Mdogo wa mke wangu (binti) amenidharau na kunitukana mbele ya mke wangu

Utakua unaishi kwenye nyumba yao ww sio bure.
Wanaanzaje kukufharau kiasi hicho. waambie wakatafute mteja muuze mgawane alaf ona reaction yao.

Cha kufanya, hilo duka uza vitu tunza hela, hiyo nyumba kachujue mkopo benki alafu ije ipigwe mnada. Kua kichaa vitu uza alafu wote fujuza. Wakishaondoka kafungue duka upya, jenga nyumba upya na usioe tena.
 
Mtoa mada kuna upande hujauelezea, unaishi kwako au kwa mkeo? Mkeo ana mkwanja kukuzidi? kama ndio basi hii ni sababu why wanakupanda kichwani kama ni vinginevyo basi hujitambui au usharogwa, shtuka.

Mimi nina hasira ningekua nishafukuza mtu na kibano juu ila sasa kama wao ndio wanakulea inabidi utulie tu.
 
Mkuu nakupongeza sana kwa hekima hiyo ya kuzuia hasira, niliwahi piga dogo langu kwa hasira niliumia sana kuona akitoka damu mdomoni na puani.

Jipe muda tafakari namna bora ya kutatua huo mgogoro kwa win-win state.
 
Anasema mpe dada yake talaka, mgawane mlivyochuma.
Vijana wa siku hizi bana, wanawaza mali tuu.

Sent from my SM-A025F using JamiiForums mobile app
Inaonekana dada na mdogo ake wanaongea mengi juu ya Mangi(mume) hapo Mume ana chake- hiyo Ndoa ipo ICU hilo Duka la Vipodozi mke ameshaona mgodi na tayari ameshapiga picha kuwa jamaa (mume) haitajiki tena . Ushauri wangu .Mume afanye maujanja Duka lifirisike(Ahamishe mtaji na mali kwenye uwekezaji mpya bila wife kujua) Kisha amwache aanze upya!

Hapo anaishi at Death Row(kinachofuata kuuliwa au kuachwa bila mali) Mdogo wa Mkewe anongea kile kinachotoka kwenye Kinywa na akili ya dada ake! Shemeji ametumika kuleta ujumbe tu.
 
Hiyo biashara ya mkeo itakuponza upoteze familia. Jitahidi tafuta hela.
Lakini mdogo mtu kama hajaondoka basi wewe ni tatizo, wee ndionuondoke ukajifunze
 
Nahisi ndilo linalo fuatia kakaa
Pole kwa masahibu yanayokusibu.
Unaonesha wewe ni mtu mpole kupitiliza.

Pamoja na upole wako inabidi sasa uamke, hizo dalili walizoonesha mke na mdogo wake zinaweka uhai wako mashakani.
Mtimue huyo shemeji, na huyo mkeo mpe msimamo wako mpya utakaoutengeneza kuhuatia hili tukio.
 
Wakuu naomba ushauri.

Mimi ni mkazi wa Morogoro ninaishi kwenye nyumba yangu niliyotafuta pamoja na mke wangu. Baada ya wahitimu kumaliza chuo mwaka huu mke wangu aliniomba mdogo wake aje kuishi nasi pamoja.

Sasa baada ya kipindi kupita mke wangu ameonesha ukaribu sana na mdogo wake ikafika mpaka kumueleza mengi juu ya maisha yetu ndani.

Kisa
Jana nilienda dukan kwetu na mke wangu (duka la vipodozi), lengo kumfuata shemeji na kupiga hesabu na kufunga duka. Dakika chache mke wangu alipokea simu kutoka kwa baba yake mazazi akimuomba aje aishi nyumbani kwangu.

Walikubaliana wao yeye na baba yake mzazi akiwa na mdogo wake na hata akaamua kumtumia nauli bila ya mimi kuhusishwa chochote. Ikumbukwe yote haya yanafanyika dukani tukiwa wote watatu namaanisha mimi, mke wangu na shemeji. Baada ya hili zoezi kuisha ndipo mke wangu ananieleza kuwa "Baba atakuja kesho na nimeshamtumia na nauli"

Mi nikamjibu kwa njia ya ujumbe wa simu, "Unaniambia ama unanipa taarifa?" Baada ya hii kauli alinuna na kukasirika sana na kuamua kuongea Kikurya yeye na mdogo wake (mimi mchaga). Mimi hapo sielewi kitu ila nyuso zao ni kama wamefura kwa hasira.

Dada mtu aliamua kurudi nyumbani kwa pikipiki, mdogo mtu (shemeji) alibaki dukani na kufunga hesabu. Baada ya muda kidogo niliwasha gari na kuelekea nyumbani. Nilipofika nyumbani sasa nikamuuliza mke wangu kwanini umekasirika kwa ujumbe kama ule angali sijaandika tusi?

Ailinijibu we niache kwanza, ushamzika baba yako hivyo huna cha kupoteza. Mimi nikamwambia taswira kama hiyo unanijengea picha mbaya kwa mdogo wako, maana yanayoongeleka ni mengi sana hasa juu ya mimi na wewe.

Maana unayomueleza nduguyo huwaeleza hata watu wa karibu. Dah, baada ya kusema hivyo akampigia simu mdogo wake na kumwambia shemeji yako anasema wewe huwa una muongelea vibaya hapo dukani kwa watu wake wakaribu.

Alifunga duka na akarudi nyumbani spidi ya jeti na kunikuta sebulen nimekaa naperuzi JF. Kwanza alipofika tuu nyumbani aligonga mlango kwa nguvu sana kana kwamba kuna mtu ana tuvamia. Alipotimba sebulen akaanza kwa kusema ilikuwaje mkanizungumzia mimi na hao marafiki (majirani wa dukani) zako?

"Halafu shemeji unajua wewe ni mnafiki sana? Unadhani matendo yako kwa dada siyaoni humu ndani? Ujue shemeji wewe una roho mbaya sana, naishi na wewe kwa kukuvumilia sana?Nlisha kudharau sana.

He he..he! Nlibaki nashangaa sana, kwanza ni mtoto mdogo sana kwangu, ni wa mwaka 98. Mwisho akasema bhana eeh kama vipi andika talaka kwa mkeo mgawane mlivyo chuma kila mtu asepe zake (shemeji huyo)! Hata dada yake hakuwahi kutamka maneno kama haya asee.

Wakuu, mimi nimeamua asepe kwao ifikapo Jumatatu ya tarehe 17, October. Japo mke anakuwa kama anajiuliza sana haya maamuzi yangu.

Pia msaada tafadhali maana nina mawazo sana kuhusu huyu dogo mwenye Degree ya Biashara, halafu pia ndugu lakini sina namna.

Nawasilisha.
Hapo huna chako mzee andika talaka uanze upya, wameshapanga muda sana huyo shemeji anakupa tu dondoo ya maamuzi.

Ukiweza kimbia ukaanze maisha pengine upya wewe wa kiume. Utakuja kufanya vitu ambavyo hukutegemea maishani, kimbia au toa talaka
 
Napita apo moro mda si mrefu, niko na DAF XF, cabin inatutosha watu wawili, shemeji yako ntaondoka nae free. Nampa lift mpaka Tinde. Pale atachagua aende kwa miguu ama apande Punda Mpaka Tarime. Fukuza hiyo Funza na nauli usimpe gari ya free ipo Mkuu. Kama uko serious, saa kumi njoo pale Camel msamvu, niletee hiyo ndama nikusafirishie. Ntakuwepo apo mpaka saa kumi jioni.


Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
Tatizo wanaume wa kichaga mnakuwaga wapole sana majumbani. Hapa nilikuwa naanzisha tifu sio la kawaida, mdogo mtu angerudi kwao katika hali mbaya na asingetamani tena kurudi hapo. Kama kuna consequence za kisheria ningezi face kuliko kudhalilishwa kwangu
 
Back
Top Bottom