Mdogo mdogo Machinga waanza kujenga mabanda ya mbao Msimbazi street.

Baada ya kufanikiwa kuingiza bidhaa zao ndani kabisa ya Stendi mpya , sasa katika kile kinachojulikana kama MATUNDA YA UHURU WA NCHI YAO , wameamua kusimika mabanda ya mbao yaliyoezekwa na miamvuli mikubwa.

Mtoa taarifa amedokeza kwamba , baada ya miezi kadhaa ijayo wataanza kuezeka kwa bati ili kujihami na kipindi kijacho cha mvua .

Mungu ibariki Tanzania .
So sad wadau hapana tofauti sana na soko la buguruni, maana kwa sasa sio tena nguo na viatu ni mwendo wa nyanya, vitunguu, karoti, banana mbivu kwa mbichi, matikiti, mafenesi mananasi yaani kila aina ya bidhaa inawekwa road, hii ni hatari kwa watumiaji maana yale maji yanayotiririka c salama aiseeeeeeeeeeee...#@#
 
Tanzania ya viwanda ipo njiani. Wote tunawahamisha viwandani. Hii hali ni ya mpito kuelekea uchumi wa viwanda God knows when.
 
Vibanda vya mwendo kasi navyo wavitumie.
Nadhani wasipoangalia muda si mrefu hayo mabanda yaliyojengwa kwa ajili ya mabasi ya mwendo kasi nayo yataingiliwa na wamachinga na kutumika kuuzia bidhaa zao kwa abiria wanaosubiri kupanda hayo mabasi na wale wanaoshuka.
 
Msimbazi wamejaa wauza maji na wanakaa hapo hapo kituo cha mwendokasi juzi nusu nimwage maji na juice zao
 
So sad wadau hapana tofauti sana na soko la buguruni, maana kwa sasa sio tena nguo na viatu ni mwendo wa nyanya, vitunguu, karoti, banana mbivu kwa mbichi, matikiti, mafenesi mananasi yaani kila aina ya bidhaa inawekwa road, hii ni hatari kwa watumiaji maana yale maji yanayotiririka c salama aiseeeeeeeeeeee...#@#
Buguruni ndio eneo la mwanzo kabisa kupata kipindupindu kila mlipuko unapotokea .
 
Hebu mtu mmoja tuu na aniambie tamko alilowahi kutamka huyu mzee ambalo halijaleta ukakasi na akaonekana mbunifu? Moja tuu ili Leo nivae shati la kijani
We si useme tu kama hutaki kuvaa hilo shati bhana , tutalipata wapi hilo tamko aisee ?
 
Inasikitisha sana.....

Tanzania ni chafu inanuka kila kona....Dar haijawahi kuwa safi hata siku moja
 
Back
Top Bottom