Kusema ukweli kabisa zamani nilikuwa simuelewi kabisa Mdee. Ila kwa sasa huniambii kitu kuhusu huyu binti wa shoka komando kabisa.
Kwanza anajiamini na ana akili nyingi sana huyu binti. Nimegundua hili kupitia hili suala linaloendelea la kuvuliwa uanachama na Ubunge.
Baada ya makamanda uchwara kupotoshwa jana kuhusu kesi yake, Mdee anaendelea kuwacheka tu jinsi wasivyojua Wala kuelewa chochote kuhusu sheria.
Mdee anakwambia hawezi kutishwa na mbwa anaowafuga mwenyewe. Hili ni dongo kwa makamanda uchwara wote






.
Nami naungana nae, unatishwaje na mbwa unaowafuga? Chama kakikuza, kakipigania, kakipandisha hadhi, kawapa umaarufu wanachama humo halafu leo mje kumtisha?
Ikiwa tuna Rais wetu mwanamama wa shoka SSH, hivyo naona wazi Mdee ana nafasi kubwa pia ya kuwa mwenyekiti kwenye hiko chama.
Mdee shikilia hapohapo hadi waombe poo
#kazi inaendelea#
View attachment 2270753