Mdogo wa Gwajima amtetea Makonda, asema Josephat apuuzwe vita ya madawa ya kulevya

Casuist

JF-Expert Member
Jul 23, 2014
1,189
2,970
Kwa ufupi

Mdogo wake na mchungaji Josephat Gwajima wa Kanisa la ufufuo na uzima, amesema mchungaji huyo anatakiwa aache kutumika na kuhoji kuna nani nyuma yake. Amedai mchungaji hawezi kujiingiza kwenye malumbano na mipasho ya kidunia.

Ameendelea kusema vyeti vya Makonda viachiwe mamlaka husika kuchunguza kwani kumuandama sana inaweza kusababisha watu wengine siku zijazo kuogopa kujihusisha kupambana na madawa ya kulevya.

Amesema serikali imemlea sana Gwajima na waziri wa mambo ya ndani anatakiwa amuangalie na ana tuhuma nyingi ikiwemo kadai angemfufua baba wa watoto yatima ilhali yeye anajua hajawahi kufufua hata panya.

Amedai tabia ya kubeza shughuli za maendeleo zinazofanywa na serikali sio tabia njema na haiisadii nchi. Amesema anajua vita ya madawa ya kulevya ni ngumu na hugharimu maisha, atoa wito kwa watanzania wote kuunga mkoni juhudi za kutokomeza madawa ya kulevya hasa Dar es Salaam.

Amesema anafahamu yeyote atakayejitokeza kuunga mkono juhudi za kupambana na madawa ya kulevya ataandamwa tu na hivyo kwa namna ya pekee anamshukuru mkuu wa mkoa wa Dar Paulo Makonda na atakumbukwa na vizazi vyote kwa kujitoa Muhanga kusimamia vita ya madawa ya kulevya Dar es Salaam na kila mmoja amefahamu athari za madawa ya kulevya hadi kwa watoto wadogo ndio maana anaandamwa kila kona na kuhoji walikuwa wapi kuyasema yote kabla ya vita ya madawa ya kulevya.

 
Huyu naye ana matatizo; yaani Gwajima atuhumiwe hadharani kuwa drug-dealer halafu anyamaze tu? How? Very very wrong approach ya kujisafisha na tuhuma za wizi wa vyeti ... Tuhuma za kugushi vyeti zinasafishwa kwa kuweka vyeti hadharani na sio kwa kum-attack Gwajima personally.
 
Hilo tamko limeandaliwa wapi na nani? Je, hoja ya msingi ya forgery ni kweli au sio kweli? Hayo mengine wala watanzania hawahitaji kuyajua. Nguvu zooote anazotumia hapo si angeweka vyeti mezani akammaliza kabisa Gwajima forever and ever? Vinginevyo, this is another justification ya tuhuma za wizi wa vyeti. Yaani ndio anazidi kummaliza kabisa Bashite! Ha ha ha; kuna watu wapumbavu sijawahi kufikiria.
 
Kama Huyo John si Muuza madawa kweli
asinge shupalia ujinga huo.
Huyu kajificha nyuma ya uchungaji kuuza madawa,
Wengine wamejificha nyuma ya Uenyekiti wa chama kuendesha Biashara mbaya!!
Hawata penya
waendelee kuwatumia hao mamluki
lakini hawata penya kamwe
Sasa mimi hapa huwa siwaelewi. Kama wanauza si wakamatwe? Au kutangaza ndio vita vyenyewe? Na kama huyo Daudi si kolomije kweli, si angeshaonesha vyeti?
 
Sisi watz tumechoka na ujinga wenu hoja ya msingi hapa ni.madawa ya kulevya ni siyo ujinga wenu .
Sawa! Hakuna anayepinga vita dhidi ya madawa ya kulevya; tena tunaiunga mkono sana Tume ya Kamishna Siang'a kwa jukumu zito na muhimu. Hata hivyo, vita dhidi ya madawa haihalalishi forgery za aina yoyote. Vyeti viwekwe mezani acheni blah blah.
 
Dah! huyu ndiye ndugu yake anayemfahamu in and out " hajawaki kufufua hata panya" ila waliokutana naye bongo ndio wanajifanya kumuamini. Kamrarua ile mbaya
Wote tunajua kuwa hajawahi kumfufua hata panya, lakini ukweli unabaki kuwa HAYO HAYATUHUSU. Movie inayotuhusu ni hii ya kutaka kumfufua David Alubeto Tarantini Bashkoooooolite.

Huyo anatafuta umaarufu tu, hana lolote.
 
Back
Top Bottom