Mdahalo wa wagombea Urais kufanyika Oktoba 18, 2015

Dotto Mnzava

R I P
Mar 6, 2014
865
427
Wakuu,

Leo waandaaji wa mdahalo wa Mkikimkiki 2015 wamekutana na waandishi wa habari kuzungumzia suala la wagombea urais kukubali kushiriki midahalo yao.

Mkurugenzi wa Twaweza, Aidan Eyakuze, amesema kumekuwepo juhudi za asasi za kiraia na vyombo vya habari kuandaa mdahalo ya wagombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Anasema juhudi hizo zimefanywa kwa nyakati na namna tofauti ili kukidhi kiu ya Watanzania kuwapima wagombea hao kwa kuwauliza maswali muhimu kabla ya kuwapa ridhaa ya kuwaongoza.

Anaelezea kuwa kwa sasa mashirika ya CEO Roundtable Tanzania,Tanzania Media Foundation (TMF), Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA), na Twaweza wameungana katika kuendeleza juhudi za kufanikisha mdahalo huu mahsusi.

Kama kawaida anasema mdahalo huu utatoa fursa ya kipekee kwa wananchi kuuliza maswali muhimu kwa wale wanaoomba ridhaa yao ya kuwawakilisha na kuwaongoza.

Mdahalo huu pia unawapa fursa wagombea Urais kuweka wazi ajenda zao kwa nchi yetu ili wananchi wazipime. Hivyo, tunatoa fursa kwa wananchi kuwasilisha maswali yao kwa wagombea Urais kuanzia leo hadi Ijumaa Oktoba 16.

Pia anasema maswali yanaweza kuwasilishwa kwa barua pepe, ujumbe mfupi wa maneno (SMS), mitandao ya kijamii au kupelekwa moja kwa moja kwenye ofisi ya asasi yoyote iliyotajwa hapo mwanzo.

Tumevialika vyama vya siasa vyenye wagombea Urais Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na wagombea ubunge wa majimbo yasiyopungua 55, kushirikisha wagombea wao wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wamevialika vyama husika kuchukua fursa hii ya kipekee na ya kihistoria kuwaonesha watanzania kuwa wako tayari kujibu moja kwa moja, maswali ya wapiga kura, na kuonesha kuwa serikali watakayounda baada ya uchaguzi itasimama bega kwa bega na wananchi.

Mpaka sasa, vyama vifuatavyo vimethibitisha ushiriki wao: Alliance for Democratic Change (ADC), Alliance for Change and Transparency - Wazalendo (ACT-Wazalendo) na Chama Cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA).

Mdahalo wa wagombea Urais umepangwa kufanyika Jumapili tarehe 18 Oktoba 2015. Tunaendelea kuwashawishi wagombea wa vyama vilivyobaki ili wathibitishe ushiriki wao kwenye tukio hili la kihistoria. Tumetuma barua rasmi kwa vyama vyote na tunawafuatilia ili wathibitishe ushiriki wao mapema iwezekanavyo.

Hata hivyo, amesema watakutana na wawakilishi wa vyama vitakavyoshiriki Alhamisi tarehe 15 Oktoba 2015, ili kukubaliana sheria na kanuni za mdahalo.

Na watakuwa na mkutano na wanahabari kutangaza sheria na kanuni hizo kwa wananchi siku ya Ijumaa tarehe 16 Oktoba, 2015.

Mkurugenzi wa kampuni ya Compass Communications, Maria Sarungi Tsehai, amesema wamekwisha fanya mdahalo wa wagombea urais kwa upande wa Zanzibar na hivyo hata sasa wanategemea ushiriki mzuri kutoka kwa wagombea urais kwa upande wa Bara.

-Aidha, amesema wananchi wameonekana kuwa na shauku/kiu ya midahalo ya wagombea hao na kuwataka wananchi waendelee kufuatilia vipindi vya Mkikimkiki 2015 na kwenye vyombo mbalimbali vya habari bila kusahau kwenye mitandao ya kijamii.

Amesema kama wagombea urais wa CCM na Chadema hawatahudhuria kwa madai kuwa muda umewabana, wanaweza kushiriki kwa njia mbalimbali kwa kutumia "Teknolojia" ambayo inaruhusu wao wawepo katika maeneo yao na kuweza kushiriki kikamilifu mdahalo huo.

Mkurugenzi wa Tanzania Media Foundation (TMF), Ernest Sungura, amesema hadi sasa wagombea urais wa vyama vya CCM na UKAWA (CHADEMA) wanaonekana kusua sua kwa madai kuwa muda ndio unawabana.

Aidha, amesema kupitia midahalo hiyo wananchi watapata nafasi ya kuwahoji wagombea maswali ya moja kwa moja na kuwa kama kutakuwa na chama ambacho hakitamtoa mgombea wake urais hakitaruhusiwa kutuma mwakilishi.
 
Kumekucha, baada za picha za mikutano ningependa kuwasikia wagombea wakichuana live japo nimesikia wote wanaogopana! Swali liwe moja kwa wote kuepusha maswali magumu kwa mmoja maana wote wana sifa lingana kwa kuwahi kuwa watendaji serikalini kwa miaka mingi kuepuka kashfa za kununuliwa.
 
Mdahalo wa urais watuachie sisi wenyewe wananchi tunaendelea huku uraiani kwenye vinywaji, nje ya maofisi:A S-cry:, nje ya nyumba za ibada, vilabu vya pombe za kienyeji na kadhalika. Hii ndiyo midahalo ya ukweli na ambayo sio ya wapiga ramli.
 
Kama Aidan Eyakuze ndiye anayeandaa mdahalo tupa kule,

Heshima yake na TWAWEZA imeshuka sana toka aliporuhusu taaluma kuingiliwa na wanasiasa.
 
Kama Aidan Eyakuze ndiye anayeandaa mdahalo tupa kule,

Heshima yake na TWAWEZA imeshuka sana toka aliporuhusu taaluma kuingiliwa na wanasiasa.
Siyo Aidan Eyakuzepeke yake hata CEO roundtable Mufuruki ni mpuuzi kabisa, Twitter na Facebook ndio bango la Magufuri.

12112317_1639434652993904_2237204691799741069_n.jpg
 

Attachments

  • 10996083_748568535248561_6475096006624691769_n.jpg
    10996083_748568535248561_6475096006624691769_n.jpg
    49.9 KB · Views: 605
Nani unayemuamini ili Jembe Magufuli aweze kutimba na kuporomosha sera????

:lock1::lock1::lock1::lock1::lock1::lock1::lock1::lock1::lock1::lock1::lock1:

Magufuli akienda CCM itapata aibu kubwa kama SADAM NI WA KUWEIT shida yake siyo ndogo na ninaamini CCM hawawezi kuhudhuria mdahalo huo
 
Vyama vyenye mashiko bado havijaonekana, na visipoonekana watambue wanapoteza muda. Kwanza hakuna haja ya kuwa na mdahalo wananchi hatuna uwezo wa kusema mtoeni fulani labda kama wanaenda kupiga kampeni siku hiyo. Ile katiba ya warioba si mlimtukana mzee wa watu? maswali ya wananchi mnayataka ya nini sasa?. Au mnafikiria kwa kutumia makario?
 
Jamani UKAWA wameshasema wanaogopa Dana MDAHALO.eti utawaumbua mapema.mbinu zao walizoziea ni ZA ghiliba!
 
kama unaandaliwa NA twaweza pamoja NA mufuruki,ukawa hakuna haja ya kwenda NA msiende,hao wanatumika bila kificho,acheni sisi wananchi tujadiliane wenyewe kwa wenyewe, hatutaki kuona liwasa wala yeyote anaenda huki,pili,mrusha kipindi ni star TV ambao kila siku wanatutukana,hatukubaku hatukubali hatukubali
 
Back
Top Bottom