Mdee aonya Rushwa ndani ya CHADEMA!

sirluta

JF-Expert Member
Nov 28, 2012
6,325
2,486
Hizi ni habari toka gazeti la Nipashe ambapo amekaririwa mbunge Halima Mdee akionya juu ya rushwa ndani ya Chadema.

Halima Mdee ameweza kuona tatizo la Rushwa ndani ya Chadema lakini viongozi wa juu wakijisifu kuwa chama chao hakina tuhuma za rushwa. Rushwa ni adui wa haki, kuna rushwa ya ngono, na rushwa ya fedha. Hizi ni aina kubwa za rushwa zinazotumika maeneo mengi hususani kujipatia madaraka, kazi, huduma, n.k

Hongera H. Mdee kwa kuliona tatizo la rushwa ndani ya chadema. Wewe kama mwanamke unajua ni rushwa zipi ulikumbana nazo katika nafasi uliyoshinda kati ya hizo nilizotaja hapo juu.

ILA UKIWA CHADEMA UKISEMA UKWELI, UTAITWA MSALITI! HAPO MDEE SIKU SI NYINGI ATAITWA MSALITI KAMA KINA ZITTO NA MWIGAMBA!

Tuungane wote, tupambane na adui wa haki, rushwa popote tulipo.
==================================================


mdee2-sept13-2014.jpg

Mwenyekiti mpya wa Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA), Halima Mdee

Mwenyekiti mpya wa Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA), Halima Mdee, amewaonya watu aliopambana nao kugombea nafasi hiyo kuwa rushwa kwenye chaguzi itakifanya chama kisiwe na mamlaka ya kuwanyooshea vidole CCM.

Mdee ambaye alitangazwa kushika nafasi hiyo jana, alijigamba kuwa ushindi huo ni ujumbe mzito kwao kuwa kupambana kwenye siasa ni kutumia hoja na sio maneno ya fitina, majungu ambayo yalikuwa yakisambazwa baina ya viongozi.

Katika uchaguzi huo, Mdee ambaye pia ni Mbunge wa Kawe aliibuka kidedea kwa kupata kura 165 huku aliyemkaribia kwa kura ni Janeth Rote aliyepata kura 35, Sophia Mwakagenda (18), Chiku Abwao (15), Lilian Wasira (11) na Rebecca Magwisha (4).

Katika nafasi ya Makamu mwenyekiti Bara, imeenda kwa Hawa Mwaifunga huku ile ya Makamu mwenyekiti Zanzibar imechukuliwa na Hamida Abdallah.
Akizungumza mara baada ya kutangazwa mshindi katika uchaguzi huo uliofanyika usiku kucha, Mdee alisema kuwa kampeni ilikuwa na mambo mengi huku akitaja rushwa kutumika.

“Rushwa zimetembea lakini unalala kwa mtoa rushwa unaamka kwa mtu safi, tukiyaishi haya maisha tutasonga mbele, tusiruhusu utamaduni wa rushwa wa CCM, tukiruhusu hatuna mamlaka ya kuwanyooshea vidole chama tawala,” alisema.
Kuhusu maneno ya fitina ma majungu, Mdee alisema kwa walioanza siasa siku nyingi, wameyazoea kutoka chama kingine lakini sio kwa wanawake.

“Wanawake tutasonga mbele na kuleta maendeleo kama tu tutapendana kwa sababu nia na uwezo tunao, Chadema kinasema mwaka huu ni wa wanawake, wanaweza kuleta mabadiliko katika nchi, CCM inabaki madarakani kwa sababu inamtumia mwanamke kama kipaji,” alisema.

Aliongeza kuwa, siri ya Chadema kuingia Ikulu mwaka 2015 au 2020 ni wao wanawake kwa sababu hawawezi kusaliti.

Katika hatua nyingine, mwenyekiti huyo mpya alisema wakiamua kuweka miguu chini Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT), Sophia Simba atakuwa chali. “CCM hawawezi kupiga mzigo bila posho wakati Chadema tunaweza,” alisema.

Kuhusu nafasi hiyo mpya, amewaahidi mara baada ya chaguzi zote kukamilika ataanza ziara mikoani lengo likiwa ni kuhamasisha wanawake.
Katika uchaguzi huo, waliochaguliwa nafasi ya wajumbe baraza ni Suzan Mgonokulima, Marietha Chenyenge, Restuta Njotcha na Janeth Mjugu wakati baadhi ya wajumbe wa mkutano mkuu waliochaguliwa ni Khadija Omary, Janeth Joseph, Aisha Juma, Zena Abdallah na Doroth Katabazi.

Nafasi ya wajumbe wa mkutano mkuu Zanzibar ni Asha Ahmed, Levina Phabian, Khadija Juma, Riziki Juma na Raya Ibrahim Hamis.

Katika uchaguzi wa Baraza la Vijana Chadema (Bavicha) nafasi ya katibu Mkuu imechukuliwa na Julius Mwita, Mratibu Uhamasishaji ni Edward Simbeye, Naibu Katibu Mkuu Bara, Getrude Ndibalema, na Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Omari Othman Nasoro na Mweka Hazina Evarine Meena.
SOURCE: NIPASHE
 
Hizi ni habari toka gazeti la Nipashe ambapo amekaririwa mbunge Halima Mdee akionya juu ya rushwa ndani ya Chadema.

Halima Mdee ameweza kuona tatizo la Rushwa ndani ya Chadema lakini viongozi wa juu wakijisifu kuwa chama chao hakina tuhuma za rushwa. Rushwa ni adui wa haki, kuna rushwa ya ngono, na rushwa ya fedha. Hizi ni aina kubwa za rushwa zinazotumika maeneo mengi hususani kujipatia madaraka, kazi, huduma, n.k

Hongera H. Mdee kwa kuliona tatizo la rushwa ndani ya chadema. Wewe kama mwanamke unajua ni rushwa zipi ulikumbana nazo katika nafasi uliyoshinda kati ya hizo nilizotaja hapo juu.

Tuungane wote, tupambane na adui wa haki, rushwa popote tulipo.

Mkuu acha watu wajisomee wenyewe ili waelewe zaidi kuliko ulivyoelewa wewe mwenyewe. Misinterpretation!!!!
 
Bavicha, Bawacha viongozi ni Wanawake. Akija tena Mbowe hapo kuwa bosi wao' safu ya ma-first lady inakamilika. Wanachama mjipange kisaikologia!
 
Chadema wakishashikwa makalio na post kama hizi wanakimbia kujificha kama popo! Ila popo hao wakiamshwa, watatukana hadi kuchwee... Rushwa hasa ya ngono imetawala cdm!
 
Back
Top Bottom