Mdogo mdogo Machinga waanza kujenga mabanda ya mbao Msimbazi street.

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
125,690
239,251
Baada ya kufanikiwa kuingiza bidhaa zao ndani kabisa ya Stendi mpya , sasa katika kile kinachojulikana kama MATUNDA YA UHURU WA NCHI YAO , wameamua kusimika mabanda ya mbao yaliyoezekwa na miamvuli mikubwa.

Mtoa taarifa amedokeza kwamba , baada ya miezi kadhaa ijayo wataanza kuezeka kwa bati ili kujihami na kipindi kijacho cha mvua .

Mungu ibariki Tanzania .
 
baada ya hapo tutaanza kuona wanainua maghorofa
MUNGU WABARIKI MATCHING-GUYS
 
Siku hizi hakuna tena ustarabu, barabara zote za wapita kwa miguu ni biashara: kkoo, ubungo nk...dah maamuzi haya !!
 
Wanauza hata ktk barabara mwendokasi, wakiliona basi linakuja wanandoa, likipita wanatandika...dah uhorela juu!!
 
Ifike mahali hao wanaoitwa wamachinga wajiongeze..kwa hiyo wanafurahia kutandaza bidhaa kwenye njia za waenda kwa miguu ili wapate fedha...nadhani Tanzania na viongozi wake ni nchi ya kipekee duniani.
 
hayo ndio matokeo ya kutoa maamuzi kwa msukumo wa kisiasa ili kukipatia kura nyingi chama chetu ktk uchaguzi wa 2020.

nilikatiza Leo mitaa ya barabara ya Uhuru jirani na kituo kikuu cha BRT,niliyojionea toka kwa wamachinga sina la kusema.

wanamwaga bidhaa zao mpaka barabarani na wanajiamini kweli kweli,ole wako ukanyage hats kwa bahati mbaya,sijui wametoa wapi jauri ile.
 
Back
Top Bottom