Ujenzi bora wa mabanda ya kufugia kuku wa kisasa na kienyeji

akohi

JF-Expert Member
Jul 13, 2012
788
524
Naombeni munisaidie ukubwa na namna ya kujenga banda zuri la kisasa ambalo linaweza kkufuga aina yoyote ya kuku (kisasa au kienyeji).

Nataraji kuanza na kuku wa kienyeji. Je, nianze na kuku wakubwa au vifaranga? Wangapi?

Ntashukuru kwa ushauri wenu maana naona kweli JF ni mkonbozi na nimeamua kuanza ufugaji mara baada ya kupitia nyuzi mbali mbali zenye kuhamasisha, hongereni kwa nyote mulioanzisha mada na maelezo jinsi faida inavyopatikana.


Majibu kutoka kwa wanaJF

Kwa kuku wa kienyeji.....ufugaji mzuri ni wa nusu huria kwa maana ya usiku wanalala bandani mchana nje.
Kwa kuanzia vyumba vitatu: 1: mita 3 (kuku wanaoanzia miezi 2 na kuendelea) 2: mita 2 (kwa mitetea wanaoatamia) 3: mita 2 (kwa ajili ya vifaranga ambao watahifadhiwa kwa kutumia joto, liwe la umeme, maji ya moto kwenye dumu n.k).

Linatakiwa kuwa na madirisha mbele yenye ukubwa kama wa futi 2 kwa kila chumba na mlango unaokuwezesha kuingia bila vikwazo..............Urefu wa banda kama mita 3 tu zinatosha kwa maana kwamba unaweza kuingia na kufanya usafi bila tatizo.

Kumbuka kuku ni ndege kwa hiyo unaweza kupitisha fito pembeni ili wanaotaka kulala wamening'inia wasipate shida. Chini weka pumba za mpunga au maranda ya mbao kuabsorb kinyesi ili kupunguza bakteria.

Kwa sababu ni wa kienyeji nje ya banda unazungushia uwa wa waya ili wasitoke lakini wapate nafasi ya kufanya mazoezi, na kula. Banda la aina hii lina uwezowa kuchukua kuku 300.

==========

MABANDA BORA YA KUKU:

Ujenzi wa mabanda bora ya kuku ni miongoni mwa mambo ya msingi kabisa katika ufugaji bora wa kuku wawe ni wa asili au wale walioboreshwa. Hata hivyo si kila mtindo wa ujenzi unafaa, kwahiyo ujenzi huo ni lazima uzingatie mahitaji halisi ili ufugaji huo uweze kutoa matokeo bora yanayotarajiwa na mfugaji.


Mambo muhimu katika ujenzi wa banda la kuku ni;
1. Liingize hewa safi wakati wote.
2. Liwe kavu daima.
3. Liwe nafasi ya kutosha.
4. Liwe la gharama nafuu lakini la kudumu.
5. Lizuie kuingia wanyama na wadudu hatari kwa kuku.
6. Liwe na nafasi ya kuweka vyombo vya chakula na maji.
7. Lizuie upepo wakati wa baridi kali.

View attachment 185801
Mh.Pinda akitembelea banda la kisasa la kuku

HEWA NA MWANGA:

Hewa ni muhimu kwa kila kiumbe, hivyo banda la kuku ni lazima liingize hewa safi na kutoa ile chafu na liweze kuingiza mwanga wa kutosha.

1. Kwa kifupi ni kwamba madirisha ya banda ni lazima yawe makubwa na ya kutosha ili yaingize hewa safi na kutoa ile chafu.

2. Ni vema madirisha haya yawe juu kiasi cha meta moja (1) kutoka chini ili hewa ipite juu ya vichwa vya kuku.

3. Hewa safi siyo upepo, hivyo jaribu kuzuia upepo mkali kuingia ndani ya banda la kuku ama sivyo kuku wataugua ugonjwa wa mafua na niumonia na vifaranga vinaweza kufa kwa ugonjwa wa baridi.

4. Jenga Banda lako kwa kukinga upepo unakotokea na kupanda miti kuzunguka banda hilo la kuku ili kupunguza kasi ya upepo na kuweka kivuli dhidi ya jua kali na joto.

UKAVU NA USAFI WA NDANI:


Kwa vile kuku si ndege wa majini kama bata , ni jambo la busara kuhakikisha kuwa mahali anapoishi hapana unyevunyevu.

1. Banda la kuku lijengwe mahali palipoinuka ili kuzuia maji ya mvua yasiingie.

2. Wajengee kuku uchaga wa kulalia kwa kuweka viguzo vyenye urefu wa meta moja na kutandika miti juu yake ili usiku walale hapo, kuliko kuwalaza ardhini au sakafuni.

3. Ukavu wa banda ni muhimu sana hasa kwa vifaranga na kuku wanaotaga. Ndani ya banda lenye unyevu mayai kuchafuka sana hata wakati mwingine huoza kwa urahisi na jitihada zako zitakuwa ni bure.

4. Sakafu ya banda ni vizuri ikawa ya zege lakini kutokana na uhaba wa fedha sakafu inaweza kutengenezwa kwa mabanzi (mabanda yaliyoinuliwa) au udongo mgumu na au mchanga ambao utafunikwa kwa mabaki ya taka za mpunga na yale ya mbao.

5. Ili kuepuka unyevunyevu ni vyema eneo/mahali pla kujenga banda pawe pameinuka na penye kupitisha hewa ya kutosha.

View attachment 185802
Banda la kuku

PAA LA BANDA:


Paa la banda liwe madhubuti ili kuzuia maji ya mvua kuingia hasa wakati wa masika. Sakafu ya banda iwe juu zaidi ya usawa wa nje. Paa linaweza kuezekwa kwa mabaki ya vipande vya bati , madebe na kama ikishindikana tumia nyasi zinazofaa kwa ajili ya kuezeka nyumba katika eneo hilo.

NAFASI YA KUFANYA KAZI:

Banda la kuku lisiwe na nguzo au mbao nyingi sana ndani kiasi cha kumfanya mhudumiaji wa kuku ashindwe kufanya kazi zake. Hali hiyo itamfanya apoteze muda mwingi katika kuzizunguka nguzo hizo, hasa wakati wa kuokota mayai au kufanya usafi.

VIFAA:


Unapotaka kujenga banda la kuku kwanza kabisa tayarisha vifaa vinavyotakiwa. Vitu kama miti au nyasi, nyavu au fito, misumari au kamba ni muhimu kuviandaa mapema.

Pili ni lazima uwe na plani/ramani kamili ya banda hilo. Kwa wastani kila kuku anahitaji nafasi ya Meta za eneo la 0.11 hadi 0.22 (futi 1 hadi 2 za eneo.) kutegemeana na umri wa kuku.

UJENZI RAHISI:

Kuku wafugwao hatimaye ni lazima wafidie gharama za Ujenzi wa mabanda na chakula. Gharama zikiwa kubwa sana huenda ukaifanya shughuli ya ufugaji isiwe na faida hata kidogo hali hiyo itamfanya mfugaji aone ufugaji hauna maana yoyote kwake. Lakini ukijenga banda lako kwa kutumia vifaa vinavyopatikana kwa urahisi utaongeza faida zaidi kwakuwa umepunguza gharama za uendeshaji wa mradi.

VIPIMO:


Banda la kuku linatakiwa liwe na Meta 15 hadi meta 22 za eneo yaani Meta 3 hadi 4.5 za upana kwa meta 5 za urefu. Banda hili linaweza kutunza kuku 100 wakubwa kwa wakati mmoja.

HITIMISHO;


· Ujenzi wa mabanda unasisitizwa katika kuboresha ufugaji wa kuku wa asili ili;

· Kuongeza uzalishaji na kupunguza vifo vya vifaranga kwa majanga mbalimbali kama vicheche ,mwewe, mapaka, mbwa na wizi wa kuku wanaozurura holela.

· Vile vile inatarajiwa kwamba kuku wanaozuiliwa kwenye banda na kuwekewa chakula mchanganyiko wataongeza uzalishaji kwa kiasi kikubwa.
 
Kabanda kangu kako hivi, ninafuga kuku 50

mfano banda.jpg


Ujenzi wa viota vya kuku wa kienyeji

Kuku anapotagia porini, mayai huliwa na wanyama kama vile nyoka na wengineo. Kuku pia anaweza kudhuriwa na wanyama hao na wakati mwingine kuibwa.

Viota ni mahali ambapo kuku hutaga mayai, kuhatamia na kuangua vifaranga. Hii inamaanisha kuwa viota ni sehemu muhimu sana ya kuzingatia ili kuweza kupata mayai mengi yaliyo salama pamoja na vifaranga.


Aina za viota


Kuna makundi mawili ya viota vinavyotumiwa na kuku pamoja na ndege wengine wafugwao.


• Kiota kilicho tengenezwa na kuku mwenyewe

Kiota+1.tif


Hii ni aina ya viota ambavyo kuku huchagua mahali pa kutaga na kuhifadhi mayai. Inaweza kuwa mahali popote ambapo kuku ataona mayai hayataweza kudhurika au kuonekana. Kwa mfano, vichakani, stoo au kona yenye giza. Njia hii si nzuri kwani husababisha upotevu wa kuku na uharibifu wa mayai.


Kwa kutagia stoo au sehemu iliyojificha ya ndani, japokua ni sehemu salama ambayo haiwezi kufikiwa kirahisi na wezi au wanyama, mayai yanaweza kuharibika. Kuku akitaga sakafuni, sehemu yenye nailoni au magunia mayai yanaweza kuharibiwa na unyevu. Mayai hayo si mazuri kwa kutotoleshea. Itabidi mfugaji ayatumie au ayauze kwa ajili ya chakula.


Katika ufugaji wa ndani, kuku hutaga mayai sehemu yoyote hasa kipindi ambacho kuku huanza kutaga. Hii husababisha mfugaji kuyakanyaga mayai kwa bahati mbaya au kuku wenyewe kula mayai hayo na kupunguza uzalishaji wa mayai.


• Kiota kilicho andaliwa na mfugaji
Kiota+2.jpg


Kuku wanapotengenezewe viota vizuri huhatamia kwa utulivu kuongeza uzalishaji
Hii ni aina ya viota vilivyo andaliwa kiustadi na kuwekwa mahali stahiki kwa kumrahisishia kuku sehemu ya kutagia. Viota hivi huwekwa ndani ya banda au sehemu nyingine iliyoandaliwa. Viota vya aina hii huandaliwa kwa kuzingatia idadi ya kuku wanaotarajiwa kutaga, pamoja na upatikanaji wa vifaa vya kutengeneza viota.


Mahitaji


Unaweza kutumia vifaa kama vile boksi la karatasi, mbao, nyasi, nguo aina ya pamba (isiwe ya tetroni), matofari na maranda. Boksi, tofali, na mbao husaidia kutengeneza umbo na ukubwa wa kiota. Nyasi maranda na nguo (viwe vikavu) husaidia katika uhifadhi wa mayai yasiharibiwe na unyevu, pia ni mazuri kipindi cha kuhatamia kwani hutunza joto.


Ukubwa wa kiota unatakiwa uwe ni wa kumwezesha kuku kuenea na kujigeuza. Hii ina maana kuwa unatakiwa uwe wastani wa sentimita 35 upana sentimita 35 na urefu sentimita 35.


Namna ya kupanga viota kwenye banda


Ili kuwa na ufanisi mzuri, inabidi idadi ya viota kwenye banda iwe robo tatu ya matetea yaliyofikia umri wa kutaga. Hii huondoa msongamano wa kutaga katika kiota kimoja. Kwa mfugaji mwenye kuku wengi inampasa kuchagua vifaa ambavyo atajengea viota vinavyoweza kutumia eneo dogo na huku akipata viota vingi.


Kwa kuku wanaohatamia, inabidi watengewe chumba chao ili kuzuia uchanganyaji wa mayai. Kila sehemu katika banda si nzuri kuweka viota. Hivyo, katika uchaguzi inakupasa uzingatie mambo yafuatayo:
• Viota visiwe karibu au chini ya kichanja cha kupumzikia, vyombo vya chakula na maji.
• Kiota kisiwe sehemu ambayo mfugaji atakua anapitapita. Mfano, karibu na mlango au dirisha.
• Kiota kisiwe mkabala na sehemu ambayo upepo mkali au mwanga utakua unaingia.


Wakati wa ujenzi wa banda unaweza kujenga vyumba viwili ambavyo kimoja kikubwa utatenga sehemu ya chakula, maji na sehemu ya kupumnzika.


Chumba cha pili utatengeneza viota tu ili kuku anayetaka kutaga aende huko. Kwa kufanya hivyo, kuku wachache watakua wakienda chumba hicho, na usumbufu kwa kuku wanaotaga utakuwa mdogo.
Kulingana na kiasi cha nafasi, unaweza kujenga viota mwisho wa banda na vyombo vya chakula na maji upande wa mbele karibu na mlango. Hii itasaidia kuku kushinda sehemu yenye chakula na maji hivyo kuepusha usumbufu kwenye viota.


Kuku wanaohatamia


Viota vya kuku wanaohatamia inabidi viwe sehemu tofauti na viota ambavyo kuku wanatagia mayai kila siku. Hii itasaidia kuzuia uchanganyaji wa mayai yaliyoanza kuhatamiwa na mapya. Viota hivyo viandaliwe vizuri kwani hukaa na mayai kwa muda mrefu. Ni vema kuwatenga kuku katika chumba chao ambapo watapatiwa maji na chakula.

Umuhimu wa viota
Kiota+3.jpg


• Kwa kuwa na viota vya kutosha itapunguza usumbufu wa kuingia kukusanya mayai kwa mfugaji.
• Njia mojawapo ya kuzuia kuku kula mayai.
• Upotevu wa kuku na mayai utapungua.
• Utapata mayai bora kwa ajili ya kutotolesha.
• Kupunguza mayai kupasuka, pia mayai kuwa safi.

• Kuku kuwa huru wakati wa kutaga au kuhatamia.

Credit: Sekta ya mifugo Tanzania

 
Jamani hako kabanda kazuri sana kwa kuku wa kienyeji wa zero grazing yaani wanalala usiku asubuhi unawafungulia si ndio?
Kuku wanaofugwa ndani banda inabidi liwe na madirisha makubwa na yanayotizamana ili kuwezesha hewa kutembea, pia upande wa jua kali yaani magharibi uwe mdogo kuliko upande usiopigwa jua ili wasiadhiriwe na jua kali kiasi kikubwa
mtu kama anataka mfano wa banda google kuna mitandao inayoonyesha mfano wa mabanda ya kuku.
 
Nashukuru wakubwa, walau sasa napicha ya nini kifanyike, nadisign na kujenga then ntalipiga picha mu comment...Asanteni
 
Asante kwa kuomba msaada wa banda la kuku. Majibu yatasaidia wengi maana ufugaji wa kuku uwe hob kwa familia maana nyama nyekundu kwa gauti na upotevu wa madini ya zink so cancer nyingi kwa vibofu. Tuhamasike tufuge kuku wa afya zetu.
 
literature nyingi nilizopitia wana-recommend kuku 18 per square meter (kwa kuku wadogo wa hadi wiki 4) na wakubwa (wiki 4-8) kuku 9 per square meter.umri zaidi ya wiki 8 ni kuku 4 kwa square meter. ila wafugaji wanaweza kutupa experience zao, kama safari -ni safari anaweza kutupa dimensions za hilo banda lake zuri lenye kuku 500
 
literature nyingi nilizopitia wana-recommend kuku 18 per square meter (kwa kuku wadogo wa hadi wiki 4) na wakubwa (wiki 4-8) kuku 9 per square meter.umri zaidi ya wiki 8 ni kuku 4 kwa square meter. ila wafugaji wanaweza kutupa experience zao, kama safari -ni safari anaweza kutupa dimensions za hilo banda lake zuri lenye kuku 500

layers or broiler au wa kienyeji
 
Wekeni mtusaidie nasi tunataka kuingia kwa hiyo biashara ya ufugaji, usihofu competition....Tz we are very far from satisfying the chicken demand/market..
 
Nawashukuru wote walitoa mchango na kuonyesha mfano wa mabanda pia aliye uliza swali.Nami nimepata picha ya kabanda kangu.
 
Mnaouliza ukubwa wa banda ninavyojua kuku wakubwa wa mayai 7-9 kwa square metre moja na wa nyama 9-10 kwa square metre moja
ina maana kuku mia tano ni banda (500kuku/10)= 50m2 approx 5mx10m au kipimo chochote upate 50m2 hii kwa broiler
layers kwa sababu ya viota na pia sababu wataishi muda mrefu wanahitaji space zaidi kuweza kufanya mazoezi (hawahitaji uzito mkubwa)
kuku 500/9 = 55.5m2 approx 5mx11m
ila ngoja wengine waje watoe ushauri zaidi
space pia inategemea mzunguko wa hewa, kama huna space au umebanwa usijaze kuku ili kuepuka vifo kwa magonjwa yanayoambukizwa kwa hewa. All the best
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom