kat.ph
JF-Expert Member
- Dec 19, 2013
- 2,222
- 1,676
MDOGO-MDOGO, DIAMOND ATABWIA UNGA
PESA ina kelele mno! Ukiwa na fedha, unaweza kujitahidi kujificha lakini ikawa vigumu. Unawezaje kujificha wakati noti zimetuna kwenye waleti? Ubavu upi unao wa kujionesha maskini wakati benki unawapa wakati mgumu wahesabu pesa zako kutokana na wingi wake?
Inakuwaje tena Chibu Dangote, mwite Diamond Platnumz ambaye mama yake humwita Nasibu, ndiyo, anaitwa Nasibu Abdul Juma, ajioneshe fukara wakati fedha anazo? Shoo, mauzo ya miito ya simu, mikataba ya matangazo na kadhalika. Dogo pesa ipo!
Wakati mwingine mtu ukiwa na fedha unaweza kujiona kila kitu umemaliza, kwa hiyo ukataka kufanya yale ambayo hayatarajiwi. Ni kama msela fulani alifanya starehe zote akaona amemaliza, yaani hajaacha kitu, akajiuliza nini ambacho hajafanya?
Jibu likamjia kichwani kuwa hajawahi kufanya mapenzi na mwanaume mwenzake. Pesa anayo, akasema hilo lazima alitekeleze. Akaanza kushughulika na wanaume wenzake. Kushughulika kwa maana ya kuwashughulikia.
Wanawake wote aliokuwa nao aliwafukuza, maana aliona hawana maana tena. Alishawatumia kiasi cha kutosha, akaona hawana jipya la kumuongezea. Wafupi, warefu, kimo cha kati. Wanene, wembamba na wa kati. Wazungu, Waarabu, Wabantu. Wasomali, jamii ya Kagame. Akaona hawana jipya tena.
Hivyo basi, baada ya kujikita kwenye mapenzi na wanaume wenzake, akaona huo ndiyo mpango mzuri. Wapenzi wake wakawa wanaume. Tena akawa anajisifu na kusikia raha. Bila wasiwasi akawa anajigamba: “Unakuwa na fedha halafu mapenzi yako unafanya na wanawake? Sasa tofauti yako na maskini ipo wapi?”
Akawa anahoji: “Ukisoma shule ya msingi, ukimaliza unakwenda sekondari, sasa inakuwaje tena unang’ang’ania shule ya msingi kila siku? Wewe na wanawake kila siku, badili, angalau utumie na wanaume. Kidume hasa ni yule ambaye anamwita mwanaume mwenzake baby.”
Dunia na laana zake, tajiri huyo mfanya starehe za kila aina akawa anawapata wanaume kwa mahitaji yake. Aliendelea na mchezo wake huku akijiaminisha kuwa huo ndiyo ukidume. Na kweli, wapo ambao walimuona ni mjanja sana kwa matendo yake.
Ambacho hakujua ni kuwa baada ya sekondari kuna chuo, kwa maana safari moja huanzisha nyingine. Tajiri huyo baada ya kuwafanya wanaume ndiyo wake zake, baadaye alianza kuhisi hao wanaume wanafaidi, maana nao wanapenda mchezo huo.
“Mbona na wenyewe hawajisikii vibaya? Tena wanafurahia mchezo wenyewe. Itakuwa wanafaidi kuliko mimi ambaye nawatumia,” aliwaza na kujiuliza. Tajiri akawa anashawishika kuamini kuwa mtu kuwa shoga anafaidi zaidi kuliko mwanaume.
Akawaza tena: “Mbona hii starehe ya kuwatumia wanaume wenzangu na yenyewe imenichosha? Sioni tena jipya, kwa hiyo kinachotakiwa hata na mimi nipate mwanaume nionje ladha ambayo shoga huipata kwa mwanaume wake.”
Tajiri akaamua kutafuta mwanaume ambaye kwake atakuwa mume, siyo mke tena. Akafanya majaribio, akajaribu tena na tena, kutahamaki akageuka kuwa shoga, tena shoga aliyekubuhi. Tajiri akawa anachonga nyusi na kuvaa vikuku.
Tajiri akaanza kuremba sauti. Tajiri akaanza kupigilia fasheni za kike. Mungu wangu, kutahamaki tajiri akawa anapigana na wanawake kugombea wanaume. Maisha ya tajiri yakabadilika kutoka mtu wa starehe, mkali wa wanawake na mwenye kuoa wanaume hadi mume shoga wa kuolewa. Naam, tajiri akaolewa!
Haitokei kwake tu, wengi yaliwafika. Starehe za kujaribujaribu mara nyingi huwa hazina mpaka wala kikomo, safari moja inaanzisha nyingine. Alionja sigara, akaona kwani bangi ina ladha gani? Baadaye bangi akasema haina nguvu, ngoja tu ajipigilie unga. Alipojikita kwenye matumizi ya unga, akageuka teja wa kutupwa. Maisha hayapendi kujaribujaribu kila kitu.
Ukijaribu unga unakwenda kuwa teja. Ni kama tajiri yule aliyeonja ladha aipatayo mwanaume shoga, mwisho akaolewa, akawa anampikia mume wake, anamkunia nazi, na chakula akizidisha chumvi anaulizwa na mumewe kwa nini anashindwa kupika vizuri? Halafu mume anamtishia kuwa atakwenda kwa wengine wenye kujua kupika. Usipende kujaribu.
Somo la kujaribujaribu liende kwa Diamond. Mtindo wake wa maisha unabadilika kwa kasi mno. Labda ni kwa sababu Marekani anakwenda mara kwa mara. Kuna kipindi tulimshuhudia akiwa amebandika kipini puani. Mshtuko ukaibuka, kipini tena!
Katika wimbo, Muziki Gani ambao ameshirikishwa na Nay Wamitego, Diamond mwenyewe anawashangaa wanamuziki wa Hip Hop: “Hata mimi mengi nayajua ila wewe mtemi utaanzisha utata, mchezo wenu kutoboa pua bora ninyamaze usinipige mbata.”
Natambua kuwa kile kipini alibandika, hakutoboa pua, ila tofauti ni nini. Anayetoboa lengo lake ni kuvaa kipini kama ilivyo yeye anavyobandika. Diamond anataka kuwa kama yule tajiri, amejipamba, sasa anaamua kuvaa na vipini puani.
Dunia inakwenda kwa kasi mno! Diamond wa leo ametandaza dhahabu mdomoni. Meno yake sasa hivi utadhani ya Lil Wayne. Shida kubwa ni kwamba hata kuongea siku hizi anapata tabu. Mdomo wa Diamond umekuwa mzito.
Akiwa anazungumza utafikiri ana mapengo ya chini kwa jinsi anavyopata wakati mgumu. Ndipo alipofikia, Umarekani unamtawala. Siku zijazo tunaweza kuona mengi zaidi yanajitokeza kwa bwa’mdogo huyo aliyetokea Tandale na kufanya matukio makubwa ya kimuziki barani Afrika.
Nachukua fursa hii kumkumbusha Diamond kutambua ustaa siyo mpaka aonekane Mmarekani. Mbona alikuwa hana kipini puani na aling’ara Afrika? Mbona hakuwa na dhahabu mdomo na alimpata mwanamke wake cheupe wa Kiganda, Zari The Boss Lady?
Athari kubwa ya kuigaiga ambayo Diamond anaenda nayo, ipo siku ataambiwa kuwa akina Lil Wayne na Chris Brown wanakuwa vichaa walivyo kwa sababu huwa wanaonja unga, naye itabidi aonje. Na akifika huko, moja kwa moja atageuka kuwa teja. Simuombei afike huko, ila kwa mwendo wake wa kuigaiga, sitashangaa siku nikisikia Diamond anavuta madude.
Na Luqman Maloto
Ndimi Luqman Maloto