Babati: Viongozi wa CCM wilaya ya Babati wamshamburia askari Polisi kwa mateke na fimbo, kisa tu kuulizwa kibali cha mkutano

Kamanda Asiyechoka

JF-Expert Member
Sep 13, 2020
3,166
4,581
Viongozi CCM mbaroni kwa kumjeruhi Askari Polisi

KATIBU wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilayani Babati Filbert Mdaki (52) na Katibu wa Jumuiya ya Vijana UVCCM wa Wilaya hiyo, George Sanka (46) wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumpiga Askari Polisi mateke na fimbo.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara, Benjamin Kuzaga, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, ambapo amesema kuwa tukio hilo lilitokea Desemba 16 majira ya saa 11 jioni katika kijiji cha Kirudiki wilayani Babati.

Kamanda Kuzaga amesema watuhumiwa hao walimshambulia Koplo Baraka wa Kituo kidogo cha Polisi Kiru kwa mateke na fimbo baada ya kufika kwenye mkusanyiko wa wananchi wa Kijiji cha Kirudiki.

Askari huyo baada ya kuona mkusanyiko alifika ili aulizie juu ya kibali cha mkusanyiko huo, ndipo viongozi hao wakamshambulia maeneo mbalimbali ya mwili,” amesema kamanda Kuzaga.

Amesema uchunguzi wa tukio hilo unaendelea na ukikamilika watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani.
IMG_20211221_162812.jpg


Chanzo cha Habari IPP Media
 
Back
Top Bottom