Hapo ndipo penye uchaguzi, ufuate baraka za wazazi pengine upate ndoa ndoano? Au uufuate moyo wako pengine utaishi kwa furaha?
Kwakuwa haya yote huwa hayajulikani mapema wakati wa kufanya maamuzi ndio unajaribu kutafakari vigezo na masharti yote ya uhusiano...
Kwamfano ukiona mtu anakulazimisha uhamie kwao ndio muoane sio wewe ulie radhi kumfuata kwa kuwa unampenda na hamtaki muende bomani, chunga sana hicho ni kiashiria kibaya kwamba penzi la kweli halihusiki bali kulazimishana na ipo siku kitanuka tu...

Vile vile ukiona wazazi wana choice zao very specific kwa mfano tunataka uolewe au uoe mtoto wa fulani.. hapo napo mapenzi ya kweli hamna ni maslahi tu na furaha ya wazazi inatafutiwa kupitia kwako...

Mkipendana kweli kweli na kwa dhati hakuna atakayevutia kwake kwani kila mmoja atakuwa rahisi kumfuata mwenzake kitakachobaki ni nyie wawili kuamua muende ipi kati ya hizo zilizopo...
tena mkiwa wajinga wa mapenzi kama mimi mnaweza kusema tujaribu zote kwa zamu kisha tuamue kubaki na moja baada ya kufanya kautafiti ketu...

Hapo hata lije greda linaloitwa ndugu, wazazi, jamii, marafiki, wote watagonga ukuta
 
2 Wakorintho 6:14-15

14 Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza?
15 Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini?

Masuala ya imani japo wengine wanadhani si ya muhimu katika ndoa, lakini ukipuuzia usilalamike mbele ya safari. Usibadili dini kwa sababu tu nataka kuoa/olewa. Badili dini kwa kuelewa na kuamini hicho kilichokufanya ubadili.

Ndio maana Mungu akasema usifungiwe nira na wasioamini. Muktadha hapa ni kuwa wote muwe mnaamini kitu kimoja katika masuala ya dini.Kwa hiyo kama wewe ni RC oa RC, KKKT oa KKKT n.k. kwa sababu wote mna imani inayofanana. RC akioa KKKT hapo ni shida mtatofautiana tu mbele ya safari. RC au Muislam akio/olewa na SDA hapo ujue ni mtafaruku tu mbele ya safari. Mtakuja kugombana wakati wa malezi ya watoto. Lakini la Muhimu ndoa ni kuambatana, kuambatana kanisani na watoto kama famila ni kuweka msingi m zuri wa malezi. Baba au Mama unaenda kanisani peke yako then mna gombania watoto wawe dini ya nani.

Ukiamua kubadili dini uamue kwamba hutarudi kwenye dini yako ya zamani, ukioa kisha ukarudi ujue umeanzisha mgogoro usioisha katika ndoa na ndoa yaweza vunjika.

Maelezo mazuri sana yenye ujumbe haswaa... tatizo ni pale ambapo nimependa nje ya dhehebu langu au nje ya dini yangu... niache niliyempenda nitafute wa dhehebu langu ambaye nitampenda kiasi maana moyo haujawahi kupenda wawili sawa kwa sawa hata siku moja?
Hivi hapo kutakuwa na furaha kwenye ndoa iwapo kila siku nawaza fulani angekuwa dhehebu langu tungekuwa mke na mume sio huyu nilienae?

Kwa mtazamo wangu hiyo pia ni dhambi ya udanganyifu maana umefunga ndoa na mwingine kumbe mapenzi yako kwa mwingine
 
Natamani kuona somo la mahusiano likifundishwa kwa vijana (pengine sekondari) lenye mtaala unaojumuisha pamoja na mengine.. mwanamke na hisia zake, mwanaume na matamanio yake, mwili wa mwanamke na mwanamke kwa ujumla wake, mahusiano ya ndoa na wazazi, dini, jamii, kazi, na kadhalika.

Pengine vijana wengi wangekuwa na ufahamu mkubwa juu ya wenzao na juu yao pia kabla hawajaingia kwenye mahusiano na ndoa...

Nimesahau na ukimwi pia iwe sehemu ya silabus
 
Heshima kwenu wakuu,

Nimeona nilete humu, nikiamini kuwa kuna watu wameona mengi. Mimi nina mdogo wangu, alipata mchumba yapata miezi tisa sasa, wote ni wakristo tofauti ni madhehebu.

Kwamaelezo yao wapendana na wanajiandaa kufunga ndoa. Tatiza lilijtokeza hawawezi sasa ni pale ambapo binti alipo lifikisha kwa wazazi wake kuwa amepata mchumba na kutaja dhehebu lake ikawa tatizo.

Wazazi wa binti wanamtaka mdogo wangu abadili dini lasivyo hakuna mke, mdogo wangu nae hataki, mchumba wake nea anawaogopa wazazi hivyo hadi saivi hawajajua muafaka japo wanawasiliana kama
kawada ila kila mmoja anapata kigugumizi afanyenini.

Kwa wenye uzoefu ama mawazo mmbadala hebu sadieni hapa kwa ushauri

Hapo tatizo maana kunauzi nlisoma eti kunadin zinatumia wanawake wao kuwaingiza wa kwenye hiyo dni/dhehebu sasa kama ndo hivyo .......... Sina ushaur....ila akaze tuu mwanamke ahamie din yenu
 
Kwanza swala kwamba mkristo Ni nani sio jambo la kupatiwa ufafanuzi na Wikipedia kama baadhi ya wenzetu wanavyodhani. In fact, some of scholars thinks that Seventh Day Adventistism is not Christianity but merely a sect. If we consider ourselves Christians, you have no right to say that we are not Christians but we have the right to prove why we say and hold that we are Christians.

I am a Christian, and not only a Christian, but I'm a Seventh Day Adventist Christian. Siamini katika kuoa binti yeyote Kwa sababu tu eti tunapendana. Biblia inasema jambo lolote lifanyike kwa utukufu wa Mungu. Tukumbuke kwamba ndoa ni muunganiko wa mke na mume walioamua kuishi pamoja katika kipindi chote cha maisha yao. Pia, ndoa inaathiri maisha yako ya sasa katika ulimwengu huu na ule ujao pia. Sasa nawezaje kufunga pingu za maisha na mtu ambaye haamini kile ninachokiamini? Mimi naamini katika kutunza sabato ya Mungu, nawezaje kuoa mke asiyeamini kama ninavyoamini? Naamini katika ubatizo wa maji mengi, nawezaje kufunga pingu za maisha na asiyeamini katika hili? Naamini kwamba wafu wakifa hawajui neno lolote, nawezaje kufunga pingu za maisha na mtu anayeamini kwamba mara tu watu wanapokufa wanakwenda peponi au jehenamu? Naamini kwamba tukio la kurudi kwa Yesu ni tukio dhahiri linaloonekana kwa macho, nawezaje kufunga pingu za maisha na anayeamini unyakuo wa siri? Biblia inauliza; Je, wawezaje kutembea wawili wasipokuwa wamepatana? Katika safari ya maisha ya ndoa lazima kupatana kuwepo, tena kuwe kupatana katika kila hali.


Upo mfano halisi katika kisa cha Samsoni. Soma kitabu cha Waamuzi 14:1-3, inasema....... "1. Samsoni akatelemkia Timna, akaona mwanamke huko Timna, mmojawapo wa binti za Wafilisti. 2. Kisha akapanda, akawaambia baba yake na mama yake, akasema, Nimemwona mwanamke huko Timna, mmojawapo wa binti za Wafilisti; basi mnipatie, nimwoe. 3. Ndipo baba yake na mama yake wakamwambia, Je! Hapana mwanamke hata mmoja katika ndugu zako, au katika jamaa zangu zote, hata uende kumwoa mwanamke kwa hawa Wafilisti wasiotahiriwa? Samsoni akamwambia baba yake; Mnipatie huyo, kwa maana ananipendeza sana".

Hapa utaona hekima ya vizazi vyote. Wazazi wa Samsoni walimtaka Samsoni aoe kutoka miongoni mwa watu wa kwao, wanaoamini kama alivyokuwa Samsoni. Samsoni hakuwasikiliza na mnajua kwamba aliishia kutobolewa macho.


Ilikuwa ni hekima ya Mungu kwamba ili kutunza usafi wa maadili lazima hata jamii ya watu wanaomwamini wasioane na wasioamini. Kumbukumbu la Torati 7:3-5, Yoshua 23:12.

Swala la imani katika kuoa hiwezi kuliepuka kama wewe ni mfuasi mwaminifu wa kile unachoamini
 
Back
Top Bottom