Mdee, Bulaya, Jacob, Kileo, Mwago na Asenga Wanashikiliwa Polisi Sitakishari, wadaiwa kufanya fujo Segerea

Jee mnahakika huyo anayewaagiza hayo ni rafiki kweli wa jamii yenu? Akili zenu zinafanya kazi au ni just like machine tuu?
Wabunge kama Halima na Bulaya wakiwa na viongozi wengine wanaenda kumpokea kiongozi wao mkuu toka gerezani kitu gani kinawafanya muwakamate kuwapiga na kuwadhalilisha?
Mbona juzi Polepole na magari yao wameingia hadi ndani kutaka kumteka Msigwa na hakuna lililofanyika?
Hamjui mna karibisha balaa katika familia zenu? Ona sasa katika mitandao jina la askari aliye mpiga mtama Bulaya hadi kuzimia linatangazwa huku ikielezwa mkewe anapatikana gereza LA Keko eneo gani analo uza chapati. Jee hapo hajahatarisha maisha ya mkewe na watoto?
Polisi nao huko Sitaki Shari wanawatendea wabunge hao waliopigania huduma bora za nyumba, posho na uniform kama adui zao jee hiyo nayo akili?
Mnajazwa uccm vichwani hadi hamjitambui ndio maana mnajikuta mnaitwa div 4 failure!
Jipimeni kama mnastahili kuendelea kuhesabika kama MNA weledi.View attachment 1387545

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyo ni kmgm siyo documents za serikali. Huna cha kumfanya mbaya zaidi umejulikana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamani matatizo mengine ya kujitakia
Halafu unakuta wapuuzi wengine wanalaumu jeshi la polisi, hii ilikua wazi kabisa walienda kutafuta shari. Hizi siasa zilipitwa na wakati. Hawawezii kuitoa CCM kwa namna hii. Hii michango imewapa kichwa sasa, tutaona mengi na wao wataonja rungu nyingi.
 
Chadema mnapotaka kutupeleka siko, utafanyaje mkusanyiko ndani ya eneo la gereza? Mkusanyiko wenu wa kumpokea mwenyekiti wenu ulitakiwa ufanyike nje kabisa ya eneo la gereza. Ndani ya eneo la gereza kuna sheria zake unazotakiwa kuzifuata. Hata Marekani kuna maeneo kwa mfano area 51 mtu yeyote asiyehusika haruhusiwi kupita au kuingia ndani ya eneo na ukiingia unapingwa risasi.
 
Hizo nchi mnazosikia zina vita vya wenyewe kwa wenyewe zilianza hivi hivi.
Huu uonevu mpaka lini?
Kwanini nchi haina wazee wa kuwakemea watawala wanapokosea?

Haya mambo yataendelea hivi mpaka lini?

Wanadhani wanajifurahisha ila wanalea mimba na kitakachozaliwa kitawamaliza wengi.

Wakati ni sasa wa kujisahihisha before it is too late.

Mungu ibariki Tanzania.
Si mnataka shotcut na kick? Maumivu mnastahili.
 
Yote kwa yote tunaambiwa ilikuwa ni makosa makubwa sana viongozi au watu wa CDM kuwepo karibu na gereza na hata kuingia.

Sasa tupate pia majibu huyo Polepole wa CCM alienda pale kufanya nini? Na kama nani na ilikuwa halali kwa hoja zipi?

Raia tunafanywa kama vile tuna akili za kuvukia barabara tu!


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom